Mpenzi msomaji wa makala hii, napenda nikwambie kitu kwamba siku izi watu wengi wanapenda kuanzisha biashara zao binafsi uku lengo lao kuu nikuachana na kuajiliwa kisha wajiajiri wenyewe na kujipatia kipato kupitia biashara zao walizo zianzisha.
Biashara za kufanya ziponyingi sana hapa duniani,ambazo ukizisimamia vizuri zinakutimizia marengo yako.
Mbali ya kwamba biashara nyingi zenye faida ya haraka ni zile biashara ambazo zina madhara makubwa kwa afya wa wanadamu mfano waweza kuwa Sigara, Pombe, madawa ya kulevya nk.
Ila zipo biashara ambazo nazo zinakuwa na faida japo kuwa inapatikana taratibu na uchukua mda mrefu kidogo kuonekana tofauti na biasha nilizo tangulia kuzitaja hapo juu.
Biashara izo ni pamoja na Unga wa Sembe, Sukari, mafuta ya kula, Pipi, jojo, soda, maji, madaftari, karamu, nk. Sasa basi, ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yako yoyote ile utakayokuwa umeichagua kuianzisha unatakiwa kuwa na mipango mazubuti juu ya usimamizi na uendeshaji wa biashara yako.
Mipango iyo nipamoja na kujua namna ya kutenganisha faida na pesa ya mtaji, kuweza kujua namna ya kuendesha mfumo mzima wa mauzo pamoja na manunuzi, kulipa mishahara nk.
Angalizo, huwezi kufanya biashara bila kumbukumbu, biashara yoyote ile inahitaji utunzaji wa kumbukumbu, usipoweza kipengele hiki basi jua kabisa wewe huwezi kufanya biashara yenye tija, bali unaweza kufanya biashara ya mazoea tu basi. Kujaribu sio kushindwa ebu anza leo uone miujiza ya biashara.