Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MINI SHOP CHETA

Mini ShopCheta au Duka Dogo

Ni duka dogo kweli kama jina lake linavyojieleza hapo juu. Duka hili linatoa huduma ya mahitaji ya kawaida ya kila siku kwa wakazi wa Kitongoji cha Cheta pamoja na maeneo ya jirani au kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mini Shop inatoa huduma ya jamii kwa watu wote. Mini Shop ilianzishwa tangu mnamo tarehe 18/01/2018.

Tulianza tunauza bidhaa chache sana, bidhaa izo ilikuwa ni pamoja na Dawa ya Mbu zile za vidonge za kuchoma, Viberiti, Karanga, Ubuyu pamoja na Tauro za wanawake (Ped). Na kipindi icho tulikuwa tunauza bidhaa izo kutokea nyumbani kabla ya kujenga Frem hii rasmi ya kufanyia biashara kama inavyo onekana hapo kwenye picha.

Mini Shop a.k.a Duka Dogo tunauza bidhaa mbali mbali ila kwa ucheche tu, zifuatazo ni baadhi ya bidhaa tunazouza. 

Maji
Pipi
Unga
Tambi
Ngano
Amira
Juice
Mikate
Sigara

Chumvi
Mchele
Sukali
Karamu
Battery
Viwembe
Vitunguu
Viberiti
Biscuits
Madaftari

Vichongeo
Majani ya Chai
Dawa ya Mswaki
Jumbo Ball Gum
Sabuni za kuogea
Mafuta ya kupaka
Viungo vya Pirau
Mafuta ya kupikia
Sabuni za kufuria

Maharage ya Njano
Maharage ya Kombati
Tauro za wanawake (Ped)
Pon Pon au Bambino za watoto wachanga
Pia Mini Shop ni wakala wa Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Karibu sana dukani kwetu, karibu sana Mini Shop_Cheta tukuhudumie leo.


TAFITI JUU YA MAAMBUKIZI YA HIV/AIDS KWA KIZAZI KIPYA

Ndugu msomaji tafiti hii mpya inayohusu maambukizi mapya ya ugonjwa HIV/AIDS inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waathirika ni vijana wakifuatiwa na watu wazima.

Kuna mambo mengi yameelezwa ndani ya report hii ikiwemo njia za kuepuka usiambukizwe na jinsi unavyoweza kuambukizwa nk. Ili kuyasoma yote hayo bofya [HAPA]

Wanawake wanaokunywa pombe kupita kiwango wapo katika hatari ya kuathirika maini

Wanawake wanaokunywa pombe kupita kiwango kinachokubalika wapo katika hatari ya kuathirika maini mapema kuliko wanaume.
Mkurugenzi wa kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa mama, baba, mtoto na vijana, Dk. Ali Mzige, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na NIPASHE.

Alisema hali hiyo inatokana na mfumo wa mwili wa mtu kutofautiana na wa mwingine na pia kutegemeana na aina ya pombe na kiasi anachokunywa.

Dk. Mzige alisema kitaalamu mwanamke anapaswa kunywa chupa moja ya bia kwa siku na mwanaume chupa mbili.

Hata hivyo, alisema hivi sasa wanawake wamekuwa wakinywa kupita kiasi mijini na vijijini, kitu ambacho ni hatari kiafya.

"Wanywaji wa pombe wa muda mrefu, ambao tunaweza kuwapa jina la ‘chapombe' wanaanza kuwa na dalili za afya zao kuyumba na kutetereka wanapofikia umri wa miaka 30-40," alisema Dk. Mzige.

Alizitaja athari wanazopata wanywaji wengi wa pombe kuwa ni pamoja na sukari mwilini kushuka, protini mbalimbali na za kiwango tofauti kushuka, shinikizo la damu, nguvu za kiume na za kike kupungua, kumbukumbu kupungua na baadaye kupotea kabisa.

Alisema pia mtu yeyote ambaye ini lake limeharibiwa na pombe, maumivu makali, homa, kukosa hamu ya kula chakula na kichefuchefu.

AFYA YAKO KARIBIA ASILIMIA 90 ZOTE ZIKO HAPA, FUATA MAELEKEZO SASA

Kupashana habari nijambo ambalo halina mipaka na pia ukumbuke ya kwamba habari waga haina mwisho.

Kama habari waga haina mwisho basi napenda nikukalibishe wewe ili ujifunze mambo mengi kupitia ujumbe uliopo hapo juu, fuata maelekezo ili kujifunza.

BOFYA HAPA KUYAJUA MAAJABU YA HARUFU YA KUKU

Utafiti umebaini kuwa harufu ya kuku inaweza kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria. Watafiti nchini Ethiopia na Sweden wamegundua kuwa

mbu wanaobeba vimelea visababishavyo  Malaria huwa wanafanya kila wawezalo kukaa mbali na kuku wanaofugwa majumbani. Nini maoni yako?

UGONJWA WA KIPINDUPINDU WASAMBAA KWA NJIA YA SAMAKI ZAIDI BOFYA HAPA

Watu tisa wamelazwa katika zahanati ya Mpekenyela wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi baada ya kula samaki wanaosadikiwa kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Kipindupindu na kuwasababishia kuhara na kutapika na  kupoteza nguvu.

Kufuatia tukio hilo wafanyabiashara wawili wa Samaki katika kata ya Mpekenyela na Namungo wilaya ya Ruangwa Somoe Kishoka na Fatuma Saidi wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuuza samaki wenye vimelea vya Kipindupindu.


Akizungumzia tukio hilo mganga mfawidhi wa zahanati ya Mpekenyela Mikidad Mbule  anathibitisha kupokea wagonjwa hao,huku ndugu wa mgonjwa aliyelazwa  kutokana  na maambukizi anaelezea hali hiyo ilivyomkuta.


ZIFUATAZO NI DAWA ZILIZOFUTIWA USAJILI, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Dawa zifuatazo zimefutiwa usajili na shilika la chakula na dawa TFDA Tanzania.

1. Dawa ya Fungus ya vidonge Ketoconazole inasababisha madhara kwenye ini(Hepatotoxicity)

2. Dawa ya maji ya malaria Amodiaquine-ikitumika peke yake inaleta usugu wa vimelea vya malaria (Drug resistance)

3. Dawa ya maji ya kutibu  mafua na kikohozi aina ya PHENYLPROPANOL AMINE inaleta madhara hatarishi kama kiharusi(Haemorrhagic stroke)

4. Antibiotic ya sindano Chlorampenicol Sodium Succinate ya India pamoja na Cloxacillin capsule zinasababisha shida ya kupumua na kupoteza fahamu.


KITUO CHA AFYA CHA MWENDAKULIMA KINAKABILIWA NA UPUNGUFU WA DAWA NA VIFAA TIBA, ZAIDI BOFYA HAPA

Kituo cha afya cha Mwendakulima kinakabiliwa na upungufu wa dawa na vifaa tiba Shinyanga.

Kituo kipya cha afya cha Mwendakulima kilichoko wilayani Kahama katika mkoa wa Shinyanga kinakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa dawa, vifaatiba pamoja na uhaba wa wahudumu hali ambayo inasababisha wananchi wanaoishi katika kijiji hicho kufuata huduma za kiafya katika vituo vilivyoko katika vijiji vya jirani wakihofia kutopata huduma bora katika kituo hicho cha afya cha Mwendakulima.

Akizungumzia changamoto zinazokikabili kituo cha afya cha Mwendakulima ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa kampuni ya ACACIA inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi muuguzi mfawidhi katika kituo hicho Bi.Selestina mbezi ameiomba serikali kupeleka wahudumu wa afya katika kituo hicho pamoja na kukipatia dawa na vifaa tiba vya kutosha ili kuokoa maisha ya wananchi wanaotumia muda mrefu kufuata huduma za kiafya katika vituo vingine vilivyoko mbali na kijiji hicho hali inayotishia kupoteza maisha ya wagonjwa hususan wanawake wajawazito.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Mwendakulima Bw.Mussa Ibingo amedai kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni ya ACACIA katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii hivyo kuna kila sababu za kuhakikisha serikali inapeleka dawa na vifaatiba vya kutosha katika kituo hicho mapema iwezekanavyo huku baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakitibiwa katika kituo hicho cha afya wakionyesha kuridhishwa na kuduma waliyoipata.

MAMBO 10 YANAYOWEZA KUARIBU FIGO LAKO, BOFYA HAPA KUYAFAHAMU

Ndugu mdau wa Mutalemwa Blog, leo nimekuletea mambo 10 ambayo yanaweza kusababisha kuaribika kwa figo lako la mwili, endapo utayafanya kwa mara nyingi kupita kiasi chake.

1. Kutokukojoa mapema mkojo ukikushika
2. Kutokunywa maji ya kutosha
3. Kula chumvi sana kwenye chakula.
4. Kutokujitibu magonjwa ya kawaida kwa haraka na vizuri
5. Kula nyama sana

6. Kutokula chakula cha kutosha 
7. Kutumia Vidonge vya kukata maumivu kwa wingi 
8. Kutokula kwa wingi vyakula vyenye virutubisho 
9. Kunywa pombe kupita kiasi 
10. Kutopumzika vya kutosha.

HABARI ZA HIVI PUNDE: VIGOGO WA 4 WASIMAMISHWA KAZI, ZAIDI BOFYA HAPA

Wairi wa afya, maendeleo ya jamii,  jinsia watoto na wazee mhe.

Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi vigogo wanne 4 wa bohari ya dawa Msd kanda ya Dar-es-Salaam kwa upotevu wa fedha kiasi cha Tsh 1.5Billion.

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA SULUHISHO LAKE.

Nguvu za kiume Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.

Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.

Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya.

Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli, kisukari, shinikizo la damu na hata uzito ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa. Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni lazima udhurike kwanza.

Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

Dawa za nguvu za kiume za asili:

1. Kitunguu swaumu. Chukuwa punje 8 mpaka 10 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja.

2. Tikiti maji, faida za tikiti maji kiafya. Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi siku zote.

3. Ugali wa dona. Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.

4. Chumvi ya mawe. Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.

5. Maji ya kunywa. Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.

Umeipenda makala hii?? Jiunge na wasomaji wengine zaidi ya 200,000 kwenye blog hii Au like page yetu ya Facebook iliyopo=> HAPA <= na uwe mtu wa kwanza kupata makala mpya kila zinapoandikwa humu au kuandikwa kwenye mtandao wetu wa Tazama Line.

6. Mbegu za maboga pumkin seeds. Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 30 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako.

7. Asali na Mdalasini. Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

8. Unga unga wa udishe. Unga wa mti wa udishe ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwani huimarisha sana mishipa ya uume. Udishe inapatikana pia katika mfumo wa juisi. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari pia unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama.

Udishe pia unatibu magonjwa yafuatayo bila shida yoyote; Pumu, Chango la uzazi, Kupooza mwili, Unaondoa kabisa gesi tumboni na Kuongeza nuru ya macho kuona.

Udishe unao uwezo pia wa kuongeza ukubwa wa uume wako. Labda utauliza kwa namna gani?, kwa sababu moja ya kazi zake mwilini ni kuponya mwili uliokuwa umepooza, mwili unapokuwa umepooza ina maana hata damu yako pia inakuwa haitiririki vizuri kama inavyotakiwa na tuliona hapo juu kwenye somo hili umhimu wa mzunguko wa damu ulio bora katika nguzu za kiume.

Kwa kuwa mwili ulikuwa umepooza, udishe unapokuja kukutibu inakufanya kuwa mtu uliyechangamka na damu yako itaanza kuwa inatiririka kwa mtiririko mzuri zaidi na kama matokeo yake utaanza kuona hata ukubwa wa mheshimiwa unaanza kuongezeka kidogo kidogo. Na hii ni hasa kwa wale ambao walizaliwa na uume wa kawaida lakini sababu ya punyeto, lishe duni au stress walijikuta maumbile yao yanaanza kusinyaa au kupungua badala ya kuongezeka.

Namna ya kutumia udishe. Kama ipo katika mfumo wa unga: – Chemsha maji nusu lita ongeza kijiko kidogo cha chai cha unga huu, unaweza kuongeza pia asali vijiko viwili au vitatu na unywe kama chai kutwa mara 2, yaani asubuhi nusu lita na jioni tena nusu lita nyingine.

Kama ipo katika mfumo wa juisi:- Ukiamka asubuhi unamimina dawa robo litaya dawa (ml 250), unakunywa yote na jioni tena robo lita nyingine, na dozi moja inachukuwa siku 11.

TAARIFA MHIMU – Juisi ya udishe ndiyo nzuri zaidi kuliko unga wake sababu inakuwa ni fresh zaidi, na wanaume wengi waliotumia juisi wanarudisha majibu mazuri zaidi kuliko wale waliotumia unga, hivyo kuanzia sasa udishe inapatikana katika mfumo wa juisi tu. Hivyo ukija WhatsApp au ukituma sms uliza moja kwa moja ‘Juisi ya Udishe ipo’?. Pia si vibaya kama utanieleza kiundani tatizo lako lipoje hasa na siyo kuuliza tu dawa peke yake.

Unahitaji juisi ya udishe, Asali yenye mdalasini  au mbegu za maboga? Basi muachie ujumbe kwenye WhatsApp +1 805 855 1133,  Au kama unataka jibu la haraka zaidi muandikie sms ya kawaida dk kwenye namba 0769142586 (acha tu ujumbe atakujibu). Tegemea kujibiwa kila baada ya lisaa limoja au masaa mawili. Ukiona amechelewa sana kukujibu usiache kumtafuta tena hata siku inayofuata.

UMUHIMU WA TENDE NA KAZI ZAKE

leo ni siku ya Jumapili nyingine tena napenda tufahamishane kuhusu hizi faida kadhaa za tende pamoja na umuhimu wake.

Tende ni tunda ambalo linaongoza kwa kuliwa sana katika kipindi cha mfungo na ndiyo tunda pengine kuliko tunda lingine.

Pamoja na kutumika sana katika kipindi hiko pia lina ladha nzuri mdomoni, huku likisheheni madini na vitamini lukuki na hivyo kuwa na faida nyingi kiafya.

Ulaji wa tendo humsaidia sana mhusika kupata kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili.

Pia ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo kumsaidia mhusika kuondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia.

Tende pia husaidia kuupatia nguvu mwili na kukuondoa uchovu, hii ni kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’. 

Hali kadhalika tende ina madini aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini hayo husaidia kuimarisha mishipa ya fahamu.

Pamoja na hayo tende pia huwasaidia wale wenye matatizo ya ugonjwa wa anemia, (kupungukiwa damu) wanapotumia tende huweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi.

Tende vile vile huimarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).

Nachoweza kusema ni kwamba kuna faida nyingi za tende na unaweza kuila tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizi 10 na nyingine.

KWA WALE WANAOPENDA KUNYWA MAJI BARIDI, BOFYA HAPA

Wengi wetu tunapenda sana kunywa maji ya baridi hasa katika joto kali na maji haya ya baridi kwa wakazi wa jiji kama la Dar es Salaam ndio huona yanawafaa zaidi kutokana na joto linalopatikana kwenye jiji hilo.

Ni ukweli usiopingika kuwa unywaji maji ya baridi huleta faraja zaidi kwa mhusika, hivyo si jambo la kushangaza mtu kuhitaji maji ya namna hiyo kila mara baada ya mlo.

Licha ya kwamba maji ya baridi ni mazuri zaidi, lakini nayo yana madhara yake kiafya, moja ya madhara ya maji ya baridi ni pamoja na kudhorotoshe mfumo wa umeng'enyaji chakula tumboni.

Kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya lishe wanasema kwamba mtu anapokunywa maji ya baridi mara baada ya kula chakula, maji hayo huchangia kuganda kwa mafuta yaliyomo kwenye chakula.

Kutokana na kitendo hicho basi hupelekea  usagaji wa chakula kwenda pole pole sana na hivyo huweza kumuingiza mhusika kwenye matatizo ya ukosefu wa choo 'constipation'.

Hata hivyo, imeonekana kisayansi kuwa kunywa maji ya baridi baada ya chakula ni hatari pia kwa afya ya moyo tumbo na mwili mzima kwa ujumla. Hivyo kama wewe ni mzoefu wa kutumia maji ya baridi ni vyema ukaanza kuepukana nayo taratibu kumbuka kwamba afya ya mwili wako hujengwa na unachokula na kunywa leo.

MENDE WATUMIKA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO

Kwa hali ya kawaida mende huchukiwa sana na watu na huhusishwa na uchafu na maradhi. Lakini hivi unaweza kuamini kwamba wadudu hawa wana manufaa makubwa sana kwa binadamu?

Najua itakuwa ni ngumu kuamini, kwani wengi tumezoea kusikia mimea mbalimbali na matunda ikitumika kutibu magonjwa mbalimbali ikiwa pamoja na matatizo ya vidonda vya tumbo, lakini ni vyema taarifa ikakufikia kwamba mende wanatumiwa pia katika matibabu.

Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika. Wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupigana na sumu.

Wanaweza kusaidia katika kutengeneza dawa za kusaidia binadamu kukabiliana na bakteria zinazohangaisha sana watu kwa mfano E. Coli na MRSA ambazo zimekuwa hazisikii dawa.

Hii si mara ya kwanza mende kutumiwa kwa matibabu. Mwanahabari Lafcadio Hearn karne ya 19 alipitia maeneo ya kusini mwa Marekani na kuripoti jinsi watu wenye pepopunda walivyokuwa wakipewa chai iliyotengenezwa kwa kutumia mende.

“Sijui ni mende wangapi hutumiwa hadi upate kikombe cha chai, lakini wakazi wa New Orleans wana imani sana na tiba hii,” aliandika.

Leo katika hospitali Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosagwa hutumiwa kutibu vidonda vya moto na pia huwezwa kutibu vidonda vya tumbo.

Mende pia hupikwa na kuliwa nchini Uchina
Kufuatia hali hiyo mende wanahitajika sana hivi kwamba Wang Fuming aliamua kufungua biashara ya ufugaji mende eneo la Shandong, mashariki mwa Uchina. Huwa anafuga mende 22 milioni kwa wakati mmoja. Anasema tangu 2010, bei ya mende waliokaushwa imepanda mara kumi.

Imeelezwa kuwa  kuna aina 4,500 ya mende, na ni aina nne pekee ambao huwa waharibifu, huku wengi wao wakiishi karibu na nyumba za watu na hutekeleza jukumu muhimu katika ikolojia kwa kula vitu vilivyokufa na vinavyooza.

KAKA NA DADA UGONJWA WA SUNZUA NI HATARI SANA

Sunzua kitaalamu warts ni ugonjwa wa ngozi unaofahamika na wengi. Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo kitaalamu huitwa human papilloma virusi.

Virusi vinavyosababisha ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya ngono.

Ugonjwa huu hutokea sehemu mbalimbali za mwili, lakini huwatokea wengi sehemu za siri.
Sunzua kama ugonjwa wa zinaa, huathiri sehemu za siri pamoja na njia ya haja kubwa.

Wagonjwa ambao wanaishi na Virusi vya Ukimwi wako kwenye mazingira hatarishi zaidi ya kupata sunzua.
 
Virusi vinavyosababisha maradhi ya sunzua huambukizwa kwa njia ya ngono na ni mara chache huweza kusambaa kwa njia ya kugusana.

Maradhi haya husababisha ngozi kutokuwa na muonekano wake wa kawaida kuwa na milima na mabonde kiasi cha kusababisha kukatika kwa urahisi na kufanya virusi kuendelea kupenya.

Aina hii ya ugonjwa kwa wanawake huathiri sehemu za nje za maumbile ya siri na mara nyingine huweza kujitokeza na kuathiri shingo ya kizazi.

Kwa wanaume sunzua huathiri uume wenyewe, korodani, nyonga mpaka kwenye mapaja.

Kimsingi sunzua huwa haziumi na sanasana huwa zinawasha na huweza kujitokeza katika kipindi cha miezi miwili mpaka tisa baada ya maambukizi ya virusi.

Kwa wanawake, sunzua ya kwenye shingo ya kizazi huweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi.Kwa sababu hiyo, mwanamke anapaswa kujichunguza ili kuchukua hatua mwafaka za matibabu mapema zaidi.

SIKU NZURI ZA KUSHIKA MIMBA

Habari za leo wasomaji wangu?  Kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mungu kwani ameniwezesha kufika siku hii kwa amani.

Mada leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.

Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba na kutupa watoto na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa.

Mimba nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga asipate.

Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu ambayo: Mzunguko mfupi wa siku 25 kurudi nyuma, mzunguko wa kawaida wa siku 28 na mzunguko mrefu wa siku30-35.
Wanawake wengi mzunguko wao huwa ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo nitawaongelea zaidi.

Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi ya mwezi unaofuata.

Kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 Oktoba basi hiyo ndiyo siku yako ya kwanza.

Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.

Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?

Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa 24 hadi 48 baada ya kujamiiana hivyo kama mwanamke atafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo zitarutubishwa

JE UNATOKWA NA MICHIRIZI KWENYE NGOZI?

Tatizo la kutokwa na michirizi kwenye ngozi ni moja ya mambo ambayo yameonekana kuwakumba wanawake wengi na kwa kiasi kikubwa wengi wao huonekana kukwazika na hali hiyo.

Ukikutana na mtu mwenye tatizo hilo unaweza kujua huenda alibata jeraha na akabakiwa na mabaka au kovu, lakini siyo kovu na wala mtu hakupata ajari au kuumizwa na kitu chochote.

Kwa kawaida au mara nyingi alama hizi za michirizi humtokea mtu maeneo ambayo huwa na nyama nyingi au mafuta ya kutosha, Mfano kwenye mapaja, upande wa juu wa mikono, tumboni, kwenye makalio, lakini pia baadhi ya watu hutokea maeneo ya kifuani au kwenye matiti kwa wanawake.

Hata hivyo kwa kawaida michirizi hiyo huwa haileti maumivu ya aina yoyote, isipokuwa hubadili muonekano wa ngozi ya muhusika tu, kwani baadhi ya watu michirizi hiyo huweza kuwa ni mikubwa sana na kumkosesha amani mhusika.

Tatizo hili huchangiwa na kuongezeka kwa uzito kwa ghafla au wengine huweza kukumbwa na tatizo hili kutokana na aina ya ufanyaji wa mazoezi fulani fulani.
Viazi mviringo ndio ni suluhisho
Moja ya tiba asili ya tatizo hili ni pamoja na matumizi ya viazi mviringo.

kinachofanyika ni kupata vipande vidogo vidogo vya viazi hivyo kisha mhusika atasugua sehemu yenye tatizo na ataacha kwa muda usio pungua saa moja kisha ataosha kwa kutumia maji ya uvuguvugu, njia hii ukitumia kwa muda mrefu kutwa mara mbili kila siku husaidia sana kuondosha michirizi hiyo.

Pamoja na hayo ni vyema kuzingatia kunywa maji ya kutosha kila siku kwani maji hayo husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini kupitia ngozi na hivyo hukuwezesha kuwa na ngozi yenye afya nzuri zaidi

IJUE MIMEA TIBA NA AFYA KWA UJUMLA

Habari za leo mpenzi msomaji wa tovuti yetu karibu katika muendelezo wetu wa kupeana taarifa mbalimbali kuhusu mimea tiba na afya kwa ujumla.

Ikiwa leo ni Jumatatu ya Oktoba 19, 2015 napenda tuzungumzie mapesheni, tunda hili mara nyingi wengi hupendelea zaidi kulitumia kwa kutengenezea juisi ili kuleta ladha nzuri zaidi na amahakika limekuwa likichangia kuleta ladha nzuri kwenye juisi.

Mmea wa mpesheni kwa kawaida hukuwa kwa kutambaa, hivyo katika ukuaji wake ni muhimu kuweka miti ili uweze kusaidia kukua vizuri.

Mapesheni yanasifika kwa kuwa na virutubisho bora kwa afya ya binadamu ikiwemo vitamin A, C, B2, B6, na E, flavonoids, pectin pamoja na madini ya chuma. 

Aidha, mapesheni yanauwezo mzuri katika kupunguza maumivu ya mishipa ya fahamu na maumivu ya tumbo la hedhi, huku ikisaidia sana kutibu matatizo ya wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo na hali ya kuzubaa kwa wazee na watoto.

Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa, wajawazito na watoto wachanga wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotumia tunda hili, hii ni kutokana na katika majaribio ya utafiti huo walibaini matunda hayo yanauwezo wa kusababisha uchungu na kusababisha watoto kuzaliwa kabla ya wakati, lakini pia huweza kusababisha usingizi hivyo si vizuri kutumiwa na madereva.

IFAHAMU DAWA YA KIMONDO NA DK.MANDAI

Maambukizi katika njia ya mkojo au kama unavyojulikana kwa wengi UTI ni miongoni mwa tatizo ambalo huathiri mfumo wa mkojo ikiwa ni pamoja na ureter ambayo ni kama bomba linalosafirisha mkojo kutoka kwenye figo.

Ugonjwa huu unaathiri zaidi kibofu cha mkojo na urethra lakini unaweza pia kuathiri figo, ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli (E. coli)

Kimsingi unapofika Mandai Herbalist Clinic unaweza kupata dawa nzuri iitwayo Kimondo, hii ni miongoni kati ya dawa ambazo uwezo wake ni mkubwa wa kumaliza shida ya U.T.I hata kama ni ile sugi haijalishi imekusumbua kwa muda gani, lakini unapotumia hii dawa tu basi lazima uagane na tatizo la U.T.I

Dawa hii ya kimondo imechanganywa vizuri kitaalam kwa mimea mbalimbali ambayo nayo inauwezo wa kumaliza uvimbe ndani ya mfuko wa uzazi yaani 'fibroid'

Halikadhalika dawa hii husaidia sana kuongeza kinga za mwili, kusafisha tumbo na kutibu minyoo pia.

Inawezekana unahitaji kuipata dawa hii basi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

JE ULIKUWA UNAFAHAMU KITU KAMA HIKI?? BOFYA HAPA

Hiki ni kidonge cha Panadol, kabla ya kutumia kidonge kama hiki au kidonge cha namna yeyote ile ni vyema ukikate katikati ili kuangalia ndani ya kidonge hicho unachotaka kukitumia kina usalama kiasi gani!

Ndugu yangu, kumbuka afya yako ni muhimu kuliko vitu vyote unavyovifahamu katika ulimwengu huu. Endelea kuwanasi tukujuze zaidi. 
Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top