Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Kwa hali ya kawaida mende huchukiwa sana na watu na huhusishwa na uchafu na maradhi. Lakini hivi unaweza kuamini kwamba wadudu hawa wana manufaa makubwa sana kwa binadamu?
Najua itakuwa ni ngumu kuamini, kwani wengi tumezoea kusikia mimea mbalimbali na matunda ikitumika kutibu magonjwa mbalimbali ikiwa pamoja na matatizo ya vidonda vya tumbo, lakini ni vyema taarifa ikakufikia kwamba mende wanatumiwa pia katika matibabu.
Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika. Wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupigana na sumu.
Wanaweza kusaidia katika kutengeneza dawa za kusaidia binadamu kukabiliana na bakteria zinazohangaisha sana watu kwa mfano E. Coli na MRSA ambazo zimekuwa hazisikii dawa.
Hii si mara ya kwanza mende kutumiwa kwa matibabu. Mwanahabari Lafcadio Hearn karne ya 19 alipitia maeneo ya kusini mwa Marekani na kuripoti jinsi watu wenye pepopunda walivyokuwa wakipewa chai iliyotengenezwa kwa kutumia mende.
“Sijui ni mende wangapi hutumiwa hadi upate kikombe cha chai, lakini wakazi wa New Orleans wana imani sana na tiba hii,” aliandika.
Leo katika hospitali Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosagwa hutumiwa kutibu vidonda vya moto na pia huwezwa kutibu vidonda vya tumbo.
Mende pia hupikwa na kuliwa nchini Uchina
Kufuatia hali hiyo mende wanahitajika sana hivi kwamba Wang Fuming aliamua kufungua biashara ya ufugaji mende eneo la Shandong, mashariki mwa Uchina. Huwa anafuga mende 22 milioni kwa wakati mmoja. Anasema tangu 2010, bei ya mende waliokaushwa imepanda mara kumi.
Imeelezwa kuwa kuna aina 4,500 ya mende, na ni aina nne pekee ambao huwa waharibifu, huku wengi wao wakiishi karibu na nyumba za watu na hutekeleza jukumu muhimu katika ikolojia kwa kula vitu vilivyokufa na vinavyooza.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.
Share habari hii kadri uwezavyo.
Filed Under:
AFYA
on Tuesday, November 10, 2015