Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Polisi wanaolinda migodi ya Acacia Mining wanadaiwa kuua watu zaidi ya 65 na kujeruhi wengine 270

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Dar es Salaam. Polisi wanaolinda migodi ya Acacia Mining wanadaiwa kuua watu zaidi ya 65 na kujeruhi wengine 270 wanaoingia mgodi wa North Mara kutafuta magwangala, ripoti ya matokeo ya uchunguzi wa mgogoro wa mgodi huo na wananchi inaeleza.

Magwangala ni vipande vya mawe vinavyobaki baada ya mgodi huo kuondoa madini ya dhahabu. Kwa kawaida magwangala husalia na sehemu ndogo ya dhahabu, ambayo wananchi huyataka kwa ajili ya kujipatia riziki.

Ripoti za vifo hivyo imetolewa na kamati iliyoundwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Februari mwaka huu kwa ajili ya kutafuta mwafaka baina ya viongozi wa mgodi wa Acacia North Mara na wananchi.


Kamati hiyo ilimjumuisha Kamishna wa Madini, John Mayopa, ambaye alikuwa mwenyekiti, John Heche (mbunge wa Tarime), na wenyeviti wa vitongoji na Serikali za Mitaa wa eneo hilo.

Alipoulizwa kuhusu ripoti ya kamati hiyo, katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa alisema tayari imeshakamilisha ripoti yake, lakini bado ipo kwa wanasheria kwa ajili ya kuhakikiwa.

“Ripoti ipo tayari lakini haijawa ‘released’ (haijatolewa) mpaka wanasheria waipitie, baada ya wiki tatu nadhani itakuwa tayari,” alisema.

Lakini gazeti la Globe and Mail la Afrika Kusini lilichapisha ripoti ya kamati hiyo ikisema idadi ya vifo hivyo imepatikana baada ya wanakijiji kuulizwa maswali kuhusu uhusiano wao na polisi wanaolinda mgodi huo unaoendeshwa na kampuni hiyo inayomilikiwa na Barrick Gold ya Canada.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top