Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka ulimwenguni, ingia hapa kujua nani anaongoza

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka ulimwenguni ambapo mpaka sasa Argentina ndio inayoongoza duniani.


Kwa upande wa Afrika Senegal ndio vinara na ipo nafasi ya 33 ulimwenguni, huku wakifuatwa na Ivory Coast katika nafasi ya pili ambapo wanafungana na Tunisia kwenye Nafasi hiyo na nafasi ya 36 ni Misri na wapo nafasi ya 34 ulimwenguni.

Majina ya wasanii watakaowania tuzo za EATV yatajwa, bofya hapa kuyaona

Awamu ya kwanza ya kutaja majina ya wasanii watakaowania tuzo za EATV kwa mwaka huu wa kwanza yametajwa Jumanne hii. 

Kwa kuanzia yametajwa majina ya wasanii kutoka katika vipengele viwili kati ya kumi vilivyopo kwenye tuzo hizo huku zoezi hilo likitarajiwa kufanyika kwa siku nne ambapo litakamilika Ijumaa hii ya Novemba 11. 

Hii ni orodha ya wasanii waliotajwa kwenye vipengele hivyo. 

Mwanamuziki bora chipukizi 

Man Fongo 
Feza Kessy 
Ruky Baby 
Mayunga 
Bright 

Muigizaji bora wa kiume 

Saidi Ali – Ndugu wa mume 
Meya Shabani – Profile 
Daudi Tairo (Duma) – 
Salim Ahmed (Gabo) – Safari ya Gwalu 
Dotto Matotora – Likwacha Lala

JUMA NYOSSO anaendelea kutumikia adhabu yake ya ‘kikatili’-kutokucheza soka kwa miaka miwili kwa kosa la kumshika sehemu ya makalio nahodha wa Azam FC

JUMA NYOSSO anaendelea kutumikia adhabu yake ya ‘kikatili’-kutokucheza soka kwa miaka miwili kwa kosa la kumshika sehemu ya makalio nahodha wa Azam FC, John Bocco na bahati mbaya zaidi rufaa yake ‘imewekwa kapuni’ kwa mwaka mmoja sasa.

Najiuliza sana, ‘hivi ni kweli soka ni mchezo wa kiungwana?’ Katika nchi zilizoendelea wanaamini soka ni mchezo wa kiungwana ndio maana matukio yote yanayojiri katika mchezo huu huchukulia ni ya kiungwana.

Soka lina kanuni/sheria zake ambazo zinaufanya mchezo huu kuwa na maana ya fair play. Kama, Nyosso alipewa adhabu kubwa vile, ni kwanini basi, Agrey Morris anaendelea kuwaumiza wachezaji wenzake na hachukuliwi hatua za kinidhamu?

Jumatano ya wiki iliyopita mlinzi huyo wa Azam FC alimchezea faulo mbaya mshambulizi wa Stand United, Mnigeria, Chidiebere Abasirim na kumvunja taya.

Hakuna aliyekemea hilo. Labda ni kwasababu ya urafiki ama uoga. Aggrey ni ‘mkatili’ kuliko Nyosso ndiyo maana alifanya jaribio lingine la kutaka kumvunja mshambulizi wa Yanga SC, Mzambia, Obrey Chirwa katika pambano la jana Azam FC 0-0 Yanga SC.

Misimu miwili iliyopita mlinzi huyo wa kati wa timu ya Taifa ya Zanzibar alimchezea rafu mbaya aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi kiasi ambacho watazamaji wote wa mechi ile walihamaki na kudhani labda Okwi atakuwa ameumizwa vibaya.


Agrey si muungwana na licha ya kwenda kumjulia hali, Chidiebere siku moja baada ya kumuumiza kwa makusudi mchezaji huyo alikuwa tayari kumuumiza pia Chirwa.

Uungwana ni vitendo wala si maneno matupu na katika hili la Aggrey dhidi ya Chidiebere TFF inapaswa kuchunguza kisha kuchukua hatua ya kumfungia mchezaji huyo wa Azam FC ili kumuonya vinginevyo atakuja kuua mchezaji mwenzake uwanjani.

Jamaa anacheza vibaya sana na nashangaa anaendelea kupata mashabiki, labda kwa vile matukio yake yote ya kutisha ameyafanya kwa wachezaji wa kigeni.

Kumfungia Nyosso miaka miwili na kushabikia vitendo vya kihuni kupitiliza vinavyofanywa na Aggrey si haki.

Ombi langu kwa TFF ni kulichunguza tukio la kuumizwa kwa Chidiebere na kutafuta tukio lile la Agrey dhidi ya Okwi kisha kutazama mechi ya jana ya Azam v Yanga ili kupata kujiridhisha zaidi kuhusu tabia mbaya kiuchezaji ya mlinzi huyo wa Azam FC.

Kama Nyosso alifungiwa kwa kumshika Bocco sehemu ya makalio na kumuacha Agrey na ukatili wake akiendelea kuwaumiza wenzake si haki. Kumfungia Nyosso na kushabikia ‘ukatili’ wa Aggrey Moris si haki, TFF ifanye uchunguzi.

Wimbo mpya wa msanii Bexy wa Music-Nisamehe uko hapa

Wimbo mpya wa msanii Bexy wa Music unaokwenda kwa jina la Nisamehe uko hapa.


Waweza kuusikiliza na=> Download hapa <=


Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D-Ommy, washindi tuzo za Afrimma 2016

Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D-Ommy, wameibuka washindi kwenye tuzo za Afrimma 2016, zilizofanyika Dallas, nchini Marekani Jumamosi hii.

Diamond ameibuka tuzo ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki, Harmonize Msanii bora chipukizi na D- Ommy, DJ bora wa Afrika.


“Team Tanzania Mungu ni mwema siku zote,” ameandika Harmonize baada ya ushindi huo.

Hapo juu ni Harmonize akiwa na Akothee aliyeshinda tuzo ya msanii bora wa kike Afrika Mashariki na Willy M Tuva. Diamond na D-Ommy hawakuwepo kwenye tuzo hizo.

Help me with your phone please...you know what happen after phone?? Click here and see

Help me with your phone please...you know what happen after phone?? Click here and see 
Updating status.. accident... waiting ... ambulance to take me hospital.

KAMA UNATAKA KUCHEKA EBU FUNGUA HABARI HII UTACHEKA MPAKA BASI

1. Juma: Uwa bibi yako anasoma Biblia??
Naumi: Ndio ni kweli uwa anasoma biblia, tena usoma usiku na mchana.

Juma: Ivi unahisi ni kwanini uwa anasoma sana biblia kiasi hicho??
Naumi: Nahisi anakalili kwa ajili ya siku yake ya mwisho. 

2. Mwalimu akamuuliza "John kwa nini umechelewa kufika shuleni??"
John akamjibu Mwalimu "Ni kwa sababu ya alama za barabarani"

Mwalimu akamuuliza tena "Alama gani?"
John akamjibu "Zile alama zilizoandikwa nenda pole pole shule iko karibu"

"Kutoka maktaba"
3. Msichana akamuuliza muhudumu wa train "Hii ndiyo train yangu??
Muhudumu akamjibu yule dada "Hapana train hii ni mali ya shirika la Reli

Msichana akasema "Acha kunichekesha. Namaanisha kuwa naweza kuchukua train hii mpaka New Delhi??"
Muhudumu akamjibu "Hapana dada. Kwanza naogopa maana train hii ni nzito sana huwezi kuinyanyua hata second 1.

4. Mvurana alikuta Miss call kwenye simu yake. Akaenda shule kisha akamuuliza mwalimu wao wa kike aitwaye Miss. "Miss kwa nini jana umenitumia call??"

Mwalimu huyo akamjibu mtoto yule "Hapana mimi sijakutumia call?

Mtoto akajibu, "Ok, vizuri "mimi jana niliporudi nyumbani simu yangu ilisema nimepata Miss call"

MAHUSIANO: Mume wangu ana miezi miwili sasa halali nyumbani anarudi kila siku asubuhi kubadilisha nguo.

MAHUSIANO: Mume wangu ana miezi miwili sasa halali nyumbani anarudi kila siku asubuhi kubadilisha nguo. Nimegundua amepata mchepuko ambaye ni Sekretari wake ofisini.

Amefikia mpaka hatua ya kumtambulisha kwa watoto wangu. Nafikiria kuomba talaka. Tupe maoni yako juu ya wanaume kama hawa kwenye ndoa.

DAKIKA 20 ZA KUJIACHIA NA DJ TASS KUTOKA TANZANIA, BOFYA HAPA

Msikilize mkali wa kupiga mixing za hatari hapa nchini Tanzania akifahamika kwa jina la kazi kama Dj Tass. Jamaa ni hatari sana.

Msikilize sasa akiwa live akifanya yake

         {{ CLICK HERE /BOFYA HAPA }}

MZEE PITA HAPA MBELE TUKUHUDUMIE MZEE WETU, BOFYA HAPA KUONA MAJIBU YA MZEE

UJIO MPYA WA WIMBO WA NIKUPE NINI KUTOKA KWA MSANII PIANO

Mambo vp watu wangu wa nguvu!
Jumapili hii ndo naachia wimbo wangu unaitwa NIKUPE NINI. Mimi bila wewe siwezi xo naomba sapot yako mdau wangu wa nguvu Mutalemwa.

Shukrani kwako unaenisapot also kwa maproducer wangu Robby Touchz & Alfredy Mjema kwa kuhakikisha mambo yanakaa sawa. Nini maoni yako kwake Piano??

JERRY MURO AITWA KAMATI YA MAADILI TFF, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

MKUU wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanha Jerry Muro ameitwa kwenye kikao cha kamati ya maadili cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufuatia kitendo chake cha kupingana na kuishambulia katika kuelekea mechi yao ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho Barani Afrika uliofanyika Juni 28.

Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Muro kuitwa na anatakiwa kufika Julai 02 katika ofisi za TFF saa Nne asubuhi au kama atashindwa kufika basi atume mwakilishi wake au utetezi wake kwa njia ya maandishi.

Muro amethibitisha hilo na kusema kuwa amepokea barua hiyo na hii ikiwa ni mara ya tatu na katika mara zote amekuwa anashinda kwa hoja na kwa. wakati huu mkakati wao mkubwa kuona nafungiwa kujihusisha na masuala ya mpira na zaidi anashangaa ni jinsi gani wanasema amewashambulia kupitia vyombo vya habari.

Barua hiyo inamtaka Muro kujitokeza siku hiyo au hata kama hatoweza kufika basi atume utetezi wake kwa maandishi au mwakilishi wake na hata kama hatofika basi kikao cha kamati ya maadili kitaendelea kama kawaida na watatoa maamuzi kama kawaida.

KUTOJUA KINGEREZA SIO DHAMBI ASEMA PROFESSOR JAY, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Msanii wa Hip Hop na Mbunge wa Mikumi, Professor Jay amesema kutokujua Kiingereza siyo dhambi. "Hii sijui kiingereza,

Kiingereza ni Kushoboka tu. Viongozi wengi mbona tunaona wanakuja hapa Tanzania hawajui Kiingereza." Kwa upande wako unadhani kuna umuhimu wowote wa kukijua kiingereza?

HII NDIO TOFAUTI KATI YA NENO WEDDING NA WELDING, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Injinia aliulizwa swali kwamba kuna todauti gani kati ya welding ambayo inamaanisha kuchomelea na wedding neno lenye maana ya harusi?? Ikafika zamu ya injinia huyo kujibu maswali hayo mawili, akaanza kwa kusema maneno yafuatayo hapo chini.

Tofauti siokubwa sana kwasababu zote ni viungo, ila kwenye welding kuna cheche kwanza na kisha kitu kinachokuwa kimechomelewa kinaungana milele.

Wakati kwenye wedding watu mnaungana kwanza kisha cheche zinafuata baadae.

Kwaiyo tofauti ya welding na wedding ni utokeaji wa cheche tu basi kwaiyo ni vyema ndoa ikawa na tabia kama ya kuchomelea ili cheche ianze kisha watu waungane milele na sio kuungana kwanza kisha cheche zikafuata.

TAZAMA VIDEO IKIMUONYESHA DEMBA BA ALIVYO VUNJIKA MGUU AKIWA UWANJANI

Hapo ndipo inapofikia mwisho safari ya mpira ya Demba ba, mungu amjaalie hapone kama umeguswa type amen.

Tazama video inayo muonyesha mchezaji huyo alivyo vunjika mguu akiwa uwanjani akicheza mpira [ BOFYA HAPA ]

KWANINI NDOA HAZIDUMU?? MAJIBU YOTE YAKO HAPA

Kwanini ndoa hazidumu?? Majibu yako hapa

Ndoa zina haribiwa na vitu vingi sana ila kwa siku ya leo tutazungumzia juu ya kitu kinachoitwa "USHIRIKINA" kwenye ndoa zetu za kiafrika.

Ushirikina ndani ya ndoa pia ni jambo ambalo kwa kiasi kikubwa sana huchangia ndoa nyingi sana kuvunjika, na kuleta madhara makubwa kwa wale waliofanyiwa ushirikina huo.

Ushirikina huo hufanyiana wao wanandoa wenyewe kwa wenyewe au hufanywa dhidi yao (yaani hufanyiwa na watu baki).

Tukianza na wanandoa wenyewe kwa wenyewe kufanyiana ushirikina, na itatubidi tuangalie pande zote mbili ili kuweka mambo sawa, upande wa wanaume, pia na upande wa wanawake.

Tuanze na upande wa wanawake: Wanawake wengi wamekuwa wakienda mbio kufanya ushirikina wakiwa ndani ya ndoa au wakiwa wameachika, na wakiwa ndani ya ndoa zao huwa wanafanya hivyo kwa malengo mengi miongoni mwa malengo hayo ni pamoja na;

1. Kuwafanya waume wao wazidishe mapenzi zaidi kwao. Kwa dhana zao mbovu kuwa mapenzi huzidishwa kwa kupitia uchawi, ndugu zangu akina mama na akina dada, mapenzi ya kweli na ya dhati hayazidishwi kwa nguvu za giza (uchawi), wala limbwata, ilo mlitambue.

Sio mapenzi ya dhati kwa sababu kinachofanywa ni kuwa mume huyo anavishwa jini ambalo huumfanya imma, apende, achukie, aache, awe mtiifu na mambo mengine kama hayo.

Ila utambue kuwa mapenzi ya kweli huzidishwa kwa kuhurumiana, kuenziana na kustahamiliana katika shida, raha na kusameheana kwa kosa kubwa au dogo na hayo yote ili yapatikane kwenye ndoa yenu lazima mume na mke wote kwa pamoja muwe ni wachamungu.

2. Kuwafanya waume zao kuwachukia wake wengine kama ni ndoa ya wake zaidi ya mmoja, ili aachike au waachike wengine abakie mwenyewe, na hii kutokana na wivu wa kipumbavu, uchoyo, roho mbaya na hasadi walizonazo wenye mioyo yao.

                     Picha kutoka maktaba 

3. Kufanya mume asiwe na maamuzi yeyote katika ndoa yake, badala yake abaki kuwa mtekelezaji tu wa chochote kile atakachoamrishwa na mkewe, kiwe cha halali au cha haramu, kiwe kinawepesi au kinauzito bwana huyo atafanya kwa sababu sio yeye bali anakuwa chini ya nguvu za jini alilovishwa.

4. Anapokuwa mwanamke ameachika lengo kubwa la kufanya ushirikina ni kumfanya mume huyo amrejee, au kumtia matatizo huyo mwanaume ili asiweze kuoa tena, au kila akioa mke mwingine asiweze kudumu naye, au kumfanyia ushirikina wenye kumpunguza nguvu za kiume, au kumuathiri kiuchumi, au kumfanya apate wazimu, au hata kumuua, au kumsababishia matatizo mengi.

Sasa tuangalie ushirikina kwa upande wa wanaume; pia nako huku tunakuta kuwa wanaume nao wanafanya ushirikina katika ndoa zao wakiwafanyia wake wao kwa malengo kama yafuatayo hapo chini.

1. Kumdhibiti mke muovu ili awe mwema. Jambo ambalo halina ukweli wowote kwa sababu njia ya kumuelekeza na kumsaidia mtu si kwa kutumia ushirikina, bali ni kurekebisha ufahamu wake kwa kutumia maneno yenye nguvu ya Mungu.
(Hakuna kitabu cha dini kinacho mruhusu mwanadamu kutenda dhambi au maovu).

2. Vile vile wanaume hufanya ushirikina kwa lengo la kuwafanya wake wawe watiifu zaidi na waogope kuzini nje ya ndoa zao, hufanya vile wakimaanisha kwamba wake zao wakizini tu nje ya ndoa basi waume hao wajue, au wakizini nje ya ndoa zao wagandane na hao waliozini nao, watu wa pwani wanaita/sema “tego”.

3. Pia kama watakuwa wamewaacha hao wake zao hufanya ushirikina kwa lengo la kurudiana nao, au kumhusudu katika mambo mbalimbali kama kumtia maradhi kama vile; kutokwa damu nyingi sehemu za siri, kumfanya asizae, au asiolewe na mume mwingine nk.

Mara nyingi ushirikina kama huu hufanywa na wanaume hao hasa kama ukorofi wao ndio uliopelekea wake zao kudai talaka, au kuachishwa kinguvu, hali ya kuwa wao bado walikuwa wanawahitaji hao wake zao.

Ebu tuangalie ushirikina ambao unakuwa ni dhidi ya wanandoa; ushirikina ambao unakuwa ni dhidi ya wanandoa ni ule ushirikina wa watu wenye husuda wasiotaka kuona ndoa za watu zinadumu, na watu kuishi kwa raha na maelewano.

Na wakati mwingine watekelezaji wa ushirikina wa namna hii ni wanafamilia au wana ukoo kama Baba, Mama, Dada, Shangazi, Mjomba au watu wengine wa nje ya familia na ukoo huo.

Niwakati wako wa kujitafakari ukiwa kama mwana ndoa, je uko upande gani? Na kwa nini umeamua kuwa upande huo?

IZI NI TETESI ZA SOKA KUTOKA MAJUU, INGIA HAPA KUJUA ZAIDI

Manchester United wamewaambia Juventus kuwa wako tayari kulipa pauni milioni 100 kumsajili kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, na watampa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki (Mail on Sunday).

Arsenal watampa mkataba mpya Arsene Wenger kwa matumaini ya kumshawishi asiondoke baada ya tetesi kuzagaa kuwa chama cha soka cha England, FA, kinamnyatia (Observer), meneja mpya wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 85, pamoja na kiungo Mjerumani

anayechezea Real Madrid, Toni Kroos, 26, ambaye kipengele chake cha uhamisho kina thamani ya pauni milioni 63 (Sunday Mirror), mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wamekubali kumsajili kiungo kutoka Poland anayechezea Sevilla Gregorz Krychowiak, 26, kwa pauni milioni 22 (Marca)

Liverpool watapambana na Everton katika kumsajili kiungo kutoka Ubelgiji Axel Witsel, 27, anayecheza soka Zenith St Petersburg nchini Urusi (Sunday Mirror), mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Robin van Persie, 32, huenda akarejea katika Ligi Kuu ya England baada ya klabu yake ya sasa Fernabahce ya Uturuki kuwaambia West Ham na Crystal Palace kuwa wanaweza kumsajili (Sun on Sunday)

Chelsea wamefanikiwa juhudi za kumsajili beki kutoka Senegal, Kalidou Koulibaly, 25, anayechezea Napoli kwa pauni milioni 30 (Sunday Mirror)

Tottenham wanajiandaa kutoa pauni milioni 38, kumtaka mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi, 23, na tayari wamepeleka wawakilishi wao Italy kuzungumza na mchezaji huyo kutoka Argentina (GianlucaDiMarzio)

kipa wa Spurs Hugo Lloris, 29, ananyatiwa na Real Madrid kwa pauni milioni 35 (Sunday Mirror), meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino yuko tayari kumuuza Ryan Mason, 25, kwenda Hull City iliyopanda daraja kwa pauni milioni 10 (Sun on Sunday),

kiungo wa Watford Jose Manuel Jurado, 30, amehusishwa na kuhamia Espanyol na kuungana na meneja wake wa zamani Quique Sanchez Flores (Fichajes),

Middlesbrough watakamilisha usajili wa pauni milioni 11.75 wa kiungo kutoka Atalanta, Marten de Roon, 25, baada ya kukubaliana maslahi binafsi na mkataba wa miaka minne (Gazette), timu nne za EPL zimekuwa zikiwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Wales, Hal Robson Kanu tangu alipopachika bao dhidi ya Ubelgiji kwenye michuano ya Euro 2016.

Kanu ni mchezaji huru baada ya kuachiliwa na klabu yake ya Reading (Sky Sports), Stoke huenda wakalazimika kulipa takriban pauni milioni 20 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22 (Stoke Sentinel). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

LIONEL MESSI AJIUZULU BAADA YA KUKOSA PENALTI, ZAIDI INGIA HAPA

Mshambulizi wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amestaafu kutoka soka ya kimataifa. Mchezaji huyo bora zaidi duniani alitangaza hatua hiyo baada ya kukosa penalti iliyoiwezesha Chile kuilaza Argentina katika fainali ya mchuano wa Copa America.

"Kwangu mimi ,soka ya kimataifa ama hata kuichezea Argentina sitaweza tena.
''Nimefanya kila niwezalo.''

''Kwa kweli inaniumiza kuwa sijawahi kutwaa kombe lolote la kimataifa'' alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa mia 29.

Mshambulizi huyo ameisaidia mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Barcelona, kutwaa mataji 8 na mataji manne ya ubingwa wa bara ulaya.

Hata hivyo kimataifa Messi amewahi kushinda taji moja tu lile la nishani ya dhahabu ya Olimipiki ya mwaka wa 2008 Olympic.

Argentina imeshindwa katika fainali tatu za kimataifa. Argentina imeshindwa katika fainali tatu za kimataifa.

Argentina walilazwa moja kwa nunge na Ujerumani katika kombe la dunia la mwaka wa 2014 huko Brazil. Timu hiyo aidha imeshindwa na Chile mara mbili katika fainali za mchuano wa Copa America kupitia kwa mikwaju ya penalti.

Messi vilevile alikuwa katika kikosi kilichoshindwa na Brazil katika mchuano huo wa mwaka wa 2007 wa Copa America. Argentina walitoka sare ya 0-0 baada ya muda wa kawaida na ule wa ziada.

Akiwa Uhispania Messi ametikisa wavu mara 453 kati ya mechi 531 alizoshiriki.
Hata hivyo Chile waliibuka videdea kwa mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalti.
Messi alipoteza mkwaju wa kwanza.
Akiwa Uhispania Messi ametikisa wavu mara 453 kati ya mechi 531 alizoshiriki.

Aidha Messi ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa La Liga akiwa na mabao 312.

NDIYE HUYU ALIYECHEZA MOVIE YA YESU (JESUS), HISTORIA YAKE IKO HAPA

Anajulikana kama Brian Beacon, yeye ni muigizaji maarufu duniani aliyeigiza filamu ya Yesu (Jesus). Alizaliwa mnamo tarehe 13/02/1946 kwenye mji wa Oxford nchini Uingereza (UK). Alijifunza sanaa katika chuo cha Oxford Youth Theatre cha humo nchini mwao.

Msanii huyu amepata kuigiza filamu kama The Triple Echo ilikuwa mwaka 1972, na miaka miwili baadae akafanya filamu inayofahamika kama Vampyres ambapo ilikuwa mwaka 1974, Lakini pia mwaka 1979 alifanya filamu ambayo ilikuwa gumzo dunia nzima filamu ya Yesu (Jesus) hadi ikafikia watu wengi tukawa tunahisi ndiye yesu kweli kutokana na jinsi alivyovaa uhusika (character).

Na mnamo mwaka 1985 alicheza filamu ya A Zed and Two Noughts. wasambazie na wenzio ili wamjue vizuri huyu msanii kwa kipaji chake alichokitumia kwa kuvaa mfano wa maandiko matakatifu na kuufikishia ulimwengu ujumbe stahiki.

IKIWA NI SIKU MOJA BAADA YA TCRA KUZIMA SIMU FEKI NCHINI TANZANIA

Ikiwa ni siku moja baada ya mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzanian TCRA kuzima simu feki
Matokeo yake yamekuwa kama unavyoona kwenye iyo picha hapo juu, simu imegeuka gari la kuchezea watoto.
Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top