Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MINI SHOP CHETA

Mini ShopCheta au Duka Dogo

Ni duka dogo kweli kama jina lake linavyojieleza hapo juu. Duka hili linatoa huduma ya mahitaji ya kawaida ya kila siku kwa wakazi wa Kitongoji cha Cheta pamoja na maeneo ya jirani au kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mini Shop inatoa huduma ya jamii kwa watu wote. Mini Shop ilianzishwa tangu mnamo tarehe 18/01/2018.

Tulianza tunauza bidhaa chache sana, bidhaa izo ilikuwa ni pamoja na Dawa ya Mbu zile za vidonge za kuchoma, Viberiti, Karanga, Ubuyu pamoja na Tauro za wanawake (Ped). Na kipindi icho tulikuwa tunauza bidhaa izo kutokea nyumbani kabla ya kujenga Frem hii rasmi ya kufanyia biashara kama inavyo onekana hapo kwenye picha.

Mini Shop a.k.a Duka Dogo tunauza bidhaa mbali mbali ila kwa ucheche tu, zifuatazo ni baadhi ya bidhaa tunazouza. 

Maji
Pipi
Unga
Tambi
Ngano
Amira
Juice
Mikate
Sigara

Chumvi
Mchele
Sukali
Karamu
Battery
Viwembe
Vitunguu
Viberiti
Biscuits
Madaftari

Vichongeo
Majani ya Chai
Dawa ya Mswaki
Jumbo Ball Gum
Sabuni za kuogea
Mafuta ya kupaka
Viungo vya Pirau
Mafuta ya kupikia
Sabuni za kufuria

Maharage ya Njano
Maharage ya Kombati
Tauro za wanawake (Ped)
Pon Pon au Bambino za watoto wachanga
Pia Mini Shop ni wakala wa Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Karibu sana dukani kwetu, karibu sana Mini Shop_Cheta tukuhudumie leo.


GOROFA MAARUFU SOUTHAFRICA WANAKOISHI WATANZANIA NA WAAFRICA HALINA UMEME WALA MAJII.

GOROFA MAARUFU SOUTHAFRICA WANAKOISHI WATANZANIA NA WAAFRICA HALINA UMEME WALA MAJII.
SERIKALI YA NCHI HIYO KAMA IMELITELEKEZA LIKO JOBERG

Takribani watu 39 wamefariki dunia na wengine wapatao 69 wamejeruhiwa vibaya

UTURUKI: Takribani watu 39 wamefariki dunia na wengine wapatao 69 wamejeruhiwa vibaya baada ya ukumbi mmoja wa starehe kufanyiwa shambulio la Kigaidi usiku wa kuamkia leo. 

Washambuliaji wawili wanaohofiwa kuwa ni wa Kikundi cha Kigaidi cha ISIS ndio wametekeleza shambulio hilo. 

Wananchi katika mji mkuu wa Seoul Korea Kusini wanaandamana wakishinikiza Rais wao, ajiuzulu

KOREA KUSINI: Wananchi kwa maelfu katika mji mkuu wa Seoul wanaandamana wakishinikiza Rais wa nchi hiyo, Park Geun-hye ajiuzulu.

Rais Park Guen Hye, anatuhumiwa kwa kuwa na uhusiano wa karibu na baadhi ya watu, wanaokabiliwa na shtaka la kujaribu kuibia Serikali fedha nyingi kupitia kampuni kadhaa za taifa hilo.

Wakamatwa wakidaiwa kujihusisha na ulaji wa nyama za watu, zaidi bofya hapa

Serekali ya kenya imewakamata baadhi ya watu ambao inasadikiwa wamekuwa wakijihusisha na ulaji wa nyama za watu 


watuhumiwa hao wamekutwa na badhi ya viungo vya watu wanaodaiwa kuuwawa kwa lengo la kufanywa kitoweo.

Matokeo ya kura zenu juu ya Donald Trump na Hillary Clintoni ni kama ifuatavyo

Shukurani za dhati kwako wewe shabiki wetu wa Tanzania ulieitikia wito wa kushiriki katika zoezi la kuchaguwa kati ya Donald Trump na Hillary Clinton, nani ungependa awe rais ajaye wa Marekani.


Matokeo ya kura zenu ni kama ifuatavyo:
Tanzania
Donald Trump: 39.6%
Hillary Clinton: 60.4%
Mataifa mengine ya dunia:
Donald Trump: 31.2%
Hillary Clinton: 86.8%

MAAFISA POLISI WARUHUSIWA KUVAA HIJABU KAZINI, ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali ya Scotland imeidhinisha vazi la hijabu na kulijumuisha kwenye sare za maafisa wa polisi wa kike wa Kiislamu ili kuongeza idadi yao katika idara hiyo. 

Mkuu wa idara ya polisi nchini humo Phil Gormley, ametoa maelezo na kubainisha furaha kubwa kwa kutangaza uamuzi huo, na kufahamisha nia yao kutaka kusaidiana na maafisa wa Kiislamu katika suala la usalama wa taifa. 

Muungano wa maafisa wa polisi wa Kiislamu SPMA nchini humo pia ulitoa maelezo na kufahamisha kwamba uamuzi huo utaweza kuimarisha mahusiano bora kati ya jamii za Scotland na jumuiya ya Kiislamu. 

Mkuu wa SPMA Fahad Bashir alisema, ''Uamuzi huo uliochukuliwa na serikali ni sahihi. Tunapata faraja kuona nchi yetu ikichukuwa hatua muhimu kama hizi zenye mwelekeo mzuri.'' 

Hapo awali, maafisa waliokuwa wakiruhusiwa kuvaa hijabu walikuwa ni wale waliohudumu kwa miaka zaidi ya 15 na wanaoshikilia nyadhifa za juu. 

Katika mwaka 2001, sare rasmi za polisi zilitambulishwa ambapo hijabu pia ilijumuishwa.

Samsang yawataka wateja wake kurudisha mashine milioni 3 za kufulia wakidai zinalipuka

Samsung imewataka wateja wake kurudisha takribani mashine milioni 3 za kufulia zinazodaiwa kuwa zinaweza kulipuka wakati zikifanya kazi.

Mwezi Septemba kampuni hiyo ya Korea Kusini ilitangaza kurudishwa kwa simu za Samsung Galaxy Note 7 ambazo ilidaiwa kuwa zinalipuka wakati wa kuchajiwa.

Kampuni ya vifaa vya umeme ya Samsung yatangaza kurudishwa kwa takribani mashine milioni 3 za kufulia kwa kuwa kuna taarifa za kuwa mashine hizo zinaweza kulipuka wakati zikifanya kazi.

Mwezi Septemba kampuni hiyo ya Korea Kusini ilitangaza kurudishwa kwa simu za Samsung Galaxy Note 7 ambazo ilidaiwa kuwa zinalipuka wakati wa kuchajiwa.

Help me with your phone please...you know what happen after phone?? Click here and see

Help me with your phone please...you know what happen after phone?? Click here and see 
Updating status.. accident... waiting ... ambulance to take me hospital.

TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA NCHINI IVORY COAST?? BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Huyu anayevutwa na Askari sio kibaka, sio mwizi, sio mfuasi wa chama cha upinzani ambao wengi wamezoea kuonewa bila sababu. Huyo ni Rais wa nchi. Ni Rais wa zamani wa Ivory Coast Ndg.Laurent Gbagbo.

Kitaaluma Gbagbo Mkemia, lakini kabla ya hapo alikua mwalimu wa shule ya sekondari. Alihitimu PhD yake ya Kemia mwaka 1979 kutoka chuo kikuu cha Paris Diderot University (Ufaransa).

Hakuwahi kufikiria kuwa Rais wa nchi hiyo licha ya kujaribu kugombea mara kadhaa. Alipata nafasi ya urais kibahati bahati baada ya kiongozi wa mapinduzi wa nchi hiyo Jenerali Robert Guéï kukata jina la mtangulizi wake Henri Konan Bédié, pamoja na jina la Waziri Mkuu wa zamani aliyekua anapewa nafasi kubwa ya kushinda Ndugu Alassane Ouattara.

Wakati Gbagbo akigombea Urais wa nchi hiyo alijipambanua kama mtetezi wa wanyonge, mpenda demokrasia, mtu anayeumizwa na matatizo ya watu maskini, na mpenda haki. Alijipambua kama mtu wa "KAZI" kwa ajili ya kuinua maisha ya watu maskini. Akajinasibu kujenga viwanda hasa vya Cocoa, kahawa na mafuta yanayochimbwa nchini humo.

Lakini alipoingia madarakani akaanza kukandamiza demokrasia, kubana vyama vya upinzani, kubana vyombo vya habari, kupandisha kodi hadi kwenye bidhaa zinazotegemewa na watu maskini. Akaanza kutoa upendeleo kwa watu wa familia yake na kuteua ndugu zake kushika nafasi za juu katika wizara na idara za serikali.

Akamkamata na kumuweka kizuizini Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Ndugu Alassane Ouattara ambaye aliamua kujiunga na chama cha upinzani cha Republican (RDR) mwaka 1994. Akasahau kwamba wakati Ouattara akiwa Waziri Mkuu yeye alikua Mbunge tu ktk serikali Félix Houphouët-Boigny. Licha ya wafuasi wa chama chake kukamatwa bila sababu, Oattara hakuweka kinyongo. Bado alisalimiana na Gbagbo na kumheshimu kama Mkuu wa nchi.

Lakini Gbagbo akalewa madaraka. Akafikia hatua ya kuona kwamba yeye ndiye mtu pekee aliye sahihi katika nchi hiyo na maneno yake ni sheria. Akapuuza katiba ya nchi. Akaagiza kukamatwa kwa vijana wengi waliokua wafuasi wa vyama vya upinzani wanaomkosoa. Akapiga marufuku maandamano ya kisiasa.

Baadhi ya raia wa Ivory Coast wakalalamika kuwa Rais wao ameanza kuwa "Dikteta". Lakini kila aliyesikika akimuita Gbagbo dikteta aliishia korokoroni. Hatimaye Gbagbo akawa ndiye msemaji wa mwisho, mwenye nguvu na mamlaka juu ya mambo yote na kauli yake haitakiwi kupingwa wala kusahihishwa.

Ziara yake ya kwanza nje ya nchi alimtembelea Rais wa Burkina Fasso, swahiba wake Blaise Compaoré ambaye alikua na elements za udikteta. Compaore ndiye aliyemuua Thomas Sankara (the true son of Africa) na kujitangaza Rais mwaka 1987.

Kwahiyo Gbagbo aliporudi na kuanza kuongoza nchi yake kibabe, kukamata wanaomkosoa na kufungia vyombo vya habari, wananchi wakajua ni matokeo ya urafiki wake na dikteta Compaore.

Hali ya uchumi ya Ivory Coast ikazidi kudorora siku hadi siku. Watumishi wengi wa umma hawakulipwa mishahara yao kwa wakati, wawekezaji wengi wa kigeni wakafunga biashara, hakukua na nyongeza ya mishahara kwa watumishi lakini nyongeza ya kodi ilikua kwenye kila bidhaa na huduma.

Rais Gbagbo akapandisha ushuru/kodi katika Bandari ya Abidjan. Wafanyabiashara wengi wa nchi za Burkina Fasso na Mali wakaanza kupitisha mizigo yao kwenye bandari za Togo, Benin, na Liberia. Rais Gbagbo aliposhauriwa na wachumi juu ya athari ya maamuzi yake alikua mkali na kutishia kuwafukuza kazi waliomshauri. Alisema ni heri zije meli chache zenye kulipa kodi kubwa kuliko meli nyingi zenye kulipa kodi ndogo.

Hatimaye idadi ya meli zinazotua katika bandari ya Abidjan zikaanza kupungua kutoka meli zaidi ya 35 kwa mwezi hadi wastani wa meli 8 hadi 12 kwa mwezi (ingia hapa  http://www.marinetraffic.com/en/ais/index/eta/all/port:1150/portname:ABIDJAN). Pia mapato ya bandari yakaanza kupungua. Kilimo cha Cocoa ambalo ni zao kuu la biashara nchini humo kikaanza kuporomoka na uzalishaji wa mafuta ukaanza kupungua.

Uchumi ukazorota na hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu. Rais Gbagbo akadhani watu wameficha pesa majumbani kwao, kumbe ni matokeo ya mfumo wa uchumi alioutengeneza mwenyewe.

Lakini wakati hayo yote yakiendelea, mamlaka ya mapato ya Ivory Coast (Cote' d’Ivoire General Direction of Taxes) ikawa inatangaza kukusanya mapato makubwa na kuvuka lengo kila mwezi. Wananchi wakajiuliza hayo mapato yanaenda wapi kama watumishi hawalipwi mishahara, huduma muhimu za jamii zimeongezwa kodi, madai ya watumishi hayafanyiwi kazi, miundombinu haijengwi, hospitalini hakuna madawa, benki zimesitisha mikopo, na Rais mwenyewe analalamika pesa haipo katika mzunguko. Je hayo makusanyo makubwa ya kodi yanatoka kwenye vyanzo vipi, na yanatumikaje mbona maisha yanazidi kuwa magumu?

Hatimaye mwaka 2010 wananchi wa Ivory Coast wakashindwa kuendelea kuvumilia shida, manyanyaso, ubabe, hali ngumu ya maisha, ukandamizaji wa demokrasia, na udikteta uchwara wa Rais Laurent Gbagbo. Kwenye uchaguzi mkuu wa November 28 mwaka 2010 wakamchagua Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo (kipenzi cha watu, mtu asiye na visasi) Alassane Ouattara kwa asilimia 54.1% ya kura zote halali.

Tume HURU ya uchaguzi ya nchi hiyo, Ivorian Election Commission (CEI) ikamtangaza mgombea wa upinzani ndugu Ouattara kuwa mshindi wa kiti hicho cha Urais. Lakini Rais Gbagbo akakataa kuachia madaraka. Akajitangaza kuwa yeye ndiye mshindi na akadai kuwa amepata asilimia 51% ya kura zote halali.

Baada ya kujitangaza mshindi akatangaza pia kuivunja tume ya uchaguzi (CEI) na akatangaza kutotambua matokeo ya Tume hiyo. Pia akatoa amri kwa jeshi la nchi hiyo kufunga mipaka yote ya nchi (ya kuingia na kutoka) na akafukuza waandishi wote wa habari kutoka vyombo vya habari vya kimataifa waliokua wakiripoti uchaguzi huo. Akazifungia Radio na magazeti yote ya nchi hiyo yaliyotangaza kuwa ameshindwa uchaguzi.

Lakini wananchi wakaungana kupinga hatua hizo za kidikteta za Rais Gbagbo. Wakaaondoa tofauti zao za kidini, kikabila na kikanda kama ambavyo wamekuwa wakigawanywa na wanasiasa kwa muda mrefu. Wakaamua kuungana kwa pamoja kupinga maamuzi hayo. Wakristo ambao wengi wapo kusini mwa nchi hiyo na waislamu ambao wapo kaskazini wakaweka tofauti zao chini na kuungana kwa pamoja kupinga udikteta uchwara wa Rais Gbagbo.

Maandamano makubwa ya kumshinikiza Gbagbo kuachia ngazi yakafanyika katika mji mkuu wa Abidjan na kuzingira Ikulu yake. Japo mwanzoni Polisi waliuwa raia walioandamana lakini haiwakukatisha tamaa wengine kuingia barabarani. Hatimaye kufikia Aprili 10 mwaka 2011 Rais Gbagbo akawa amezingirwa na maelfu ya watu katika Ikulu yake. Watu wenye hasira ya uonevu aliowafanyia, watu wenye uchungu wa kuumizwa na kunyanyaswa, watu wenye kiu ya demokrasia.

Gbagbo akajua siku yake ya kiyama imefika, hofu ya mauti ikamvaa. Ikulu aliyoiona kama "paradiso" yake, ikageuka kuwa "bonde la uvuli wa la mauti". Akaomba msaada kwa walinzi wake wamtoroshe. Lakini walinzi wakashindwa kumtorosha kutokana na msongamano mkubwa wa wananchi waliozingira Ikulu.

Wananchi waliokua wamezingira Ikuku hiyo wakadai kuwa wanamtaka Gbagbo atolewe nje wamuadhibu kwa mikono yao wenyewe vinginevyo watachoma Ikulu hiyo afie ndani. Hatimaye serikali ya Ufaransa (mkoloni wa zamani wa Ivory Cost) ikatoa helcopter maalumu na makomandoo kadhaa kwenda kuepusha maafa ambayo yangeweza kutokea.

Makomandoo hao wakafika Ikulu ya Gbagbo na kumkuta amejificha uvunguni mwa kitanda kwenye handaki la chini kwenye ikulu hiyo akiwa na mkewe Simone Gbagbo. Wakamtoa na kuondoka nae. Wakamuepusha na "mauti" kutoka kwa raia wake.

Hatimaye Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo (kipenzi cha watu) Alassane Ouattara akatangazwa na kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo. Na Gbagbo akapandishwa kizimbani ICC ambako anakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binadanu (crimes against humanity), ikiwa ni pamoja na mauaji ya wapinzani wake, ubakaji, vitisho/ubabe na ukiukwaji wa utawala wa sheria (murder, rape and persecution).

Umejifunza_nini??

Papa Francis amemtangaza rasmi Mama Teresa kuwa Mtakatifu. Habari kamili bofya hapa

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amemtangaza rasmi Mama Teresa kuwa Mtakatifu. Papa Francis alitangaza mapema mwaka huu kuwa Septemba 4 itakuwa siku ambapo sherehe ya kutakatizwa kwa Mama Teresa itafanywa, ambayo itakuwa ni siku moja kabla kuadhimisha miaka 19 tangu kufariki kwake.

Mama Teresa alipewa tuzo ya Nobel kutokana na kazi zake zilizolenga masikini, wagonjwa, wazee na wapweke katika mitaa ya mabanda ya Kolkata, ambako zamani kulitambulika kama Calcutta.

Pia amekuwa na mchango mkubwa kwa Kanisa haswa baada ya kufanya idadi kubwa ya wakazi wa India kwenda kuhij katika kanisa la Mtakatifu Peter huko Roma.

Jina halisi la Mama Teresa lilikuwa Agnes Gonxha Bojaxhiu, mwenye asili ya Albania aliyezaliwa 1910 katika eneo ambapo sasa linatambuliwa kama Skopje, Macedonia.

Alifika India mnamo 1929 baada ya kuishi na kundi la wamishenari kwa muda nchini Ireland.

Alianzisha kundi la Wamishenari wa Misaada mnamo 1950 na akapewa uraia wa India mwaka uliofuata.

Mnamo 2015, alisifiwa na wataalamu wa Vatican kwa kusababisha uponyaji wa mwanamume wa Brazil katika mwaka wa 2008 ambaye alikuwa na uvimbe kwenye ubongo wake.

Hiyo ilimfanya Teresa kufikisha kiwango kinachohitajika kwa mtu kutangazwa kuwa mtakatifu.

Papa John Paul wa Pili alimtangaza kuwa mbarikiwa mnamo 2003. Francis aliwahi kukutana na Teresa 1994.

NDEGE YA YAANGUKA NA KUUWA WATU ZAIDI YA 6, ZAIDI BOFYA HAPA

Takribani watu 6 wamefariki katika ajali ya ndege ndogo illiyoangukia kwenye miti na kuwaka moto ilipokuwa ikitua uwanja wa Shannon.

Ajali hiyo imetokea jimbo la Virginia na mpaka sasa chanzo chake hakijajulikana.

MTOTO MKUBWA WA RAIS OBAMA AHISIWA KUVUTA BANGI, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Mtoto mkubwa wa Rais Barack Obama  Malia Obama anahisiwa siku kadhaa nyuma alikuwa amepewa kipisi cha bangi kuvuta na akavuta na kujikuta akirekodiwa na video za mapaparazi wa Marekani. Tukio hilo limekuja siku chache tu baada ya video nyingine kumuonesha binti huyo akikata viuno kwenye moja ya matamasha ya muziki huko Marekani.

Inasadikiwa Malia alivuta sigara hiyo ‘haramu’ kwenye tamasha la lollapalooza kwenye Jiji la Chicago, jimbo la Illinois ambalo ni jimbo la nyumbani kwa Rais Obama. Mmoja wa wahudhuriaji wa tamasha hilo Jerrdin Selwyn mwenye umri wa miaka 18 alidai kuwa alimkuta Malia akiwa anavuta ganja na marafiki zake na hakukuwa na shaka ya hilo kwani harufu ya bangi ilikuwa wazi

“Kulikuwa na kijana mmoja pale ambaye alikuwa anavuta na akampasia Malia ambaye alishikilia kama kwa dakika moja kisha akampatia mtu mwingine” alidai binti huyo. Na alidai pia kuwa alikuwa na picha zinazoonesha mtoto huyo wa Rais wa Marekani akivuta bangi hiyo. Source: Masama blog

PICHA TATU ZIKIONYESHA JINSI PAPA FRANCIS ALIVYO ANGUKA, BOFYA HAPA

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameanguka gafla wakati akiwa akiendelea na misa huko nchini Poland baada ya kujisikia vibaya.

Mpaka sasa haijajulikana chanzo vha kiongozi huyo kuanguka kilikuwa ni nini ila endelea kuwa nasi ili tukujuze chanzo cha tukio hili.

KOFFI OLOMIDE AKUMBWA NA MASWAHIBU MAZITO, ZAIDI BOFYA HAPA

KINSHASA, CONGO: Mahakama imemhukumu Mwanamuziki Koffi Olomide, miezi 18 jela kwa kumpiga mnenguaji wake wa kike wiki iliyopita.

Hukumu yake hiyo haina adhabu mbadala ya kulipa faini kwa hiyo kutumikia hiyo miezi 18 jela

MHE. LOWASSA AUDHURIA TUKIO LA KUWEKWA WAKFU ASKOFU JACKSON NASOORE NAIROBI, KENYA.

Leo tarehe 3 julai Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Ngoyai Lowassa alikua moja wa wageni waalikwa sambamba na Rais wa Jamuhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta.

katika tukio kubwa la kumuwekea wakfu Askofu wa jimbo kuu la kanisa la Anglikana Kenya, Askofu Dr. Jackson Nasoore Ole Sapit

Tukio hili limefanyika kwenye kanisa la "All Saints Cathedral Nairobi nchini Kenya".

Endelea kutazama picha mbali mbali juu ya tukio hili la siku ya leo.
Wakisalimiana yeye pamoja na viongozi wenzake 
Ushikamano na umoja ni jambo la msingi sana kwa nchi zetu hizi.
Endelea kuwa nasi tukujuze zaidi kupitia tovuti yetu hii ya Mutalemwa Blog. 

WATU 75 WAUAWA NA WENGINE 100 KUJERUHIWA VIBAYA, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

BAGHDAD, IRAQ: Watu 75 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa jana jioni baada ya wanamgambo wa ISIS kufanya shambulizi sokoni.

Shambulio hilo limetokea wakati ikiwa imepita wiki moja tangu jeshi la Iraq liukamate mji wa Falluja kutoka kwa wanamgambo wa ISIS.

MTANZANIA MMOJA YAMKUTA MAKUBWA BAADA YA KUDHALILISHA MHUDUMU WA KIKE WA NDEGE YA EMIRATES

Dubai. A Tanzanian (name withheld), travelling on an Emirates Airline flight from Dar es Salaam to Dubai, was charged at a Dubai court today after he pulled a cabin crew attendant towards him, hugged and kissed her as he took a selfie.

He has gone on trial for molesting the 25-year-old American employee.

Dubai Court of First Instance was told the incident took place in an an Emirates Airline flight from Dar es Salaam to Dubai on April 22, 2016.

Prosecutors said the man asked for a picture with the attendant as she served passengers and she agreed.

While she was posing for the snap, the accused put his hands around her shoulder and then hugged her, she said.

“My supervisor yelled at the man for hugging me,” the American woman told prosecutors.

He asked her again for a picture and she agreed.

She said: “I stood next to him for the shot when he hugged me again and even and kissed my neck.” She said she was angry and pushed the passenger away to the back of the plane.

Another air stewardess said that the passenger appeared normal and did not cause any trouble or the rest of the flight.

However, the attendant informed police when the plane landed in Dubai and the man was arrested.

Police said the passenger, who only speaks Swahili, admitted to hugging and kissing the woman on the flight.

However, the man did not enter a plea in court and presiding Judge Fahad Al Shamsi, adjourned the case until next month.

He could face a year in jail to be followed by deportation.

WENGINE HAO RAIA WA ETHIOPIA 79 MBARONI, KISA NA MKASA INGIA HAPA

Wahamiaji 79 raia wa Ethiopia wamekamatwa katika kitongoji cha Kitame kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

ambapo taarifa za kukamatwa kwa wahamaji hao zimetolewa na wananchi kwa maafisa wahamiaji ikiwa ni mpango wa kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu nchini. 

WAISLAMU HAWAFAI KUINGIA MAREKANI, KISA NA MKASA BOFYA HAPA

Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump

Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amesema mauaji ya watu 50 katika baa moja ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya Marekani.

Trump amemkashifu mpinzani wake wa chama cha republican Bi Hillary Clinton, kwa kutodadisi sababu za mtu huyo kutenda mauaji hayo.

Amesema hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya waislamu.

Upande wa Bi Clinton wakitoa risala za pole kwa waathiriwa wa mkasa huo papo hapo wamemtaja Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.

Wakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.

Wakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.

FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.


Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya wanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.

Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu wa aliyekuwa tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini.

NB: Ukitaka kujua unafiki wa huyu bwana Marekani hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi sana ya mauwaji ya kibaguzi mauwaji ya mitaani hata juzi mwanamuziki kauwawa club hatujamsikia kusema lolote juu ya mauaji hayo, leo mashoga kushambuliwa na mtu mwenye jina la kiislamu imekuwa ndio habari kwa wenye chuki na uislamu.

              Source: Jamii Forum 

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top