Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

ENEO LA HEKARI 2 LINAUZWA KIJIJI CHA CHETA

Eneo la hekari 2 lipo kijiji cha Cheta mkoa wa Pwani jirani kabisa na kazore magenge 20.
ni umbali wa 8km kutokea Vikindu getini linauzwa kwa Tsh. 10millions kila hekari moja.

Tuwasiliane sasa kupitia 0659 91 9292 

MKUTANO WA KAMPENI ZA VYAMA VINAVYOUNDA UMOJA WA KATIBA UKAWA VIKINDU GETINI LEO

Wakereketwa wakiwa wanasikiliza sera kutoka kwa wagombea wao.
Raia wakiwa barabarani wakimsindikiza kiongozi wao kuelekea eneo la mkutano pale vikindu getini kwa mzee bakura mwembeni.
Hapa ni eneo la mwembeni ambapo mkutano huu umefanyikia. Zaidi tembelea www.kizuritz.com

NEC YATAHADHALISHWA JUU YA UCHAGUZI MKUU 2015


Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imetahadhalishwa kuwa makini katika zoezi la kuhesabu kura pamoja na kutangaza matokeo kwenye uchaguzi ujao mwezi October 2015 ili kuepusha uvunjifu wa amani kwa Tanzania.
Yamesemwa hayo na viongozi wa makanisa ya katoliki akiwemo Askofu Anthony Banzi, ambaye ni askofu wa Katoliki jimbo la Tanga pamoja na Askofu Thomas Tarimo ambaye ni askofu Kanisa la Pentekoste jijini Tanga.

Ambapo wamesema NEC wawe huru katika kuhesabu pamoja na kutangaza matokeo ya uchagu bila uchakachuaji wowote.

HARRISON MWAKYEMBE ALIA NA EDWARD LOWASSA JANA

Mhe.Harrison Mwakyembe aongelea kuhusu sakata la Richmond kwenye mkutano wa kampeni za ccm mkoani Mbeya. 


Kiongozi huyu alikuwa Mwenyeki wa kamati teule ya Bunge ambayo ndio iliyo muondoa madarakani waziri mkuu wa zamani mhe.Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais kupitia UKAWA kwenye chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.

Mwakyembe alisema yote yaliyosemwa juu ya Lowassa kuhusu Richmond niyakweli wala si ya uhongo hata kidogo, huku Mwigulu Rameki Nchemba akiwasisitiza watanzania kuchagua viongozi waadirifu na wenye kujari matakwa ya wananchi pamoja na kusimamia mali za nchi.

UZINDUZI WA KAMPENI NA MAFUNZO YA CHAMA CHA ACT

Chama cha ACT wazalendo kimeendesha mafunzo kwa wagombea ubunge wote 219 kati ya majimbo 265 ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utendaji wa kazi zao ndani ya chama chao.

Chama hicho kinachukua nafasi ya pili kwa kuwa na wagombea wengi. Huku mhe.Zitto Kabwe akiwaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika siku ya tarehe 30/8/2015 kwenye uzinduzi wa kampeni ya chama hicho utakaofanyika kwenye viwanja vya Zakhem Mbagara.

SHULE ZAFUNGWA WAKIHOFIA KIPINDU PINDU DAR

Baadhi ya shule katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam zimelazimika kufungwa kwa mda wa wiki mbili

kwa kuhofia wanafunzi wao kuambukizwa ugonjwa huu wa kipindu pindu unaoendelea jijini hapa na kwingineko.

MOTO WASABABISHA VIFO VYA WATU 9 BUGURUNI JANA


Waungwana nimesikia hii habari muda si mrefu kutoka East Africa radio kuna familia moja imeteketea kwa moto hapo Buguruni Malapa. Watu 9 wanasemekana wamefariki kasoro baba mwenye nyumba tu.


Kwa niaba ya familia yangu nawapa Pole sana wafiwa wote na Mungu awape subra katika kipindi hiki kigumu. Wenye taarifa kamili tunaomba mtujuze.

WATU 109 WAMEPOTEZA MAISHA YAO KWA KUNYONGWA

Watu 109 wamepoteza maisha yao kwa mda miezi 8 tangu mwezi January 2015 kwenye ukanda wa nchi za Kiarabu. (Arabic State )

Watu hao wamekufa kwa kifo cha kunyongwa, eidha adharani au kwasili kutokana na ukubwa wa makosa yao, huku ikitajwa kuwa asilimia kubwa kati ya hao wengi ni wageni kutoka mataifa mbalimbali.

Report hii imetolewa na mkuu wa kituo cha haki za binadamu nchini humo, huku akisema siovyema kuuwa watu kwa kuwanyonga kama ilivyo kwenye ukanda huu wa nchi za kiarabu.

DEO FILIKUNJOMBE APITA BILA KUPIGWA.

Mgombea ubunge kupitia jimbo la Ludewa mkoani Njombe mhe.Deo Filikunjombe, amepita bila kupingwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alitoa pingamizi likashughulikiwa na kuonekana liko sahihi.

CHADEMA YAIBUA TUHUMA MPYA DHIDI YA NEC

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeibua tuhuma mpya dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kikisema kimebaini shahada zaidi ya milioni mbili za kupigia kura zinazotarajiwa kuingizwa kinyemela katika Daftari la Wapiga Kura na  kugawiwa kwa wana CCM ambao hawakujiandikisha.

Chama hicho kimedai kwamba, mbali na shahada hizo pia wakimbizi zaidi ya 70,000 mkoani Kigoma wameandikishwa katika daftari hilo kwa ajili ya kupiga kura.

Tuhuma  hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam jana mbela ya waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chadema (BAWACHA), Halima Mdee na kada wa chama hicho, Saed Kubenea.
Akizungumza katika mkutano huo, Kubenea aliwaonyesha takribani shahada 100 alizosema ndizo zitakazoingizwa kwenye dafatari hilo kinyume cha taratibu.


Shahada hizo hazina jina la mpiga kura, picha, tarehe ya kuzaliwa, sehemu na eneo alilojiandikisha pamoja na taarifa nyingine muhumu zinazowekwa kwenye shahada halali.

“Chadema tumebaini kuwepo kwa mpango wa kuingizwa kwa shahada za kupigia kura zaidi ya milioni mbili, ambazo zinatarajiwa kutumiwa na wana CCM ambao walikuwa hawakujiandikisha katika daftari la kupigia kura,” Kubenea.
“Inawezekana kabisa NEC kwa kushirikiana na CCM wamepanga kuingiza majina yao katika shahada hizi, na ndiyo maana hata kuna baadhi ya watu walikamatwa wakiwa na mashine nyumbani kwa watu,” alisema.

Kubenea alisema vitambulisho hivyo vimetengenezwa ili kuongeza kura za CCM kwa wanachama wake ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha.

“Nchi yenye idadi hiyo ya watu haiwezi kuwa  na wapiga kura milioni 23, kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Takwimu ya Taifa wanasema asilimia 60 ya Watanzania wako chini ya miaka 18, hivyo ukichukua nusu ya Watanzania milioni 45 itakuwa ni milioni 22.5 kama wote wangeingia kwenye sensa hivyo kwa tathmini hiyo nyongeza hiyo ni wizi,” alisema.

Kubenea alitoa wito kwa NEC kufanyakazi kwa uaminifu na uadilifu ili kuondokana na mipango ya kuongezwa kwa kura za watu ambao hawakujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

Kwa upande wake Halima Mdee alisema kuwa chama hicho kimepata taarifa kutoka kwa wafanyakazi wa Tume wakisema kuwa kuna wakimbizi 70,000 walioandikishwa kutoka mkoani Kigoma.

“Kuna wafanyakazi wa tume ambao ni wasamaria wema wametupatia taarifa za ndani zinazosema kuwa katika kuhakikisha ushindi unapatikana wamewaandikishwa wakimbizi 70,000 kutoka mikoa ya kigoma,” alisema.
Mdee alisema kuwa ujanja wa kutafuta kura za kupata bao la mkono imekuwa sababu ya NEC, kuchelewa kufanya uhakiki wa daftari la kupigia kura kwa mkoa wa Dar es Salaam.

NAPE ATAFSILIWA VIBAYA KWA MANENO YAKE JANA

Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, wakati wasanii mbalimbali wakitumbuiza katika uzinduzi huo, alikuwa aliwapiga vijembe vyama vinavyounda na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwamba vimebeba makapi akidai kuwa wanadhani watangia Ikulu.

Nape alikuwa akimaanisha makapi ni waliokuwa makada wa CCM ambao wamekihama chama hicho kwa nyakati tofauti na kujiunga upinzani kama  Chadema, na NCCR- Mageuzi na CUF.

Miongoni mwa makada hao walitimkia Ukawa ni waliokuwa mawaziri wakuu, Edward Lowassa (Chadema) na Frederick Sumaye (NCCR-Mageuzi).
Baada ya Lowassa kujiunga na Chadema, aliteuliwa kuwania urais akiwalisha Ukawa wakati Sumaye juzi baada ya kuhama CCM alisema amekwenda kuimarisha upinzani.

Naye Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Makongoro Nyerere, aliponda  makada wa CCM waliohamia upinzani wakiwamo Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye. ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara tangu mwaka 2007 hadi 2012, alidai kuwa Sumaye siyo mkweli kwani  alipokuwa CCM alinukuliwa akisema iwapo chama  hicho kitamteua Lowassa kugombea urais kwa  angekihama.

“Wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea urais Sumaye alisema hiki chama mkimpa Lowassa, atahama chama kwa kuwa tunamweshimu Sumaye hatukumpitisha Lowassa, lakini bado amehama na kwenda kumkumbatia fisadi,” alisema.


Alisema pale ambako mtu hazumgumzi ukweli anaitwa mwongo, hivyo kauli yake hiyo Sumaye hana tofauti na mwongo kwani katika kipindi cha miaka kumi iliyopita aliingia katika kinyang’anyiro cha urais na alifika tano bora, lakini kura hazikutosha badala yake zikatosha za Kikwete.

Alisema miaka kumi baadaye Sumaye ameingia katika kinyang’anyilo cha urais bahati mbaya hakuingia katika tano bora, lakini cha kushangaza anaanza kuishukutumu CCM kwamba ni chama kibaya 

“Mnaufahamu mchezo wa chandimu, ambao huchezwa na vijana tu na mzee akiingia akija anataka nini?alihoji na kuongeza;
“Sumaye kaingia katika mchezo huu wa chandimu mwenyewe, tutamsema.”
Mbali na Sumaye na Lowassa, wapinzani wengine waliohama CCM na kuiunga na upinzani ni wagunge waliomaliza muda wao wa Kahama, James Lembeli; Viti Maalum, Ester Bulaya; Arumeru Magharibi, Ole Medeye; Segerea, Dk. Makongoro Mahanga na wa Sikonge, Said Mkumba.

Wengine ni wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Arusha, Onesmo Ole Nangole; Singida, Mgana Msindai na Shinyanga, Khamis Mgeja pamoja Mwenyekiti wa zamani wa Dar es Salaam, John Guninita.

WARIOBA: TANZANIA INAHITAJI KIONGOZI MWADILIFU

Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema Tanzania ya sasa inahitaji kiongozi mwadilifu, mzalendo na mchapakakazi kama alivyo mgombea wa CCM, Dk John Magufuli.

Jaji Warioba akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jana Dar es Salaam, alisema Dk Magufuli ni mchapakazi kweli kweli na hana masihara anapokuwa ofisini au nje ya ofisi.

“Wote mmemshuhudia akiwa Waziri wa Maendeleo ya Uvuvi, Ardhi na sasa hivi Ujenzi, amekuwa mchapakazi na amekuwa anawaelemisha wananchi wazifahamu haki zao,”Jaji Warioba.

Dk Warioba alisema wakati alipokuwa mwenyekiti wa Tume ya Rushwa wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, alibaini kuwa sekta ya ujenzi ilikuwa inaongoza kwa rushwa, lakini tangu Dk Magufuli apewe wizara hiyo hakuna ufisadi tena.


Alisema kama Dk Magufuli angeamua kuchukua hata asilimia moja tu ya ujenzi wa Daraja la Mkapa, Daraja la Malagarasi au Daraja la Kigamboni angekuwa tajiri wa kutupa, lakini hakuwahi kujihusisha na vitendo hivyo vya kifisadi na ndio maana hana utajiri wowote.

“Tumesikia ufisadi wa EPA, Richmond, Escrow lakini hatujasikia ufisadi kwenye ujenzi na hii inadhihirisha kuwa Dk Magufuli ni mwadilifu,”Jaji Warioba.

Jaji Warioba alisema mgombea huyo wa CCM ni mkali na hapendi kazi za ovyo ovyo, lakini pia anafuatilia kwa karibu.

Alisema chanzo cha ufisadi ni kutokana na viongozi kuwa karibu na matajiri, jambo ambalo mgombea huyo hana tabia hiyo.
Alisema mgombea huyo hana makundi badala ya
ke kundi lake ni Watanzania wote hivyo akatoa mwito kwa Watanzania kumpa kura ili aweze kuwaongoza Watanzania na kuwaletea maendeleo ya kweli.

TUME YA TAIFA NEC YAWEKA HESHIMA YA KUJENGA TAIFA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeweka historia na kujenga heshima ya taifa kwa kuweza kuandikisha wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mfumo wa BVR kwa mafanikio makubwa na kuyashangaza mataifa makubwa duniani.

Katika kufanikisha hilo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) vimetajwa kuwashawishi wanachama na wafuasi wake kwa kiwango kikubwa kujiandikisha katika BVR.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kufuatilia Masuala ya Uchaguzi Tanzania (TEMCO), ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Kufuatilia Masuala ya Uchaguzi, Dk Benson Banna, alisema Dar es Salaam jana kuwa Nec inastahili pongezi kubwa kwa hatua hiyo.

Alisema utafiti uliofanywa na Temco kwa kupitia vituo 8,398 vya uandikishaji ambavyo ni asilimia 80.5 ya vituo vyote, umedhihirisha kuwa kazi hiyo ilifanyika kwa ukamilifu kwa wananchi wengi kupata nafasi ya kujiandikisha huku asilimia 64 ya vituo vikizidisha hadi muda wa kufunga katika kuwawezesha wananchi kujiandikisha.


Kwa hatua hiyo, Dk Banna alisema NEC imefuta aibu kwa Taifa, kutokana na mataifa mbalimbali ya nje kubeza uwezo wa nchi katika kufanikisha uandikishaji huo kabla ya kuanza na kwamba sasa kama Taifa, Tanzania imeanza kuonesha uwezo mkubwa wa kujitegemea katika uendeshaji wa shughuli za uchaguzi.

“Hili lazima nilisema wazi, ni aibu kwa mataifa makubwa kufadhili shughuli za uchaguzi maana kitendo hicho ni hatari kwa nchi kuweza kujiamulia mambo yake na kukuza demokrasia ya kweli, hivyo Nec wanastahili pongezi,”  Dk Banna.

Akielezea mlolongo mzima wa uandikishaji, mwanazuoni huyo alisema, Temco katika ufuatiliaji wake huo ilibaini kasoro mbalimbali ikiwemo fedha kutolewa kidogo na kwa kuchelewa hatua iliyofanya tarehe ya kuanza kwa uandikishaji kuchelewa na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Alisema pia wakati tathimini ya awali ilikuwa ni kuhitajika kwa visanduku vya BVR zaidi ya 15, 000, serikali ilikataa pendekezo hilo na kusema visanduku vinavyohitajika ni 14,000, lakini hata hivyo havikuweza kununuliwa badala yake vilinunuliwa visanduku 8,000 tofauti na ushauri wa Nec ambayo ilishauli kiwango cha chini kiwe visanduku 10,000

MHE.JOSEPH JOHN POMBE MAGUFULI AREJESHA FOMU YAKE LEO

Baada ya Lowassa kurejesha fomu ya kugombea Urais 2015 katika ofisi za NEC,  sasa ni time ya mgombea kutoka kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) , Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan.

mhe.John Joseph Pombe Magufuli akirudisha fomu akiwa na Samia S.Hassan. 

MGOMO BARIDI WA MADREVA NCHI NZIMA

Chama cha madreva wa mabasi yaendayo mikoani kimetangaza mgomo baridi kwa nchi nzima kusimamisha zoezi la kusafirisha abilia kwa siku zaidi ya tano 5 kwa madai wanaenda kuudhulia mafunzo ya usalama barabarani.

Lengo kuu la semina hiyo nikupunguza ajali za barabarani wakiwemo madreva wazembe pamoja na madreva kujua namna ya kudai haki zao ambapo baadhi ya madreva mpaka sasa hawajapewa mikataba mipya na waajiri wao.

LOWASSA ATOA POLE KWA WANA CUF SOMA ZAIDI

Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vingine vitatu vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amewapa pole wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) kwa mshituko wa kuondokewa na Mwenyekiti wao wa Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba aliyejiuzulu, huku akiwataka kutovunjika moyo, bali waongeze mshikamano ili dhamira ya kuingia Ikulu iweze kutimia.

Aidha, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ameonya kuwa, hawatamvumilia yeyote atakayeonekana kutaka kukwamisha umoja wao unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.

Lowassa aliwapa pole wanaCUF akisema endapo watatetereka, safari yao ya kuelekea Ikulu itakuwa ngumu.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wafuasi wa CUF kumsindikiza kwa wingi leo kwenda ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ya kuwania urais baadaye mwaka huu, huku akisisitiza ana imani ya kushinda.

Awali, mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Duni Haji ambaye alijiunga Chadema hivi karibuni akitokea CUF alikokuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Taifa, alisema endapo wanachama wa vyama vinavyounda Ukawa watakosea katika kupiga kura zao na kushindwa kuingia madarakani, basi watalazimika kusubiri miaka 50 ijayo ili kuingia Ikulu.

“Tusipoweza kuingia Ikulu sasa litakuwa kosa kubwa na itatulazimu kusubiri miaka 50 ijayo ili kuweza kuchukua madaraka. Vijana pekee ndio watakaoweza kuleta mabadiliko,” alisema Duni.


Akizungumzia shughuli ya kuchukua fomu leo, Lowassa aliwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kumsindikiza na kusisitiza kuwa amejiunga na Ukawa ili kutafuta mabadiliko nje ya CCM na kuwa ana imani ya kushinda kwa asilimia 90.

Lowassa alisema endapo Ukawa itashinda na kuchukua madaraka wataendesha nchi kwa utulivu na kubadilisha maisha ya Watanzania kwa kuwaondolea umasikini ambao umekuwa ukipigwa vita tangu mwaka 1962. Naye Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alisema kiongozi ndani ya Ukawa ambaye atakuwa akipingana na malengo yao kutokana na kukosa fursa binafsi, mtu huyo hafai kuwa katika umoja huo.

Alisema pamoja na umoja huo kukumbwa na misukosuko, bado wamekuwa wamoja na kutetea hatua ya wao kumteua Lowassa ambaye wiki mbili zilizopita alikuwa CCM kwa sababu ni Mtanzania. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alisema silaha pekee ya ushindi kwa Ukawa ni kuwa na umoja, ushirikiano na mshikamano na kuwa ana uhakika Lowassa atashinda, sambamba na yeye kwa upande wa Zanzibar.

ADAM KIMBISA AKANUSHA HABARI YA KUAMA CCM


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amekanusha uvumi kuwa ameungana na wenyeviti wengine wa mikoa wa CCM kukihama chama tawala nchini. Amesema wanaomzushia washindwe na walegee, kwani moyo na mwili wake upo CCM na kwamba kamwe hawezi kuhama.

Aliyasema hayo jana mjini hapa kutokana na kuwapo kwa taarifa amekihama chama hicho. Awali, jana kulikuwa na taarifa za Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo ole Nangole kuhamia Chadema, kama ilivyokuwa kwa Mgana Msindai, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida aliyetangulia Chadema wiki iliyopita baada ya kushindwa kura za maoni ndani ya CCM.

Katika kuthibitisha hayo, Kimbisa jana alikuwa akiendesha vikao vya Kamati ya Siasa ya Mkoa akiwa katika sare zake za chama. Taarifa hizo zimekuja huku Kimbisa akiwa na habari nyingine katika gazeti hili (ukurasa wa 21) akielezea kushangazwa na wanaokihama chama baada ya kushindwa katika michakato ya kuwania uongozi, huku akisema kamwe yeye hawezi kufanya hivyo.

“Mwaka 2010 niligombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini nikahesabu kura zangu mwenyewe nyumbani nikajiona nimeshinda nikalala, asubuhi nilipoamka kumbe wagombea wenzangu wakaunganisha matokeo yao mgombea mmoja akaonekana ameshinda, lakini bado sikuhama na hadi leo nina damu ya kijani.

“Mtu akihangaika kuondoka CCM baada ya kushindwa tutamfuata hukohuko na tutampiga kwa kura tu,” alisisitiza Kimbisa.


JOTO LA KUWAPATA WAGOMBEA UBUNGE CCM KUPANDA


Joto la uteuzi wa mwisho la kupata wagombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) limezidi kupanda, huku chama hicho kikitangaza uamuzi mgumu kwa wagombea waliocheza rafu na hata kupindua matokeo.

Mbali na hayo, viongozi wa ngazi ya wilaya na mikoa wanaodaiwa kuwabeba kinyume na utaratibu nao wapo hatarini kuvuliwa nyadhifa zao.

Taarifa kutoka ndani ya CCM ilisema kuwa kikao cha Sekretarieti kilichokutana mjini hapa, kilijadili baadhi ya taarifa na rufaa za wagombea, huku wengine wakiwalalamikia wenzao pamoja na viongozi kwa kucheza rafu wakati wa uchaguzi wa kura za maoni.

Miongoni mwa jambo ambalo limekuwa likizua mjadala, ni hatua ya baadhi ya wabunge kupata kura nyingi katika maeneo yao kinyume na idadi halisi ya wanachama wa CCM kwenye jimbo husika.

Moja kati ya majimbo ambayo wagombea walilalamikia hatua hiyo, ni Jimbo la Iramba ambapo Juma Kilimbah ambaye alikuwa ni moja ya wagombea, alisema pamoja na kura kupigwa bado kura alizopata mgombea mwenzao, Mwigulu Nchemba ni tofauti na idadi ya wapiga kura.

Alidai wakati wa mchakato huo, baadhi ya viongozi wa CCM akiwemo msimamizi wa uchaguzi, walikuwa wakigawa kadi kinyume na utaratibu kwa lengo la kumwezesha Mwigulu kushinda.

MWENYEKITI NA KATIBU WA CCM WAJIUNGA NA CHADEMA

Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa huo, Isack Joseph, wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ole Nangole na Joseph walifikia uamuzi huo jijini hapa jana na kusema kwa nyakati tofauti wamelazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa utaratibu wa kumpata mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulikiukwa.

Kwa mujibu wa wana CCM hao, wakati wa mchakato huo baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho walikuwa na wagombea wao mifukoni waliotaka wagombee nafasi hiyo.

Ole Nangole aliyejiondoa CCM akiwa kwenye kipindi cha awamu ya pili cha uenyekiti wake, alisema alijiunga CCM mwaka 1977 ambapo alifanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali zikiwamo mwenyekiti wa CCM wilaya kwa miaka kumi.

“Ndugu zangu waandishi wa habari nimewaita leo kuwaambia jambo moja kwamba ninahama CCM kuanzia sasa. Najiuzulu nafasi yangu ya mwenyekiti niliyoitumikia kwa miaka saba na ninajiunga na Chadema kuanzia sasa.

“Nashindwa kuwa na moyo wa chuma wa kuendelea kuwa ndani ya CCM kwa sababu CCM niliyoifahamu tangu enzi za TANU siyo hii ya sasa.

“Kuondoka kwangu kumechangiwa na kikundi cha viongozi wachache kuiongoza CCM kwa mabavu, nguvu na kwa kutumia fedha walizokwapua serikalini.

“Miaka yote tangu nilipojiunga CCM mwaka 1977, sikuwahi kukiona chama hiki kikiendesha mambo yake bila kufuata kanuni na taratibu za vikao kama kilivyofanya wakati wa vikao vya kupitisha mgombea urais mjini Dodoma hivi karibuni.

“Mkutano mkuu wa CCM uliongozwa kwa kukiuka haki na misingi kwa wanachama kwani hata nyinyi mtakumbuka kulikuwa na mchakato wa urais na wagombea 40 walijitokeza akiwamo Edward Lowassa.

“Kwa mapenzi yake Lowassa alivyokitumikia chama na Taifa, wananchi tuliamini mchakato ule kama jina lake lisingekatwa angekuwa mmoja wa wagombea ambao wangefika mbali ndani ya chama.

“Lakini jina lake lilikatwa bila sababu japokuwa sababu tulizijua tangu alipotoka kwenye uwaziri mkuu kwa vile kuliendelea kusambazwa maneno na hujuma za kisiasa dhidi yake kupitia kwa viongozi wa chama na Serikali wakiwamo vijana wadogo waliopewa fedha na madaraka ili wamchafue,” alisema Ole Nangole.

Kwa upande wake, Joseph alimnyooshea kidole Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kumtaka achunge ulimi wake pindi anapowaita Watanzania makapi ndani ya nchi yao.

Joseph ambaye ni Diwani wa Kata ya Monduli Mjini aliyemaliza muda wake na kupita bila kupingwa ndani ya CCM, alisema hakuna Mtanzania aliye makapi kwani wote wana haki ya kidemokrasia ya kuhama vyama kwa jinsi watakavyoona inafaa.

“Watasema mengi na tumeondoka watatuita makapi. Naomba niwaambie, sisi siyo makapi, wakitaka tuzungumze suala la makapi hao wanaosema hivyo wao ndio makapi halisi.

“Sisi Watanzania si makapi kwani tukichambuana kwa suala la makapi na kuangalia wewe umetokea wapi, tutakwenda kusiko. Kwanza aliyesema hiyo kauli yeye ni Msomali. Hivyo tukisema nani ni makapi yeye ndiye makapi halisi anayeishi Tanzania kwani asili yake ni Somalia,” alisema Joseph.

Joseph alitoa kauli hiyo zikiwa ni siku chache baada ya Kinana kunukuliwa na vyombo vya habari akisema wanachama wa CCM wanaohamia Chadema ni makapi.

LIPUMBA ASEMA CCM INA WAGOMBEA URAIS WAWILI

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kina wagombea wawili wanaowania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Madai hayo mapya ya Profesa Lipumba yametolewa siku tatu baada ya kujiuzulu uenyekiti CUF, akisema hiyo ni moja ya sababu za kuachia nafasi yake kutokana na uamuzi uliofikiwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuhusu mgombea urais.

Profesa Lipumba alisema dhamira yake ilikuwa inamsuta kwa kuwaingiza ndani ya Ukawa watu kutoka CCM, waliokuwa wanapingana na maoni ya wananchi kuhusu rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba na kuwapa fursa ya kuwania urais.

Juzi usiku katika mahojiano aliyoyafanya na Azam TV kutoka Kigali alikosema anafanya utafiti, Profesa Lipumba alisema kumpa nafasi waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa kuwania urais kupitia Chadema ndani ya Ukawa, ni sawa na CCM kusimamisha wagombea wawili (Lowassa) na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli.

Katika mahojiano hayo ya simu, Profesa Lipumba ambaye wiki mbili zilizopita alimpokea Lowassa akisema ni mtu safi na kwamba, ufisadi ndani ya CCM ni mfumo  alisema katika kujiuzulu kwake hakutumiwa na CCM kuparaganyisha Ukawa, bali walikuwa tayari wameparaganyika.

“Ukweli ni kwamba tumejiparaganyisha wenyewe ndani ya Ukawa. Kwa hiyo Watanzania watakuwa na wanaCCM wawili wanaogombea urais wakati Ukawa tulikuwa na wagombea watatu… mimi, Dk Willibrod Slaa, (Katibu Mkuu wa Chadema) pamoja na Dk George Kahangwa (NCCR-Mageuzi) ambaye alikiri kuwapo makubaliano hayo.

“Tulikutana nyumbani kwangu tukakubaliana Dk Slaa apeperushe bendera ya Ukawa, lakini tumewekwa kando,” Prof. Lipumba.
Alisema yupo Rwanda kwa muda na anafanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa kiuchumi. Pia alisisitiza kuwa hajahama nchi na kwamba wiki hii anatarajia kurejea nchini.

KAMA HAUNA KAZI MAARUMU USIENDE MJINI, SOMA HII

Muda mfupi uliopita kupitia kituo cha ITV kwenye taarifa ambazo zimetolewa na kituo hicho zinasema kuwa Jeshi la Polisi Tanzania limekataza Maandamano ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa wakati akienda kuchukua fomu ya kugombea Urais.
Capture 
Edward Lowassa leo anaenda kuchukua fomu ya ugombea Urais kwenye makao makuu ya NEC ambapo kwenye taarifa yake iliyotolewa na vyombo vya habari jana aliomba wanachama wa Ukawa kujiunga nae wakati wa kwenda kuchukua fomu hiyo.

SASA THIERRY HENRY AJIBU SWALI LA WANA ARSENAL

Klabu ya Arsenal ya Uingereza ambayo ipo katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anaekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema, dalili za Arsenal kuongeza nguvu ya kumtaka mshambuliaji huyo zinazidishwa na kauli ya mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo Thierry Henry.
169219
Thierry Henry
Arsenal imefanya usajili mkubwa mmoja tu katika majira haya ya usajili kwa kumsajili aliyekuwa kipa wa Chelsea Peter Cech lakini Henry anaamini kama itamsajili Benzema inaweza kurudi katika mbio za kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza toka ishinde taji hilo msimu wa 2003/2004.
thierry-henry-20051118-85377
Thierry Henry
“Nafikiri wanaweza fanya vizuri mwaka huu kama hawatakuwa na majeruhi, Giroud pekee kama mshambuliaji huwezi shinda taji, unahitaji aina nyingine ya mshambuliaji  nafikiri Giroud anafanya vizuri kiukweli ameshinda magoli 14 katika mechi 18 hicho ni kitu kizuri sana”>>>Henry
“Lakini wakati mwingine unahitaji aina tofauti ya mshambuliaji na nafikiri huenda watampata Benzema bado wapo katika nafasi ya kuwania taji la Ligi Kuu na Ligi ya mabingwa “>>>Henry
Karim-Benzema-Net-Worth
Karim Benzema
Licha ya kukiri Arsenal ipo vizuri na inahitaji kujiimarisha kwa kumsajili Benzema lakini amekubali wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kama watafanya hivyo ila la Ligi ya Mabingwa ni ngumu kushinda taji hilo.

WAFANYAKAZI WA TAZARA WALIPWE MISHAHARA YAO

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), hawajalipwa mishahara ya miezi mitatu kati ya miezi sita waliyokuwa wakiidai mamlaka hiyo.

Wafanyakazi hao hawajalipwa mishahara ya Januari, Juni na Julai, mwaka huu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), Patrick Nyakeke, alisema baadhi ya wafanyakazi hawajalipwa mishahara ya kuanzia Januari hadi Mei, mwaka huu



“Wafanyakazi zaidi ya 1,500 bado hawajapewa mishahara ya miezi ya Januari, Juni na Julai huku wengine wakiwa wanaudai uongozi wa Tazara mishahara ya miezi mitano pamoja na malimbikizo mengine,” Nyakeke.
Aidha, alisema mishahara ya Januari na Juni, mwaka huu, utalipwa na Menejimenti ya Tazara na wa Julai mwaka huu, unatarajiwa kulipwa kupitia Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ya 2015/16 iliyotengwa na serikali.

Hata hivyo, alisema baada ya wafanyakazi kuuhoji uongozi wa mamlaka hiyo kuhusu suala hilo, walielezwa kuwa watalipwa mishahara na malimbikizo ya fedha za likizo kupitia makusanyo ya Tazara ya Januari hadi Julai, mwaka huu.
Nyakeke alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo, serikali imetenga Sh. bilioni 30 ili kuhakikisha wafanyakazi wanaondokana na adha ya kusotea mishahara.

BUNDUKI 16 KATI YA 21 ZA STAKISHARI ZIMEKAMATWA

Jeshi la Polisi limesema limeshakamata bunduki 16 kati ya 21 zilizoporwa kwenye Kituo cha Stakishari. Bunduki hizo ziliporwa Julai 12 wakati watu wanaoaminika kuwa ni majambazi walipovamia kituo hicho cha polisi, Ukonga – Dar es Salaam na kuua askari wanne na watu wengine watatu.

Jana, Naibu Kamishna wa Kanda ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari kuwa zaidi ya majambazi 10 wameshakamatwa na polisi wanaendelea kuwahoji kuhusu tukio hilo.


“Silaha zilizokuwa zimebaki ni tano, 16 zimeshakamatwa na hizo tano ndizo tunafanya bidii ya kuzipata. Niwahakikishieni kuwa zitapatikana,”  Sirro.
Alisema watuhumiwa waliovamia kituo hicho walikuwa zaidi ya 15 na walitumia mbinu mpya ambayo Polisi hawakuitegemea.

Wakati huohuo; Jeshi la Polisi limewakamata watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya ofisa wa Polisi, Elibariki Palangyo yaliyotokea nyumbani kwake Yombo Kilakala, usiku wa Agosti.

Katika tukio jingine, polisi inawashikilia watu wanne wakituhumiwa kukutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh30 milioni juzi, saa 1.30 usiku huko Tandale kwa Mtogole.

MKE WA DK.WILLLIBROAD SLAA AKANUSHA YALIYOSEMWA

Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuzungumza na kusema yupo salama, mke wake, Josephine Mushumbusi amekanusha tuhuma zilizozagaa kuwa ndiye aliyemshauri kiongozi huyo wa Chadema kujiuzulu na kumzuia kushiriki vikao muhimu vya chama.

Tetesi hizo zilivuma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya Dk Slaa kutoonekana katika vikao muhimu vya Chadema na Ukawa, kuwa Mushumbusi hakupendezwa na kitendo cha Lowassa kupitishwa kuwania urais chini ya mwavuli wa Ukawa na badala yake alitaka Dk Slaa ndiye awe mpeperusha bendera.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo Mushumbusi amezikanusha, aliamua alimfungia ndani Dk Slaa kama moja ya mbinu za kumzuia asishiriki shughuli za kichama, tuhuma ambazo amezikanusha.

“Bosi wako akija kukuomba ushauri utamsaidia, lakini akija akakuambia ameshafanya maamuzi unaweza kupingana naye?” alihoji Mushumbusi akianza kutoa maelezo yake na kuendelea: “Wakati wa vikao nilikuwa namwona (Dk Slaa) anachelewa kurudi kila siku, siku moja akaja akaniambia uamuzi aliouchukua na mimi sikuwa na la kusema, nikachukua shuka nikajifunika.”

Katika mahojiano yake ya kwanza na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa tetesi hizo, Mushumbusi pia alikana kumfungia Dk Slaa ndani ya nyumba, akisema wakati maneno hayo yalipokuwa yanazagaa, alikuwa nje ya nchi na wala hakujua kinachoendelea.


“Mwenyewe najiuliza nini kinaendelea, siwezi kufanya kitu kama hicho. Nyumba yangu ina milango miwili, nawezaje kumfungia mtu, tena mwanamume, hata watoto siwezi kuwafungia. Kuna mambo mengine mwanamke huwezi kuyafanya kwa mwanamume. Mwanamume ni mwanamume tu,” alisema.

Alisema viongozi wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wanafika nyumbani kwake na walikutana na Dk Slaa na kuzungumza naye… “Kama ningekuwa nimemfungia wangezungumza naye vipi?”

Mushumbusi alisema mwanamke anaweza kufanya chochote lakini kuna baadhi ya mambo ambayo mwanamume akiamua ni vigumu kumzuia. Akifafanua tuhuma za kumshinikiza Dk Slaa kujiuzulu Chadema, Mushumbusi alisema kiongozi huyo wa Chadema ana uamuzi wake na yeye ni msaidizi tu ambaye hana uamuzi wa mwisho kwenye familia.

Hata hivyo, alisema endapo angeamua kumshawishi, uwezo wa kufanya hivyo anao lakini yeye ni mwanamke mwadilifu anayependa mafanikio ya mumewe.
“Kwani unanionaje? Mimi ni ‘strong’ (nina nguvu), ningetaka ningefanya hivyo, nisingeshindwa,” alisema.

Pamoja na hayo, Mushumbusi alilalamika kuwa tuhuma hizo dhidi yake zimesababisha asisikilizwe kama ilivyokuwa awali. Bila kufafanua kwa undani, alisema kuna kundi linalounda propaganda hizo ili abadili mtazamo kuhusu mumewe lakini jambo hilo haliwezi kutokea.
 
“Nilisema nitampenda kama alivyo, sitajali chochote wala akiwa katika hali gani au chama gani. Kazi yangu ni kumtia moyo ili kile atakachofanya kifanikiwe,” alisema. Mbali na kukanusha vikali tuhuma hizo, Mushumbusi alisema alikwishajitoa kwenye masuala ya siasa kwa miaka miwili sasa na badala yake ameamua kufanya biashara ya kuuza mkaa.

UVCCM ZANZIBAR WASEMA CCM ITASHIKA DOLA OCTOBER

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) upande wa Zanzibar, umesema unaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete kwamba CCM imejiandaa kushinda na kushika dola kwa sababu inao uzoefu wa kuongoza nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya UVCCM eneo la Gymkanna mjini hapa, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka alisema hotuba iliyotolewa na Mwenyekiti huyo wa CCM wakati wa kuwapokea wagombea wa chama hicho kuchukua fomu kutoka Tume ya Uchaguzi NEC katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, imewavunja moyo wapinzani kwa kiasi kikubwa.

Shaka alisema CCM haibabaishwi na uamuzi wa kuhama kwa waliokuwa viongozi wake mbalimbali kwani tangu mwaka 1957 wakati wa harakati za kudai uhuru viongozi wa vyama vya TANU na ASP walikuwa wakihama vyama hivyo na kwenda upinzani.

“Tunaipongeza hotuba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewaambia ukweli wapinzani kwamba CCM imejiandaa kushinda katika uchaguzi mkuu kwa sababu inao viongozi safi wenye uwezo wa kuongoza dola,” alisema.


Aidha Shaka alitumia nafasi hiyo kusema kwamba UVCCM ipo imara huku ikiwaunga mkono wagombea wa CCM wa nafasi mbali mbali ikiwemo ya urais wa muungano.

Alisema umoja wa vijana katika mchakato wa wagombea wa nafasi ya urais wa muungano haukuwa na mgombea unayemuunga mkono, isipokuwa wanachama wenyewe walikuwa huru kutafuta mgombea wanayeona anafaa.

“Mchakato wa kuwania nafasi ya urais wa muungano umemalizika na sasa tunaye mgombea John Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu. Hao ndiyo wagombea tunaowaunga mkono UVCCM katika harakati za kuwania urais wa muungano,” alisema.

Alisema mgombea aliyepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM, John Magufuli pamoja na mgombea mwenza Samia Suluhu ni viongozi wenye uwezo mkubwa wa kuongoza nchi ambao walipata kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi

NANI RAIS, MBUNGE, DIWANI MWAKA HUU OCTOBER 25?

Wakati joto la uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu likizidi kupanda, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeviagiza vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa kisheria, kutoendesha kampeni zao katika nyumba za ibada.

Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega alipozungumza na waandishi wa habari jana katika Ofisi ya Tume hiyo mjini hapa. Alivitaka vyama hivyo kuzingatia maadili kama ilivyokubaliwa na vyama vyote 22 na ambayo viongozi wake waliridhia na kusaini mbele ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mbali na nyumba za ibada, NEC pia imeviagiza vyama hivyo vya siasa, kutoendesha kampeni zao katika taasisi za umma kama vile vyuo vikuu.
Kwitega alisema NEC ni chombo huru, ambacho hakifungamani na chama chochote cha siasa na kwamba jukumu lake ni kusimamia kwa uadilifu wa hali ya juu masuala ya Sheria za Uchaguzi nchini.


Mbali na nyumba za ibada na taasisi za Serikali, pia alivitaka vyama vya siasa kuepuka kutumia lugha za matusi kejeli na kashfa wakati wa kampeni, huku akivihimiza kunadi sera zake mbele ya wananchi pamoja na yale ambayo chama husika kimetekeleza ama kinatarajia kutekeleza.

Alisema NEC itasimamia maadili ambayo yamekubaliwa na vyama vyote vya kisiasa vyenye usajili wa kudumu. Aidha, Kwitega alivitaka vyama vya siasa kutowatumia viongozi wa madhehebu ya dini, kuendesha kampeni zao katika madhehebu yao.

Alisema kwamba maeneo ya ibada ni kwa ajili ya kuabudu, sio kuendesha kampeni za kisiasa. Pazia la kampeni kwa vyama vyote, zinazotarajiwa kufanyika kwa miezi miwili, linatarajiwa kufunguliwa Agosti 22.

HABARI KUU KUTOKA MAGAZETINI IKIWA NI AUGUST 7



Magazeti ya Ijumaa 7 August 2015 yako mtaani tayari na vichwa vyake vikubwa vya habari, kazi yangu ni kukusogezea zile zote zinazoweka headlines magazetini… baadhi zikiwa na hizi kubwa kubwa.

Prof. Ibrahim Lipumba ango’ka hali tete UKAWA, ajiuluzu uwenyekiti wa miaka 16 CUF akimpinga Edward Lowassa adai UKAWA washindwa kuenzi uadilifu na uzalendo.

CCM kupitisha wagombea Ubunge leo…Edward Lowassa aipasua vipande UKAWA…NEC yaonya kampeni nyumba za ibada…Siri yafichuka CUF watoa taamko…na mke wa Dk. Wilbroad Slaa afunguka.

UKAWA wapata mtikisiko mkubwa baada ya Prof. Ibrahim Lipumba kujiuzulu uwenyekiti wa chama cha CUF na kuamua kubaki kuwa mwanachama wa kawaida wa Chama hicho…idadi ya Wabunge 51 waanguka kura za maoni ndani ya vyama vyao.

Zaidi ya majambazi 10 waliohusika na tukio la Sitakishari wakamatwa na Polisi…Wamachinga wanaendelea na ujenzi wa vibanda Jangwani pamoja na Serekali kusisitiza kuwa wanapaswa kuhama eneo hilo.


Magazeti ya leo August 7 Bofya hapa

IDADI YA WAHANDISI NCHINI TANZANIA WAFIKIA 15,364

Idadi ya wahandisi waliosajiliwa nchini imeongezeka kutoka 6,868 na kufikia 15,364 katika kipindi cha miaka 10. Kati ya wahandisi hao 15,364, wahandisi wazalendo ni 13,901 na wa kigeni 1,463.Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Steven Mrope, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi.

Mhadisi Mrope alisema katika kipindi hicho, jumla ya kampuni za ushauri wa kihandisi 279 zilisajiliwa na kati ya hizo, 201 ni ya kizalendo na 78 za kigeni.
Aidha, alisema idadi ya wahandisi washauri ni 459 ambapo kati yao, 356 ni wazalendo na 103 wageni.

“Bodi imeendelea kutembelea na kukagua hali ya uhandisi katika halmashauri zote Tanzania bara, ukaguzi huo umewezesha halmashauri nyingi kutambua umuhimu wa kuajiri wahandisi na kuwatumia katika miradi ya ujenzi,” alisema Mrope.


Alisema hiyo pia imewezesha idadi ya wahandisi katika halmashauri kuongezeka kutoka 129 mwaka 2003 hadi kufikia 508 mwaka 2015.
“Ingawa idadi hiyo ya wahandisi bado ni ndogo, lakini ni dhahiri ubora wa kazi katika halmashauri umeongezeka,” alisema.

Aliongeza kuwa Bodi imefanikiwa pia kuongeza  idadi ya wahandisi wataalam wanawake kutoka 20 waliosajiliwa mwaka 2011/12 hadi 80 waliosajiliwa mwaka 2013/14 mpaka kufikia 176 kwa sasa.

Aliongeza kuwa baada ya mabadiliko ya Sheria, Bodi imeanza kusajili mafundi sanifu ambao ndiyo wasaidizi wakuu wa wahandisi na mpaka sasa mafundi sanifu 157 wamesajiliwa. Mhandisi Mrope alisema moja ya majukumu ya Bodi ni uendelezaji wa taaluma ya kihandisi ili kufanya wahandisi waende sambamba na mabadiliko ya kisayansi na kiteknolojia.
Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top