Featured

    Featured Posts

Loading...

BILIONI 4 ZA SHEREHE YA UHURU, ZIJENGE BARABARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha kiasi cha shilingi bilioni 4 zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015.

zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.

BAADHI YA HEADLINES KWENYE KURASA ZA LEO

Good Morning mtu wangu. Kama umepitwa na dakika 20 za uchambuzi wa magazeti redioni leo asubuhi hizi ni baadhi ya stori zilizogusa headlines kwenye kurasa za leo

Kasi ya Rais Magufuli yavunja ngome UKAWA, kasi ya kutumbua matibu yawafanya vigogo kubadili majina ya mali zao, waliojifanya miungu watu sehemu za kazi sasa wajishusha, Rais Dk John Magufuli avunja rekodi Baraza la Mawaziri wananchi walisubiria kwa hamu.

Wananchi wasubiri jibu la vinara wa  biashara ya dawa ya kulevya. Mali za vigogo wa TRA za ibua mjadala mkubwa huku mmoja akutwa na nyumba 73.

Shirika la Usafiri Dar es salaam, UDA ni moja ya mashirika yaliotajwa na kupewa siku 30 na Rais Magufuli kutoa maelezo ya kina kuhusu uwekezaji wake kabla ya kurejeshwa kwenye mikono ya Serikali, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mikataba ya uwekezeaji imekeukwa kwa kutoendelezwa mali hizo zilizokuwa za umma.

Vigogo wengi wa Serikali wanaotuhumiwa kujihisihsha na ubadhilifu wa fedha za umma na kuzitumia kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo nyumba za kisasa na kuzipangisha wameanza kubadilisha majina yao ili umiliki wao usifahamike.

Jiji la Dar es salaaam kuwa chini ya Meya anaetokea kwenye umoja wa UKAWA kwa mara ya kwanza.

Bohari la dawa, MSD imejiimarisha na kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati agizo la Rais Magufuli la kuhakikisha kunakuwa na maduka ya dawa ndani ya hospitali zote za Serikali hapa nchini ambapo imeanza kwa kasi kubwa katika Hospitali ya taifa Muhimbili.

Kampuni ya madini ya Petra Diamonds, imegundua aina adimu ya almasi ya rangi ya pink yenye uzito wa karati 23.16 kutoka kwenye mgodi wake wa Wiliamson uliopo Shinyanga, almasi hiyo ni moja ya madini ya rangii yanayosakwa zaidi duniani na hupatikana kwenye migodi michache sana duniani.

TRA YAIZUIA KAMPUNI YA BAKHRESA KUPELEKA KONTENA

Mamlaka ya Mapato Tanzania imezuia kampuni ya Bakhresa kupeleka makontena yake katika bandari yake kavu.

Hii ni kutokana na baadhi ya makontena kugundulika kuwa yalipitishwa bila kulipa kodi.

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI

HABARIZAHIVIPUNDE‬:Waziri mkuu wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa afanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya DSM na kuagiza waliohusika na upotevu wa makontena 349 kukamatwa mara moja.

Kikao hicho kimeuzuliwa na mkuu wa jeshi la polisi nchini bwana Erenest Mangi, katibu mkuu wa ofisi ya waziri mkuu Dk.Faurence Turuka, katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi dk.Shaabani Mwinjaka, kamanda Suleiman Kova, Mkurugenzi wa mamlaka ya bandari TPA bwana Awadhi Masawe, pamoja na viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.

Waziri mkuu amewataja viongozi aliowasimamisha kazi ni pamoja na Kamishna wa forodha bwana Tiagi Masamaki, mkuu wa kituo kwa wateja bwana Abibu Mkunenzia, mkuu wa kitengo cha tehama bwana Haruni Mhande, bwana Hamis Ally Omary, Pamoja na mkuu wa kitengo cha bandari kavu ICD incharge bwana Eliach Mrema. 

Mbali ya kuwasimamisha kazi viongozi hao, pia ameagiza viongozi wengine watatu waamishiwe mikoani. Viongozi hao ni pamoja na Bwana Anangisie Mtafya, Msajigwa Mwandengere, pamoja na Robert Nyoni.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHANGAZWA NA KUTOTUMIKA KWA MABASI YA MWENDO KASI

HABARIZAHIVIPUNDE‬:Waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa ametembelea ofisi za TAMISEMI na kukutana na wakurugenzi.

Ambapo ameshangazwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi kutokuanza kufanya kazi hadi sasa licha ya kuelezwa katika ripoti kuwa umekamilika. Source ITV 
Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top