Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

NYUMBA INAUZWA MBAGARA CHARAMBE

Ipo Mbagala Charambe Magengeni.

Nyumba ina:
✔Frems (2)
✔Vyumba (22)
✔Siting room (1)
✔Dining room (1)
✔Umeme unawaka

⏺Ukubwa wa eneo:
⏺Urefu ni mita (24.4)
⏺Upana ni mita (24.1)
⏺Ipo sehemu iliyo changamka sana
⏺Siombali na stend ya mwendokasi
⏺Bei ya mauzo ni tsh 130,000,000/=
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba
0787 94 2854

MINI SHOP CHETA

Mini ShopCheta au Duka Dogo

Ni duka dogo kweli kama jina lake linavyojieleza hapo juu. Duka hili linatoa huduma ya mahitaji ya kawaida ya kila siku kwa wakazi wa Kitongoji cha Cheta pamoja na maeneo ya jirani au kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mini Shop inatoa huduma ya jamii kwa watu wote. Mini Shop ilianzishwa tangu mnamo tarehe 18/01/2018.

Tulianza tunauza bidhaa chache sana, bidhaa izo ilikuwa ni pamoja na Dawa ya Mbu zile za vidonge za kuchoma, Viberiti, Karanga, Ubuyu pamoja na Tauro za wanawake (Ped). Na kipindi icho tulikuwa tunauza bidhaa izo kutokea nyumbani kabla ya kujenga Frem hii rasmi ya kufanyia biashara kama inavyo onekana hapo kwenye picha.

Mini Shop a.k.a Duka Dogo tunauza bidhaa mbali mbali ila kwa ucheche tu, zifuatazo ni baadhi ya bidhaa tunazouza. 

Maji
Pipi
Unga
Tambi
Ngano
Amira
Juice
Mikate
Sigara

Chumvi
Mchele
Sukali
Karamu
Battery
Viwembe
Vitunguu
Viberiti
Biscuits
Madaftari

Vichongeo
Majani ya Chai
Dawa ya Mswaki
Jumbo Ball Gum
Sabuni za kuogea
Mafuta ya kupaka
Viungo vya Pirau
Mafuta ya kupikia
Sabuni za kufuria

Maharage ya Njano
Maharage ya Kombati
Tauro za wanawake (Ped)
Pon Pon au Bambino za watoto wachanga
Pia Mini Shop ni wakala wa Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Karibu sana dukani kwetu, karibu sana Mini Shop_Cheta tukuhudumie leo.


NYUMBA PAMOJA NA FREMU ZA BIASHARA ZINAUZWA

Nyumba hii ina idadi ya vyumba vitano (5) ambavyo unaweza kuvitumia kwenye matumizi yako binafsi kulingana na jinsi unavyotaka kutumia sehemu ya vyumba ivyo.
Cheta kwa Kijonjo

ipo karibu na barabara kuu ya serikari, kwaiyo inafaa sana kwa biashara pamoja na makazi ya kawaida tu ya kila siku kama kulala pamoja na huduma zingine.
Cheta kwa Kijonjo.

tayari imeisha fanyiwa wireling (mfumo wa umeme upotayari) kinachosubiliwa ni umeme kuwashwa tu basi alafu matumizi yaanze.
Cheta kwa Kijonjo frem

Kuhusu huduma ya maji ondoa shaka maana kisima kimechimbwa nyuma ya fremu/nyumba hii, pia eneo iloilo kuna huduma ya tofari, mchanga, cement, kokoto, nk.
Cheta kwa Kijonjo house

Nyumba hii au frem hii, ipo kijiji cha Kazole kitongoji cha Cheta kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. 

Bei ni tsh 24,000,000/- (millions ishirini na nne) pia mazungumzo yapo.

Mawasiliano:
0659 91 9292

UNAWAZO LA KUANZISHA BIASHARA YAKO BINAFSI?

Mpenzi msomaji wa makala hii, napenda nikwambie kitu kwamba siku izi watu wengi wanapenda kuanzisha biashara zao binafsi uku lengo lao kuu nikuachana na kuajiliwa kisha wajiajiri wenyewe na kujipatia kipato kupitia biashara zao walizo zianzisha.

Biashara za kufanya ziponyingi sana hapa duniani,ambazo ukizisimamia vizuri zinakutimizia marengo yako.
Mini Shop_Cheta kwa wakala_Mutalemwa

Mbali ya kwamba biashara nyingi zenye faida ya haraka ni zile biashara ambazo zina madhara makubwa kwa afya wa wanadamu mfano waweza kuwa Sigara, Pombe, madawa ya kulevya nk.

Ila zipo biashara ambazo nazo zinakuwa na faida japo kuwa inapatikana taratibu na uchukua mda mrefu kidogo kuonekana tofauti na biasha nilizo tangulia kuzitaja hapo juu.

Biashara izo ni pamoja na Unga wa Sembe, Sukari, mafuta ya kula, Pipi, jojo, soda, maji, madaftari, karamu, nk. Sasa basi, ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yako yoyote ile utakayokuwa umeichagua kuianzisha unatakiwa kuwa na mipango mazubuti juu ya usimamizi na uendeshaji wa biashara yako.
Mini Shop+Cheta+kwa wakala+Mutalemwa

Mipango iyo nipamoja na kujua namna ya kutenganisha faida na pesa ya mtaji, kuweza kujua namna ya kuendesha mfumo mzima wa mauzo pamoja na manunuzi, kulipa mishahara nk.

Angalizo, huwezi kufanya biashara bila kumbukumbu, biashara yoyote ile inahitaji utunzaji wa kumbukumbu, usipoweza kipengele hiki basi jua kabisa wewe huwezi kufanya biashara yenye tija, bali unaweza kufanya biashara ya mazoea tu basi. Kujaribu sio kushindwa ebu anza leo uone miujiza ya biashara.

Kutoka CHETA KAZOLE kwenda VIKINDU GETINI ni 6.749Km Pekee.

Ukweli ni kwamba kutoka Vikindu Getini kwenda kijiji cha Kazole sio mbali, ni wastani wa 6.749Km au 7Km pekee kutoka Vikindu getini hadi Kazole kwenye kitongoji cha Cheta.

Ila panaonekana kuwa mbali kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo ikiwemo ubovu wa barabara, ukosefu wa umeme, hospital/ Zahanati nk.

 Leo naomba niupongeze uongozi wa kijiji cha Kazole kwa kuchonga Barabara yenye urefu wa wastani wa 4Km kutoka Kazole Magenge 20 hadi kitongoji cha Cheta. 

Zoezi ili lilianza juzi tarehe 21/2/18 na kumalizika jana tarehe 22/2/18.
 Kuchonga na kufunika Mashimo kwenye baadhi ya maeneo ya barabara hii kutasaidi kwa namna moja au nyingine kwa Magari yanayotoa huduma kwa abiria kutoka Vikindu mpaka Magodani. 
Maoni yangu nikwamba mmefanya vizuri kuchonga hii barabara lakini mnaonaje ikawekwa kifusi au Changarawe ili kuifanya iwe imara zaidi ili kuwaondolea adha ya usafiri wakazi wa Kazole, Cheta na Magodani kwa kipindi cha mvua kinacho karibia kuanza mwezi ujao? 

Kwa mahitaji ya bidhaa za Panasonic, Venus, Moulinex, Ariston, Tefal, Wahl, Hotpoint, K.I.C, Hitachi, Sharp, pamoja na Toshiba.

Kwa mahitaji ya bidhaa za Panasonic, Venus, Moulinex, Ariston, Tefal, Wahl, Hotpoint, K.I.C, Hitachi, Sharp, pamoja na Toshiba.
Kwa mahitaji ya bidhaa za Panasonic, Venus, Moulinex, Ariston, Tefal, Wahl, Hotpoint, K.I.C, Hitachi, Sharp, pamoja na Toshiba.
Kwa mahitaji ya bidhaa za Panasonic, Venus, Moulinex, Ariston, Tefal, Wahl, Hotpoint, K.I.C, Hitachi, Sharp, pamoja na Toshiba.

Karibu sana dukani kwetu lililopo ndani ya jengo la Mlimani City. Duka letu linaitwa PANASONIC, tunatazamana na duka la JUSTFIT pamoja na AMINA DESIGN.

Ndani ya duka letu utaweza kujipatia bidhaa zifuatazo hapo chini nk.

1. Tv, Music System, Home Theatre, Radio na Speaker za magari, DVD player.

2. A/C, Fen, Water Pumps, Air Cooling.

3. Microwave, Friji, Frizer, Washing Mashine, water Dispense, Majiko ya umeme au ya Gesi,
Kwa mahitaji ya bidhaa za Panasonic, Venus, Moulinex, Ariston, Tefal, Wahl, Hotpoint, K.I.C, Hitachi, Sharp, pamoja na Toshiba.
Kwa mahitaji ya bidhaa za Panasonic, Venus, Moulinex, Ariston, Tefal, Wahl, Hotpoint, K.I.C, Hitachi, Sharp, pamoja na Toshiba.

4. Mashine za kunyolea ndevu au Nywere, Pasi, Jagi za kuchemshia maji, Blender, Rice cooker, Blue Tooth Devices, Battery.

Kwa maelezo zaidi tupigie kupitia 0659 91 9292

KARIBU SANA ANISUMA TRADERS LTD TAWI LA MWANZA

P.O. Box 1750 Mwanza, Plot No. 2, Block "R" Nyerere Road/Liberty Corner Opposite Al-Jumaa Masjid.

Contact: 0783 202 192/0756 407 160
Email: mwanza.tz@anisuma.com
Ndugu mteja karibu sana kwenye duka letu jipya la Sony hapa jijini Mwanza.

Dukani hapa tunauza vifaa vifuatavyo

1. Radio za Sony
2. Home Theatre System.
3. DVD Player  (Deki)
4. TV kuanzia inchi 18 nakuendelea
5. Camera
6. Radio ndogo za kushika mkononi
7. External Addisck  (kifaa cha kubebea data)
8. USB Flash ukubwa wa kila aina
9. Projector nazo tunazo
10. Speaker za kuongeza sauti kwa Tv, nk.
11. Battery za kila Size pia zipo za Kuchaji
12. Mashine za kunyolea Nywere
13. Mashine za kufulia nguo
14. Headphone na Earphone pia tunazo
15. Mashine za kunyolea ndevu
16. Pasi za nyere kwa akina mama nk.
17. Empty CD na Empty DVD-R na RW
18. Friji kila aina ya Size nazo tunazo
19. Frizer za kila Size pia nazo tunazo
20. Ovener za kila aina nazo zipo
21. Majiko ya umeme na Gesi pia yapo
22. Feni za kila aina zikiwemo za kuchaji
23. Pasi za kunyoshea nguo kila aina
24. Blender za kila ukubwa tunazo pia
25. Speaker za radio kwenye magari
26. Toster za kutengenezea mikate
27. Mashine za kuchomea nyama
28. Jagi za umeme za kuchemshia maji
29. Rice Cooker pia zipo
30. Mashine za kufanyia usafi zipo
31. Mixer za kila aina zote tunazo
32. Sound Bar za kisasa nazo tunazo
33. Mabegi ya kubebea Camera pia yapo
34. Water Dispenser nazo tunazo
35. CD za Gems pia nazo tunazo
36. Wall Blacket  (Stendi ya kuwekea Tv ukutani)
37. AC za kila ukubwa nazo tunazo
38. Juicer (mashine za kutengeneza juice) 
Tunapatikana Mwanza barabara ya Nyerere Road, Mtaa wa Liberty Corner tumetazamana na Msikiti wa Ijumaa.
Wote mnakaribishwa sana

NINI MAANA YA HISA?? BOFYA HAPA KUJUA MAANA YAKE NA JINSI INAVYOWAPATIA WATU VIPATO

Unapomiliki   au kuwa  na  wazo  la  kumiliki  kampuni  ni  vema  pia kujitahidi  kujua  mambo  kadhaa  yanayohusu  kampuni.  Kampuni  kama kampuni  inayo  mambo  mengi  sana. Katika  hayo mengi  si  lazima  ujue yote  isipokuwa yafaa ujue japo   machache   ya  msingi   ili upate ufanisi  wa kuendesha  kampuni.  Wengi  waliofungua  makampuni  hawajui   hata  mambo  madogo  yanayohusu   kampuni  na  uendeshaji  wake . Unamkuta  mtu  anamiliki  kampuni  kwa  mwaka  wa  tano  lakini  hajui  nini maana  ya hata  neno  Limited( LTD) ambalo  limeandikwa  kwenye  kampuni  yake.

Hii  ni  tofauti na  wenzetu    wazungu  ambao   hujishughulisha  na  kujua  mambo  ya  msingi   katika  shughuli  zao  mbalimbali  wanazoziendesha.  Kutokana  na hili  nimekuwa  nikieleza  mara  kwa  mara  baadhi  ya mambo  ya  msingi kuhusu kampuni.  Nakumbuka   nimewahi  kueleza namna  ya kuunda kampuni,  maana ya neno  limited,  namna  ya  kuandaa  mahesabu  ya  kampuni, jinsi  ya  kununua  na  kuuza hisa,   na  mengine  mengi. Kwa  anayetaka kuyaona  haya  atembelee  SHERIA  YAKUB  BLOG. Leo  tena  naeleza   kitu  kingine  ambacho  ni, Maana  ya  hisa  na  aina  zake ( shares) .

1.NINI  MAANA  YA  HISA.

Hisa ni  maslahi  ya  kila  mwanahisa  aliyonayo katika  kampuni  fulani. Yaani  wewe  kama ni  mwanahisa  katika  kampuni fulani  basi   yale  maslahi  yako au  kiwango chako  cha  uwekezaji  ulichowekeza  katika  ile  kampuni   ndio  hisa zako. Kama  mko  watu  kumi  katika  kampuni  basi  kila  mtu  ana  maslahi  au  kiwango kadhaa cha uwekezaji ambapo ukikusanya uwekezaji  huo  kwa  pamoja  ndio  utaitwa  hisa  za  kampuni.  Uwekezaji  au  maslahi  katika  kampuni  hutofautiana kutokana na  uwezo  wa  kila  mwanahisa.

Tofauti  hutokana  na kiwango  cha  kila  mtu  alichowekeza. Kuna  mwenye hisa  kumi, kuna  mwenye   ishirini,  kuna  mwenye  hisa mia n.k.  Hisa  siku  zote  hupimwa  kwa kiwango  cha  pesa.  Yawezekana  uwekezaji  wa  mtu kwenye  kampuni  ni magari  yaani  amepata hisa  kwa  kuchangia  magari.  Mwingine  amepata  hisa  kwa  kuchangia   ofisi.  Na mwingine   amepata  hisa  kwa  kuchangia  vifaa   vyote  vya  ofisi.  Katika  kuhesabu  hisa  michango  hii   yote  itawekwa  katika   viwango  vya  pesa  na  itasemwa  kuwa  fulani  ana  hisa  za  shilingi  kadhaa  na  sio  ana hisa  za  magari au vifaa  kadhaa.  Kwa  hiyo  hisa  huhesabiwa  kwa  mtindo/viwango   vya  fedha.

 2.   AINA  ZA  HISA.

Hisa  sio  hisa   kama  wengi  tunavyojua  isipokuwa  hisa  zina  aina  zake. Sio  kila  mwenye  hisa  ana  hisa  isipokuwa  ana  hisa  gani  au  za  aina  gani. Aina  za hisa  za mtu katika  kampuni  ndio  humwezesha  kujua  ana  haki  gani  katika  kampuni, ana  wajibu  gani   na anawajibikaje  likitokea  tatizo. Kwa  hiyo  haki,  wajibu(duty)   na  uwajibikaji(liability)  katika  kampuni  hutofautiana  kutoka  mwanahisa  mmoja  hadi  mwingine  kutokana  na  aina  za  hisa anazomiliki.  Wanahisa  wote  hawana  haki  sawa,  hawana  wajibu  sawa  na  hawawajibika  sawa  pamoja  na kuwa  katika  kampuni  moja. Hapa chini tutaona   aina  za  hisa.

( a  )  HISA  ZA  WAMILIKI  ( EQUITY  SHARES).

Hizi  ni  aina  za  hisa  ambazo  huwa  ndio  nyingi  katika  kampuni. Wale  wanaomiliki  hisa  nyingi   katika  kampuni  hisa  zao  huitwa  hisa  za  wamiliki.  Huitwa  hisa  za  wamiliki  kwakuwa   hawa  huhesabika  kama  ndio   kampuni  yenyewe  na  hivyo  wenye  hisa  hizo  ndio  wamiliki  wa kampuni.  Nimesema  hapo  juu  kuwa  wanahisa  hawana haki  sawa, wajibu  pamoja  na  uwajibikaji.  Wenye  hisa  hizi  wana  haki  kubwa  ya  kimaamuzi  katika  shughuli  zote  za  uendeshaji  wa kampuni   kwakuwa  wao  kila  hisa  moja  huwa  ni  kura  moja  na  kwahiyo  kila  kitu  hupitishwa  kwa  kura  zao.  Pia  wana  haki ya  kupata  mgao  mkubwa  kuliko  wengine. Hata  hivyo  wanawajibika  zaidi  linapotokea  tatizo  kwa  mfano   inapotokea  hasara  wao  ndio  hupoteza  zaidi. Kwa  jina  jingine  hisa  za  hawa  huitwa   HISA  ZA    SIMBA( LIONS  SHARE). Hii  ni  kwasababu  huko  mwituni  simba  hupata  mgao  mkubwa wa  nyama kati  ya  wanyama  wote.

( b ) HISA  ZA  KAWAIDA.

Hizi  ni  zile  hisa  ambazo  humilikiwa  na  watu  wengine   wa  kawaida  katika  kampuni. Mara  nyingi  hawa  ndio  huwa  wengi  japo  kila  mtu  huwa  na hisa  kidogo kidogo. Mgao  wao  wa  faida  hutokana  na asilimia  ya  kile  mtu  anachomiliki. Maamuzi  yao  katika  kampuni  huwa  ni   madogo ukilinganisha  na  wenye  zile hisa  za  umiliki( equity shares). Hata  hivyo  uwajibikaji  wao  nao ni  mdogo pia kwani hupata  hasara  kidogo  pale  kampuni  inapopata  hasara.  Pamoja  na  hayo  sheria  imewapa  kipaumbele  cha  kupewa  mgao  wa faida kabla  ya  kundi  jingine  lolote.

( c ) HISA  ZA  WAANZILISHI ( DEFERRED  SHARES).

Hizi ni  hisa  ambazo  hutolewa  kama  zawadi kwa  waanzilishi  wa kampuni. Mgao  wa  faida  wa hisa hizi  huwa  sio wa  moja  kwa  moja isipokuwa  hutegemea   na  faida  inayozidi. Kawaida mgao  wa  faida   kwa  wanahisa  wengine  hutoka  katika   faida   ya  kawaida lakini  hawa  hawapewi  mgao  kutoka  faida  ya  kawaida  isipokuwa   hupata  pale  faida  inapozidi  au  kuvuka  kiwango ilichotegemewa.

 ( d ) HISA  ZA  KAMPUNI( CORPORATE  SHARES).

Zote  nilizotaja  juu ni  hisa  za  kampuni  lakini  bado  jina  hili hupewa  hisa  hizi  kutokana  na  kuwa  ni  hisa  maalum  ambazo  hutolewa  kwa  waajiriwa/wafanyakazi  katika  kampuni  husika. Waajiriwa  hutengewa hisa  zao  na  mwenye  uwezo  huweza  kuchukua  hisa  hizo  kwa  kiwango  cha  uwezo  wake.  Mwajiriwa huendelea  kuwa  na  hisa   hizo hata  baada  ya  utumishi  wake  kukoma .  Kwa  ufupi  sana  niseme  tu  kuwa  hisa  sio  hisa  ila  hisa  ni  una  hisa  za  aina  gani

FAIDA NJE NJE NA AKAUNTI YA MALENGO, INGIA HAPA KUJUA ZAIDI

Pata nafasi ya kujishindia TOYOTA HILUX MPYA ya Mwaka 2016 kwa kufungua akaunti ya Malengo kupitia Benki ya NBC. NBCMalengo.

Kama wewe ni Bloggers | Mwandishi wa habari | Makerting | Money Makers | nk |ingia hapa

Habari za leo ndugu, ikiwa ni siku nyingine tena tunakutana hapa kujulishana habari muhimu. Leo napenda kuwatambulisha mtandao bora na rahisi kutumia katika mambo ya kutangaza bidhaa zako na kisha kulipwa kwa asilimia ya kile ulichokifanya.

Mtandao huu unaitwa PropellerAds, utendaji kazi wake unafanana kabisa na mtandao wa Google Adsense, kwa wale ambao ni wageni mnaweza kuwa hamjanielewa ila kwa wenzangu bloggers na wengineo mtakuwa mmenielewa.

Google adsense ni mfumo ambao google wanakupatia matangazo unayaweka kwenye blog au website yako kisha unakuwa unalipwa kulingana na watembeleaji walivyo yabonyeza, mfumo huu ndio sawasawa na wa Propeller ila tofauti kati ya Propeller na google ni kwamba google waga wana masharti mengi na magumu sana ambapo watumiaji wake waga wanafungiwa account zao kila mara.

Kujiunga na mtandao huu wa kibiashara bofya hapo chini palipo na maneno kwenye mabano ikisha funguka bofya kwenye eneo lenye vimistari vitatu (kama vinavyo onekana kwenye picha iliyopo hapo chini kwa upande wa kulia), kisha chagua Register, na fuata maelekezo.

             (( CLICK HERE TO REGISTER ))

Mtandao huu unawafaa sana watu wote wenye blogs/website/watu wa matangazo/watu wenye nia ya kukuza biashara zao kupitia njia za kujitangazo/na watu wenye kupenda kutengeneza pesa kupitia njia ya mtandao.

Na kwa upande wa PropellerAds hawa jamaa wana masharti nafuu kabisa pamoja na % asilimia wanayoitoa kwa kila tangazo ni kubwa ukilinganisha na ile ya googleAds.

Sasa kama wewe unataka kupiga pesa nyingi tena kwa mda mfupi tena bila masharti magumu basi jiunge na mtandao huu utakuwa mkombozi wako kwa njia ya kujipatia pesa.

Mimi binafsi nimejiunga jana ila mpaka kufikia mda huu nimeisha anza kuona mafanikio yao nasio mimi tu bali kuna watu wengine wameisha jiunga wanaweza kuwa mashaidi juu ya kile ninachokisema kuhusu Propeller. 

FOR SALE/ NYUMBA INAUZWA TSH.75 MILLIONS, PICHA NA MAELEZO ZAIDI BOFYA HAPA

Iyo nyumba ina vyumba vitatu vya kulala, sitting room, dinning room, kitchen na stoo ya nje na choo cha ziada cha nje.

Eneo la kiwanja chake ni Futi 50 kwa futi 60 au mita 18 kwa mita 20. Nyumba tayari ina umeme, maji, ipo ndani ya fensi, kuna parking ya gari nk.

Chumba cha master kina choo chake ila vingine viwili havina lakini kuna bafu na choo cha public kwa ndani ya nyumba na pia kwa nje kuna choo pamoja na stoo.

Nyumba ipo Saku Stend mkono wa kushoto- Mbagala mbele kama unaelekea Chamazi, bei tunaanzia Tzs milion 80 ila maongezi yapo. 

Hii ndio ramani yake.Tuwasiliane kupitia namba ya simu ifuatayo 0659 91 9292

TOYOTA DUET INAUZWA TSH 5.5MILLIONS, PICHA 6 ZAIDI BOFYA HAPA

Hii ni gari aina ya Toyota Duet ambayo inauzwa kwa Tsh 5.5millions na bei inapungua.

Muonekano wa taa ya gari hii, pia gari hii iko hapa Dar es Salaam. 
Gari hii Bima imeisha na exzost yake ni ya kuchomelea 2 iko vizuri sana kiukweli. 

Muonekano wa upande wa nyuma

Itakuwa vizuri ungekuja uione na utest ipo vizurisana gari hii
Muonekano wake kwa upande

Muonekano wake ikiwa imefunguliwa mirango

Munekano wake kwa upande wa nyuma. Tuwasiliane kupitia 0659 91 9292 naitwa Mutalemwa 

STARLET INAUZWA KWA TSH 6.5MILLIONS, PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Gari hii ni aina ya Starlet, ambayo imesajiliwa kwa namba T 580 CMS kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini. 


Bei ya gari hii iliyotajwa hapo kwenye kichwa cha habari inapungua kabisa kwa mteja ambaye yuko serious kuinunua.

Gari hii inapatikana Dar-es-Salaam, kwa yeyote mwenye kutaka kuja kuiona na kuinunua Tuwasiliane kupitia 0659 91 9292 naitwa Mutalemwa. 
Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top