Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Mvua kubwa ambayo imeambatana na upepo mkali, yasababisha maafa makubwa mkoani Mara

Mvua kubwa ambayo imeambatana na upepo mkali, imesababisha maafa makubwa katika vijiji vitatu vya wilaya ya Butiama mkoani Mara na kusababisha nyumba za kaya zaidi ya mia moja zikiwemo nyumba za ibada kubomolewa vibaya na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali, huku idadi kubwa ya ekari za mashamba yenye mazao mbalimbali pia yakiathiriwa na mawe yaliambatana na mvua hiyo.

Akizungumza baada ya kukagua athari ambayo imesababishwa na mvua hiyo, mwenyekiti wa kamati ya maafa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi, akiwa ameambatana na mwenyekiti wa halmashauri ya Butiama Bw Magina Magesa, wamesema mvua hiyo imesababisha madhara makubwa na kwamba watendaji wa serikali wameanza kufanya tathimini ya kina ili kujua ukubwa wa maafa hayo

Naye diwani wa kata ya Butuguri Bw. Paul Warati, akizungumzia maafa hayo, amesema tathimini ya awali inaonyesha kuwa zaidi ya kaya mia moja,majengo ya taasisi, chakula na mazao mashambani zimeathirika na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali.

Ajali iliyotokea eneo la Msikitini yasababisha foleni kubwa kwa wakazi wa Mbagala

Kitendo cha kutokea ajali maeneo ya Maikitini eneo ambalo liko katikati ya Mrongani na Mission wilaya ya Temeke kumesababisha foleni kubwa sana kwa watumiaji wa barabara ya Kirwa Road.

Ambapo folen ya kutoka mjini kwa walio fangulia imeanzia Bandari na kuishia eneo la Mission. Magari yanayotoka mjini kuelekea Mbagala rangi tatu yakifika Mtongani yanatumia barabara ya magari yanayotoma mbagala kuelekea mjini na kwingineko.
Na kwa wale wanaotoka Mbagara kuelekea maeneo ya mjini, kama Tandika, Buguruni, Ubungo nk, foreni yao imeanzia Zakhem hadi Mission. 

KILA MTU ANAENDESHA CHOMBO CHAKE JINSI ANAVYOJUA YEYE MWENYEWE, EBU TAZAMA HII


Ajali hii ilitomea kituoni kabisaa, eneo la Kizuiani Mbagala.
Gari namba T 602 DGT ndilo lililo sababisha ajali maeneo hayo.
Gari tajwa ndio iyo hapo inayoonekana kwa upande wa kushoto. Na mwenye bajaji alikuwa akidai bajaji yake haikuwa na break nzuri.
Na gari namba T 436 DFM iyo daladala unayoiona hapo upande ww kulia ilikuwa imepaki kituoni bila shida yoyote.
Baada ya gari tajwa hapo picha ya juu yake hii ilikuja bajaji yenye namba MC 495 AEQ nayo ikawa inaingia kituoni kabla haijasimama ndipo olipoingia ole daladala tajwa hapo mwanzoni kabisa mwa habari hii kisha kusababisha ajali hii.
Mabishano galichukua mda mwingi kama dakika 10 hivi, na mwenye bajaji akiwa ni mtu mwenye uremavu wa miguu alikuwa na wenzake wawili nakufanya idadi ya watu kwenye bajaji ole kuwa na jumla ya watu watatu.
Mwenye iyo daladala unayoiona hapo kushoto kwako alikuwa akidai yeye amegongwa na mwenye bajaji wakati yeye ndiye aligeingia vibaya kituoni na kumgonga mwenye bajabi kisha mwenye bajaji kujibamiza kwa ole daladala ya kulia.

Tazama picha tano za tukio la kuungua kwa ghala la Saba Spare Parts Mwenge

Kutoka hapa nilipo naona moshi mkali. Kwa mujibu wa watu waliopo eneo la tukio, wanasema moto unawaka jirani na chuo cha Tumaini kampasi ya Mwenge.


Kinachoungua ni ghala linalomilikiwa na Saba Spare Parts linateketea kwa moto muda huu. Zimamoto wamefika na wanaendelea na uokoaji.


Tazama picha zote za tukio hili la kuwaka kwa moto kwenye eneo hili.

Endelea kutazama pocha zote za tukio hili

Mtoto Happiness Josephat (6) aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza betri moyoni (JKCI), amefariki dunia.

Mtoto Happiness Josephat (6) aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza betri moyoni katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), amefariki dunia.

Mama mzazi wa Happiness, Elitruda Malley amesema Happiness alifariki dunia ghafla juzi mchana. 

Alisema   Jumapili, mtoto huyo alikuwa mzima na walikwenda kanisani kutoa sadaka ya shukrani kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa mambo aliyowatendea na wakarudi nyumbani salama. 

“Jana tumeamka vizuri lakini ghafla hali yake ilibadilika akaanza kulalamika kuwa anajisikia vibaya, tukamkimbizia Hospitali ya Selian hapa Arusha lakini tukiwa njiani alifariki dunia,” alisema. 

Elitruda alisema kifo cha mwanawe kimemhuzunisha mno na  daima atamkumbuka. 

“Alikuwa tayari amesharudi shuleni, alikuwa akiniambia kuwa atasoma kwa bidii ili ndoto yake ya kuwa daktari bingwa itimie aweze kusaidia watu wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali,” alisema. 

Hata hivyo, alisema maziko ya Happiness yanatarajiwa kufanyika leo huko Mbulu mkoani Manyara. 

Mkurugenzi wa JKCI, ambako Happiness alifanyiwa upasuaji, Profesa Mohamed Janabi amesema taarifa hiyo imemshtua ikizingatiwa mtoto huyo alikuwa anaendelea vizuri. 

“Sikuwa na taarifa, nitawasiliana na mama yake   tujue hasa shida gani ilitokea, maana zipo sababu nyingi labda alipita jirani na mitambo ya umeme au simu, hizo ni sehemu hatarishi kwa mtu aliyewekewa betri kwenye moyo,” alisema. 

Happiness alifanyiwa upasuaji huo wa historia nchini Julai 15, mwaka huu katika Taasisi ya JKCI wa kuwekewa betri maalumu kwenye moyo ambayo kitaalamu inaitwa ‘pacemaker’. 

Kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimtibia mtoto huyo, wakati alipopekekwa hospitalini hapo, mapigo yake ya moyo yalikuwa 20. 

Walisema  hali hiyo kwa mtoto si ya kawaida kwa vile  anapaswa kuwa na wastani wa mapigo 60 hadi 100 kwa umri wake. 

Mtoto Happiness alizaliwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi hali hiyo huwakumba watu wazima. 

Moja ya ndoto za mtoto huyo ambayo alinukuliwa akiisema ni kuwa daktari bingwa wa kutibu magonjwa mbalimbali.

Jela Mwaka Mmoja kwa Kumdhalilisha Mama Yake Mzazi, bofya hapa kujua zaidi

Mwanaume mkazi wa Ilala, Siwema Seif (40) amehukumiwa na Mahakama ya Mwanzo ya Ilala kwenda jela mwaka mmoja kwa kumtolea lugha ya matusi na kumdhalilisha kimwili, Zainab Ramadhan ambaye ni mama yake mzazi.

Akisoma hukumu mahakamani hapo jana, Hakimu wa Mahakama hiyo, Matrona Luanda alisema ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji, ulionesha kukosa shaka na kumtia hatiani mshitakiwa.

Shahidi huyo alisema siku ya tukio mshitakiwa alifika nyumbani kwao akaomba chakula akajibiwa kuwa kuna wali na mshitakiwa akasema hataki wali bali anataka ugali na mama akamjibu asingeweza kupika ugali na kumsisitiza Siwema ale wali.

Zainab alisema baada ya majibizano hayo, mshitakiwa alimtukana matusi ya nguoni mama yake, huku akisema hawezi kumzaa na kumkashifu kwamba hana sehemu ya kumzalia huku akitishia kumwua akiahidi kumtoa roho ndipo amjue yeye ni nani.

Kwa mujibu wa Zainab, alipoona ugomvi na matusi umezidi aliingia chumbani mwake, na ndipo mlalamikaji akamfuata na kumtukana huku akitishia kumwingilia kinyume cha maumbile.


“Baada ya hapo mshitakiwa alinivamia na kunidhalilisha kimaumbile kwa mikono yake,”alisema.

Baada ya ushahidi wa mama huyo dhidi ya Siwema, Mahakama ilitoa nafasi kwa kijana huyo kujitetea na Mahakama ikamtia hatiani.

Mwendesha mashitaka Blanka Shao alisema kwa kuwa japo mshitakiwa alikuwa mkosaji wa mara ya kwanza, kitendo alichokifanya ni cha kifedhuli tena haonyeshi kujutia, alishauri apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake.

Hakimu Luanda alimhukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa kitendo alichomfanya mama yake mzazi.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 9 Ilala, mtaa wa Sophia Kawawa, nyumba namba 10.

Vijana 14 wakabaji wenye umri chini ya miaka 16 wakamatwa Temeke

Vijana 14 wenye umri chini ya miaka 16 wenye kikundi chenye jina maarufu kama "Taifa jipya" wakamatwa.

 Wamekamatwa eneo la sabasaba katika wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kukaba na kuwapora wapitanjia kwa kutumia mapanga hali iliyowapelekea wananchi wenye asila kali kuwapiga na mmoja wao kufariki dunia.

Vijana hao wengi wao ni wakazi wa Buza na wengi wao ni wanafunzi ambapo walienda kufanya uporaji wao katika uwanja wa Zakii.

Mbali ya jeshi la polisi kuweza kufanikiwa kuwakamata vijana hao pia polisi wameweza kuwapata wazazi wa watoto hao na wanatarajiwa kupelekwa mahakamani na endapo wazazi wa watoto hao watatiwa hatiani kwa mujibu wa sheria ya watoto ya mwaka 2009 kifungu cha 6 hadi 9 watapewa adhabu ya kifungo cha miezi 6 jera au kutozwa faini ya Tsh millions 5.

Watu 10 wamefariki dunia na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Barcelona kupata ajali, picha zote ziko hapa

Watu 10 wamefariki dunia na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Barcelona walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Lindi  kupata ajali eneo na Miteja mkoani Lindi.


Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga imesema kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na tairi ya gari ya upande wa kushoto kupasuka na kutokana na mwendo wa kasi wa basi hilo, dereva alipoteza uelekeo ndipo likapinduka.


Pia Kamanda Mzinga amesema kuwa wamechunguza na kugundua kua licha ya kuwa basi hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 48, wakati basi hilo linapata ajali kulikuwa na abiria 54 kitu ambacho ni kosa kisheria.


Aidha, Kamanda Mzinga amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kuweza kubaini alipo dereva ili kuweza kufahamu ni kipi hasa kilichotokea. Hadi sasa wanamshikilia kondakta wa basi hilo lakini bado hajaweza kuelezea tukio halisi.

Polisi wanaolinda migodi ya Acacia Mining wanadaiwa kuua watu zaidi ya 65 na kujeruhi wengine 270

Dar es Salaam. Polisi wanaolinda migodi ya Acacia Mining wanadaiwa kuua watu zaidi ya 65 na kujeruhi wengine 270 wanaoingia mgodi wa North Mara kutafuta magwangala, ripoti ya matokeo ya uchunguzi wa mgogoro wa mgodi huo na wananchi inaeleza.

Magwangala ni vipande vya mawe vinavyobaki baada ya mgodi huo kuondoa madini ya dhahabu. Kwa kawaida magwangala husalia na sehemu ndogo ya dhahabu, ambayo wananchi huyataka kwa ajili ya kujipatia riziki.

Ripoti za vifo hivyo imetolewa na kamati iliyoundwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Februari mwaka huu kwa ajili ya kutafuta mwafaka baina ya viongozi wa mgodi wa Acacia North Mara na wananchi.


Kamati hiyo ilimjumuisha Kamishna wa Madini, John Mayopa, ambaye alikuwa mwenyekiti, John Heche (mbunge wa Tarime), na wenyeviti wa vitongoji na Serikali za Mitaa wa eneo hilo.

Alipoulizwa kuhusu ripoti ya kamati hiyo, katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa alisema tayari imeshakamilisha ripoti yake, lakini bado ipo kwa wanasheria kwa ajili ya kuhakikiwa.

“Ripoti ipo tayari lakini haijawa ‘released’ (haijatolewa) mpaka wanasheria waipitie, baada ya wiki tatu nadhani itakuwa tayari,” alisema.

Lakini gazeti la Globe and Mail la Afrika Kusini lilichapisha ripoti ya kamati hiyo ikisema idadi ya vifo hivyo imepatikana baada ya wanakijiji kuulizwa maswali kuhusu uhusiano wao na polisi wanaolinda mgodi huo unaoendeshwa na kampuni hiyo inayomilikiwa na Barrick Gold ya Canada.

Tetemeko kubwa la Ardhi laikumba mikoa ya Mwanza na Kagera, zaidi bofya hapa

Tetemeko kubwa la Ardhi laikumba mikoa ya Mwanza na Kagera, habari kamili iko hapa nchini.

Kumetokea tetemeko la Ardhi na limepiga maeneo ya mkoa wa Kagera na inadaiwa mikoa jirani nayo imepata mtikisiko huo.

Linadaiwa kurudia tena likiwa na mtikisiko mkubwa zaidi uku Nyumba kadhaa zikiwa zimebomoka kutokana na ukubwa wa tetemeko hilo pia Taarifa za vifo zimesikika.

Tetemeko hilo limeanza kusikika mida ya saa tisa na nusu, huku likidaiwa kuwa na ukubwa/uzito wa 5.7 na lilikuwa likitokea upande wa kaskazin magharibi.

Mpaka sasa imeripotiwa kuwa takribani watu 10 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa, kaa nadi tukujuze zaidi kupitia hapa hapa.

KWA TAARIFA YAKO, HUYU NDIYE MNYAMA MWENYE WIVU ZAIDI KULIKO WANYAMA WOTE DUNIANI

Mnyama huyu anaitwa 'NYEGERE' Chakula chake kikubwa ni asali, hupanda juu ya mzinga wa asali na KUUJAMBIA, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kuyala. Ana ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea.

Ni moja ya Wanyama wenye WIVU sana Duniani na Mapenzi makubwa kwa Jike lake, mara zote hutembea nyuma ya Jike huku akiwa ameziziba sehemu za siri za jike, na hata jani tu likiigusa sehemu hiyo basi litararuliwa na kupewa kipigo cha Nguvu kwani anaamini JANI litakuwa "limefaidi utamu" wa jike.

Aidha, kuna makabila ambayo WAGANGA wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa ngozi au Nyama yake kutengenezea LIMBWATA, Hivyo  Wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na "upendo" wa Nyegere.

Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana Binadamu Wanaume, Mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano kwa wivu kuwa utamtamani jike lake na atakimbilia kuvamia sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.

Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, kama aliujambia Mzinga wa asali na akachukua kidogo kupeleka kwa Mkewe, alafu ikatokea Mlina asali akifika na kupakua, basi Nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika atavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake.. Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.

Ni moja ya Viumbe wanaaogopwa zaidi Ulimwenguni kwani huweza kupambana na Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda, Hula nyoka wa aina yoyote na Sumu yake ni kali ambapo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi. MaktabaYaMkutubi”

MWIZI WA SIMU KARIAKOO STEND YA DALADALA ZA MBAGALA UYU HAPA

      Akipelekwa kituo cha polisi Kamata

Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza mda wa saa 6:07 jioni, ambapo kumetokea mwizi akitaka kuiba simu ya abilia aliyekuwa anataka kupanda daladala inayoenda mbagala rangi tatu.

Abilia wakiwa kwenye vuta nikuvute za kugombania kupanda gari hilo kumbe miongoni mwa hao wanaogombania alikuwepo mwizi akijaribu kuiba simu ya abilia ambaye alikuwa ni mwanamke.

Mda mfupi sana kabla mwizi huyo kufanikisha zoezi lake ndipo baadhi ya abilia walimshtukia na kuanza kumpa kichapo.

Abilia baada ya kumpa kichapo walimkagua wakamkuta mfukoni ana pochi alafu ndani yake kuna makaratasi tu wala hakuna kitambulisho chochote cha kuweza kumtambulisha, ndipo abilia waliamua kumbeba na kumpeleka kwenye kituo cha polisi hapa Kamata.

ARUSHA: YULE MAMA ALIYEPISHANA KIMAONGEZI NA MUMEWE AJINYONGA, BOFYA HAPA

Mama anayedaiwa kuchoma maduka matatu, nyumba yake ya kuishi, ajinyonga Arusha

August 21 2016 ziliripotiwa habari za mama mmoja anayejulikana kwa jina la Victoria Edward Wenga kuchoma moto maduka matatu na nyumba yake ya kuishi katika kata ya Lemara Arusha. Chanzo cha mama huyo kuchoma moto ilidaiwa ni ugomvi uliokuwepo kwenye familia kati ya mama huyo na mume wake anayejulikana kwa jina la Edward Wenga.

Habari nilizozipokea muda si mrefu zinasema kwamba mama huyo amejinyonga kwa kutumia nguo yake na kufariki dunia.

Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amesema alijinyonga akiwa kituo cha polisi kama mahabusu ambapo polisi walipata taarifa baada ya mahabausu wenzake kupiga kelele.

HABARI KAMILI JUU YA ASKALI POLISI WALIOFARIKI DUNIA UKO MBANDE HII HAPA

Sijui kama hii habari umeisha ipata lakini limetokea tukio baya huko Mbagala jijini Dar. Inasemekana askari walikuwa wanaelekea lindo benki ya CRDB MMBANDE. Waliofanya shambulizi wanadaiwa kuondoka na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.

======== UPDATE: ========

Waliofariki ni askali mwenye namba
1. E5761 CPL YAHAYA
2. F4660 CPL HATIBU NA
3. G9544 PC TTITO.

Inasemekana ni katika tukio la UVAMIZI WA BANK CRDB MBANDE mnamo saa 19:30HRS usiku na uku ikisemekana SMG moja wameondoka nayo majambazi hao.

Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa ni dereva. Majambazi hayakuingia ndani ya bank, uku Gari la Polisi aina ya (Leyland Ashok) likiharibiwa kwa risasi.

Habari kutoka katika ukurasa rasmi wa Instagram wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba amethibitisha kupoteza maisha kwa Askari Polisi Wanne na Raia wawili.

Mmoja wa majeruhi ni mfanyabiashara wa upande wa pili wa tawi la benki yalikotokea mauaji. Waziri awatembelea majeruhi na kusema wanaendelea vizuri.

Na Taarifa ya Kamanda Sirro kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi inasema hivi

Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa jumla ya askari wake wanne wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya majambazi kuvamia tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande, wilayani Temeke, Dar es Salaam.

Akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha Redio One Stereo leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema watu kadhaa wamekatawa na msako unaendelea ili kuwapata waliotekeleza unyama huo.

Sirro amesema taarifa kutoka eneo la tukio zinaonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na baada ya kufanya mauaji hao, walivamia kituo cha polisi cha Mbande kisha wakavunja stoo na kuchukua sare ya askari na silaha.

Akielezea namna tukio hilo lilivyotokea, Kamanda Sirro amesema wahalifu hao walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana lindo katika taasisi hiyo ya fedha na kuibuka ghafla na kuanza kurusha risasi.

Kwa mujibu wa Sirro, gari la polisi limechakazwa kwa risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia na ndiye aliyeweza kutoa taarifa na maelezo ya namna tukio lilivyofanyika.

“Watu kadhaa wamekamatwa na tunaendelea na msako. Tunawataka wakiwa hai au wafu,” amesema Kamanda Sirro huku akiwataka watu kujihadhari na yeyote anayejitambulisha kwao kuwa ni askari bila kuonesha kitambulisho.

Ameendelea kusema kuwa baada ya operesheni ya kukomesha mtandao wa wahalifu kama hao na wengine kukimbilia nchi jirani, masalia wameanza kujikusanya na kutekeleza matukio ya mauaji huku askari wakilengwa.

NDEGE YA YAANGUKA NA KUUWA WATU ZAIDI YA 6, ZAIDI BOFYA HAPA

Takribani watu 6 wamefariki katika ajali ya ndege ndogo illiyoangukia kwenye miti na kuwaka moto ilipokuwa ikitua uwanja wa Shannon.

Ajali hiyo imetokea jimbo la Virginia na mpaka sasa chanzo chake hakijajulikana.

MWANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA UDOM AUWA KIKATILI, ZAIDI BOFYA HAPA

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Fredrick Joseph (25), ameuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akitoka baa.

Tukio hilo limetokea jana usiku eneo la Chuo hicho ambapo mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi wakafika na kumkuta akigalagala njiani.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lazaro Mambosasa, amesema mwanafunzi huyo ambaye ametokea Musoma mkoani Mara ameshambuliwa kwa kupigwa na watu wasiofahamika.

TREN YAGONGANA NA GARI LA UDA GEREZANI KARIAKOO, ZAIDI BOFYA HAPA

Ajali mbaya sana imetokea mda huu kariakoo gerezani watu sita wamepoteza maisha apo apo

akiwemo konda wa kampuni ya Uda dereva kakimbia Mungu awalaze mahali pema wote waliopoteza maisha.

UNAYA FAHAMU MAAJABU YA ZIWA LA MBEYA?? BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Ziwa hili liko Mbeya kwenye milima ya Uporoto. Na wenyeji wanasema eti ziwa ili ubadilika rangi kila siku kulingana na hali ya hewa ya siku iyo, pua wana endelea kwa kusema kuwa ziwa ilo linatajwa kuwa ni ziwa la pili kwa ukubwa katika maziwa yanayopatikana kwenye kreta Afrika.

Wenyeji wanalihusisha ziwa hili na imani za kishirikina. Wanadai lilipigwa mawe na likahamishwa kutoka Masoko Tukuyu na kwenda kujikita Uporoto.

Hilo ziwa nshawahi kulisikia, eti wazungu walienda kufanya uchunguzi wakazama. Wakaenda kundi jingine wakajifunga minyororo ya chuma kwenye miti kisha wakaingia ziwani, minyororo ikakatika, wakazama.

ziwa hilo lina ingiza tuu maji na hali toi maji kwa sababu liko katikati ya milima alafu halina ufukwe kwani ukiwa ukingini kabisa uka jalibu kupima kuna ni parefu na haijulikani ni mita ngapi kwenda chini kwa hivyo huwezi kuogelea kwenye ziwa hilo lililoko maeneo ya upoloto ukiwa una toka Mbeya una shuka kituo kina itwa nymbe one alafu una tembea kilomita 12 ili kufika ziwani hapo.

ANASHIKILIWA NA POLISI KISA KUMCHINJA MKE WAKE WA NDOA, HABARI KAMILI IKO HAPA

Mwanaume anayejulikana kwa jina la Remy Joseph (35) anashikiliwa na polisi kwa kumchinja mke wake wa ndoa kabisa aitwaye Josephine Ndengaleo Mushi waliyeishi naye miaka 10 na kuzaa watoto wawili.

Tukio hilo la kutisha lilijiri ndani ya chumba kimoja kilichopo ghorofa ya pili ya  Hotel Friend’s Corner Ltd iliyopo Manzese Argentina, Dar ambapo walikuwa wamechukua chumba katika hoteli hiyo kwaajili ya kulala hapo.

Polisi walifanya uchunguzi chumbani na kugundua kuwa, marehemu Josephine alichinjwa shingoni, akakatwa mbavu mbili, moyo na maini vilikuwa nje ‘vikimwagika’, mwisho alichomwa kisu utosini.

Cha kusikitisha zaidi, mwili wa marehemu Josephine ulipigishwa magoti, sehemu ya miguu mpaka magoti ikiwa sakafuni na kifuani kulalia kitanda. Halafu ulifunikwa shuka

Katika hali iliyoonesha kuwa, mtuhumiwa baada ya kutenda ukatili huo alitaka kujinyonga, polisi walikuta waya wa umeme wa tivii ukining’inia kwenye pangaboi lakini ukiwa umekatika. Na pia damu na alama za kujikata visu shingoni.

Sababu ya kufanya hivyo haijujulikana ila ndugu wa mke wa marehemu walielezea kuwa mme alikuwa akimhisi vibaya mkewe.

R.I.P Josephine Mushi. Dah! hii inatisha sana? Una lipi la kusema juu ya hili?

WATU 75 WAUAWA NA WENGINE 100 KUJERUHIWA VIBAYA, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

BAGHDAD, IRAQ: Watu 75 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa jana jioni baada ya wanamgambo wa ISIS kufanya shambulizi sokoni.

Shambulio hilo limetokea wakati ikiwa imepita wiki moja tangu jeshi la Iraq liukamate mji wa Falluja kutoka kwa wanamgambo wa ISIS.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top