Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MINI SHOP CHETA

Mini ShopCheta au Duka Dogo

Ni duka dogo kweli kama jina lake linavyojieleza hapo juu. Duka hili linatoa huduma ya mahitaji ya kawaida ya kila siku kwa wakazi wa Kitongoji cha Cheta pamoja na maeneo ya jirani au kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mini Shop inatoa huduma ya jamii kwa watu wote. Mini Shop ilianzishwa tangu mnamo tarehe 18/01/2018.

Tulianza tunauza bidhaa chache sana, bidhaa izo ilikuwa ni pamoja na Dawa ya Mbu zile za vidonge za kuchoma, Viberiti, Karanga, Ubuyu pamoja na Tauro za wanawake (Ped). Na kipindi icho tulikuwa tunauza bidhaa izo kutokea nyumbani kabla ya kujenga Frem hii rasmi ya kufanyia biashara kama inavyo onekana hapo kwenye picha.

Mini Shop a.k.a Duka Dogo tunauza bidhaa mbali mbali ila kwa ucheche tu, zifuatazo ni baadhi ya bidhaa tunazouza. 

Maji
Pipi
Unga
Tambi
Ngano
Amira
Juice
Mikate
Sigara

Chumvi
Mchele
Sukali
Karamu
Battery
Viwembe
Vitunguu
Viberiti
Biscuits
Madaftari

Vichongeo
Majani ya Chai
Dawa ya Mswaki
Jumbo Ball Gum
Sabuni za kuogea
Mafuta ya kupaka
Viungo vya Pirau
Mafuta ya kupikia
Sabuni za kufuria

Maharage ya Njano
Maharage ya Kombati
Tauro za wanawake (Ped)
Pon Pon au Bambino za watoto wachanga
Pia Mini Shop ni wakala wa Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Karibu sana dukani kwetu, karibu sana Mini Shop_Cheta tukuhudumie leo.


UNAWAZO LA KUANZISHA BIASHARA YAKO BINAFSI?

Mpenzi msomaji wa makala hii, napenda nikwambie kitu kwamba siku izi watu wengi wanapenda kuanzisha biashara zao binafsi uku lengo lao kuu nikuachana na kuajiliwa kisha wajiajiri wenyewe na kujipatia kipato kupitia biashara zao walizo zianzisha.

Biashara za kufanya ziponyingi sana hapa duniani,ambazo ukizisimamia vizuri zinakutimizia marengo yako.
Mini Shop_Cheta kwa wakala_Mutalemwa

Mbali ya kwamba biashara nyingi zenye faida ya haraka ni zile biashara ambazo zina madhara makubwa kwa afya wa wanadamu mfano waweza kuwa Sigara, Pombe, madawa ya kulevya nk.

Ila zipo biashara ambazo nazo zinakuwa na faida japo kuwa inapatikana taratibu na uchukua mda mrefu kidogo kuonekana tofauti na biasha nilizo tangulia kuzitaja hapo juu.

Biashara izo ni pamoja na Unga wa Sembe, Sukari, mafuta ya kula, Pipi, jojo, soda, maji, madaftari, karamu, nk. Sasa basi, ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yako yoyote ile utakayokuwa umeichagua kuianzisha unatakiwa kuwa na mipango mazubuti juu ya usimamizi na uendeshaji wa biashara yako.
Mini Shop+Cheta+kwa wakala+Mutalemwa

Mipango iyo nipamoja na kujua namna ya kutenganisha faida na pesa ya mtaji, kuweza kujua namna ya kuendesha mfumo mzima wa mauzo pamoja na manunuzi, kulipa mishahara nk.

Angalizo, huwezi kufanya biashara bila kumbukumbu, biashara yoyote ile inahitaji utunzaji wa kumbukumbu, usipoweza kipengele hiki basi jua kabisa wewe huwezi kufanya biashara yenye tija, bali unaweza kufanya biashara ya mazoea tu basi. Kujaribu sio kushindwa ebu anza leo uone miujiza ya biashara.

Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu, bofya hapa ujifunze kitu

Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekua umemkosea nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake.

Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume humfanyii jeuri na kiburi, akinuna na wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti,  utapoteza ndoa yako. 

Ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba. Asipokutafuta mtafute, asipoongea na wewe ongea naye wewe. Hakunaga mke anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe.

Kunyenyekea hakukugeuzi housegirl  na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana. 

Ujeuri weka pembeni!
ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao

NOTE: Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu. Panapotakiwa hekima na akili zitumie!

YALIYONIKUTA SITAKI YAKUKUTE WEWE, EBU JIFUNZE KUPITIA HAPA

Kwa wale watu kwa ujumla wanaoingia kwenye mahusiano hasa ya kudumu, yanaweza kuwa ndoa au ya mwelekeo wa ndoa ni vyema tukawa tumejiandaa kwa lolote litakalotokea na kulichukulia hata kama ni nzito namna gani.

Kumbuka hakuna kitu kisichokuwa na mapito au changamoto kosa kubwa tunalolifanya pale tunapoingia kwenye mahusiano hayo ni pale tunapofikiri kuwa mwenzi wako huyo ni malaika na hawezi kukosea kwa namna yoyote ila wewe ndio binadamu ukikosea usamehewe na muendelee kuvumiliana ila wewe uvumilivu huna.


Pale mnapompenda mtu jua kuwa na yeye anamadhaifu yake ambayo unatakiwa kumvumilia hata kama ni ya namna gani, hata iwe ni usaliti wa ndoa ni lazima mvumilie na sio kumuacha au kumkashifu.Utakuta mtu anasema kwa jambo hili siwezi vumilia na anasahau hata yeye anavumiliwa tu.

Ni lazima tujue kuwa huwa tunakutana na watu wanaotufaa kwa yale madhaifu yetu na sio watu wakamilifu wa madhaifu yetu, yaani mfano unaweza kukuta mwanamke hawezi labda kufua nguo vizuri na wewe swala la kufua nguo sio shida sana.

So unachotakiwa kufanya sio kudharirisha na kuwa na akili mgando ya mfumo dume hapo ni kuweka mfanya kazi au fua na sio kudharirishwa kwani mke sio mfanyakazi na kuna tofauti ya majukumu ya mfanyakazi na mke pia na heshima zao zinatofautiana, au mwanaume ni bwana mipango mzuri lakini utekelezaji wako ni ziro nawe unaweza kusimamia. Hivyo we simamia na usiwe na dharau, kwani sifa ya kwanza ya mwanamke ni utii.

KWANINI NDOA HAZIDUMU?? MAJIBU YOTE YAKO HAPA

Kwanini ndoa hazidumu?? Majibu yako hapa

Ndoa zina haribiwa na vitu vingi sana ila kwa siku ya leo tutazungumzia juu ya kitu kinachoitwa "USHIRIKINA" kwenye ndoa zetu za kiafrika.

Ushirikina ndani ya ndoa pia ni jambo ambalo kwa kiasi kikubwa sana huchangia ndoa nyingi sana kuvunjika, na kuleta madhara makubwa kwa wale waliofanyiwa ushirikina huo.

Ushirikina huo hufanyiana wao wanandoa wenyewe kwa wenyewe au hufanywa dhidi yao (yaani hufanyiwa na watu baki).

Tukianza na wanandoa wenyewe kwa wenyewe kufanyiana ushirikina, na itatubidi tuangalie pande zote mbili ili kuweka mambo sawa, upande wa wanaume, pia na upande wa wanawake.

Tuanze na upande wa wanawake: Wanawake wengi wamekuwa wakienda mbio kufanya ushirikina wakiwa ndani ya ndoa au wakiwa wameachika, na wakiwa ndani ya ndoa zao huwa wanafanya hivyo kwa malengo mengi miongoni mwa malengo hayo ni pamoja na;

1. Kuwafanya waume wao wazidishe mapenzi zaidi kwao. Kwa dhana zao mbovu kuwa mapenzi huzidishwa kwa kupitia uchawi, ndugu zangu akina mama na akina dada, mapenzi ya kweli na ya dhati hayazidishwi kwa nguvu za giza (uchawi), wala limbwata, ilo mlitambue.

Sio mapenzi ya dhati kwa sababu kinachofanywa ni kuwa mume huyo anavishwa jini ambalo huumfanya imma, apende, achukie, aache, awe mtiifu na mambo mengine kama hayo.

Ila utambue kuwa mapenzi ya kweli huzidishwa kwa kuhurumiana, kuenziana na kustahamiliana katika shida, raha na kusameheana kwa kosa kubwa au dogo na hayo yote ili yapatikane kwenye ndoa yenu lazima mume na mke wote kwa pamoja muwe ni wachamungu.

2. Kuwafanya waume zao kuwachukia wake wengine kama ni ndoa ya wake zaidi ya mmoja, ili aachike au waachike wengine abakie mwenyewe, na hii kutokana na wivu wa kipumbavu, uchoyo, roho mbaya na hasadi walizonazo wenye mioyo yao.

                     Picha kutoka maktaba 

3. Kufanya mume asiwe na maamuzi yeyote katika ndoa yake, badala yake abaki kuwa mtekelezaji tu wa chochote kile atakachoamrishwa na mkewe, kiwe cha halali au cha haramu, kiwe kinawepesi au kinauzito bwana huyo atafanya kwa sababu sio yeye bali anakuwa chini ya nguvu za jini alilovishwa.

4. Anapokuwa mwanamke ameachika lengo kubwa la kufanya ushirikina ni kumfanya mume huyo amrejee, au kumtia matatizo huyo mwanaume ili asiweze kuoa tena, au kila akioa mke mwingine asiweze kudumu naye, au kumfanyia ushirikina wenye kumpunguza nguvu za kiume, au kumuathiri kiuchumi, au kumfanya apate wazimu, au hata kumuua, au kumsababishia matatizo mengi.

Sasa tuangalie ushirikina kwa upande wa wanaume; pia nako huku tunakuta kuwa wanaume nao wanafanya ushirikina katika ndoa zao wakiwafanyia wake wao kwa malengo kama yafuatayo hapo chini.

1. Kumdhibiti mke muovu ili awe mwema. Jambo ambalo halina ukweli wowote kwa sababu njia ya kumuelekeza na kumsaidia mtu si kwa kutumia ushirikina, bali ni kurekebisha ufahamu wake kwa kutumia maneno yenye nguvu ya Mungu.
(Hakuna kitabu cha dini kinacho mruhusu mwanadamu kutenda dhambi au maovu).

2. Vile vile wanaume hufanya ushirikina kwa lengo la kuwafanya wake wawe watiifu zaidi na waogope kuzini nje ya ndoa zao, hufanya vile wakimaanisha kwamba wake zao wakizini tu nje ya ndoa basi waume hao wajue, au wakizini nje ya ndoa zao wagandane na hao waliozini nao, watu wa pwani wanaita/sema “tego”.

3. Pia kama watakuwa wamewaacha hao wake zao hufanya ushirikina kwa lengo la kurudiana nao, au kumhusudu katika mambo mbalimbali kama kumtia maradhi kama vile; kutokwa damu nyingi sehemu za siri, kumfanya asizae, au asiolewe na mume mwingine nk.

Mara nyingi ushirikina kama huu hufanywa na wanaume hao hasa kama ukorofi wao ndio uliopelekea wake zao kudai talaka, au kuachishwa kinguvu, hali ya kuwa wao bado walikuwa wanawahitaji hao wake zao.

Ebu tuangalie ushirikina ambao unakuwa ni dhidi ya wanandoa; ushirikina ambao unakuwa ni dhidi ya wanandoa ni ule ushirikina wa watu wenye husuda wasiotaka kuona ndoa za watu zinadumu, na watu kuishi kwa raha na maelewano.

Na wakati mwingine watekelezaji wa ushirikina wa namna hii ni wanafamilia au wana ukoo kama Baba, Mama, Dada, Shangazi, Mjomba au watu wengine wa nje ya familia na ukoo huo.

Niwakati wako wa kujitafakari ukiwa kama mwana ndoa, je uko upande gani? Na kwa nini umeamua kuwa upande huo?

EVERYTHING IN MARRIAGE IS POSIBLE, GO HERE FOR MORE INFO

Nowadays incidences of heart break between couples is increasing probably because of long distance between couples, and cheating, also cheating is not being accepted for all parents in our families.

Money greedy, religious and race reasons, endless fights, loss of feelings, death of one you loved and so other things.

Those incidences have caused a lot of problems in our families community like confusion, suicide, poor performance in the offices, in the class, in the decision, also loss of focus in the life, quitting of job and etc.

Generally, heart breaking can't be prevented but complications coming from heart break can be prevented  and someone can go back in his or her previous normal life as before. So in order you win in this progress please try to avoid the following in your marriage.

1. Delete your ex contact, this is main source of conflict in your marriage, keep on calling or texting his or her will make things worse especially if she or he doesn't want you anymore and probably you are replaced ready by someone else, so just keep quite and even if you have the number in your head don't write them any ware because silence is the best weapons.

2. Be busy with other things, go out with friends, visit places where you was never visited before, watch action movies, and avoid to listen love songs or movies by the time being because they will eat you and don't just stay alone thinking all day long.

3. Don't hide your feelings, tell your friends or other members of your families  or relative and other people what happened to you and what will easy your pain and you will feel at least relaxed, but hiding things won't do any good to you.

4. Don't stop your tears, if you feel like crying please don't force your heart to stop what you support to do is cry it.

Remember this is not only what you should avoid in your marriage, there is so many things what you must be avoided for anyone who are in marriage, but for today I feel to let you know this four things. If you like Swahili news Go Here

PICHA IKIAMBATANA NA UJUMBE WA SIKU YA LEO INASEMA IVI

URAFIKI WA MASHAKA HUTOWEKA MARA SABABU HIYO IKITOWEKA

Maneno haya yamesemwa na mheshimiwa kama unavyo jionea mwenyewe kwenye picha.

MAMA MKWE HATAKI KUNIONA, BOFYA HAPA KUJUA KISA NA MKASA

Ndugu zangu, Mimi nina tatizo na mama mkwe wangu kwa kifupi nimeishi na mtoto wake kwa miaka 15, sasa na tumepata watoto wawili lakini jambo la kushangaza ametoa kauli nzito kwangu akisema kuwa ataniua, kunifunga jela, au kuniroga.

Ugomvi wetu ni watoto wangu ambao niliondoka nyumbani kwenda Morogoro kutafuta maisha, mke wangu akabaki nyumbani kama miezi miwili akaja kunifuata.

Tumekaa kama miezi 6 akarudi nyumbani kuchukua watoto ambao aliwaacha kwa mama yake mzazi lakini mama akamnyima watoto na aliporudi tukajadiliana na kupata jibu kuwa niende.

Mimi nikaondoka, lakini nilikutana na matusi mazito. Kwa hekima sikumjibu chochote nikaaga na kuondoka.

Ikapita miaka minne bila kuulizana chochote! Jambo la kushangaza mwanzo wa mwezi wa 8 tulikuja wote kwa ajili ya kusalimia na kuomba watoto lakini katamka wazi mbele ya mke wangu kuwa hanipendi na hataki nikanyage kwake niwe na mwanae.

Mke wangu alijua utani kumbe mama yake alikuwa hatanii. Sasa mimi nataka kuondoka nimuache mke wangu yeye hataki na anataka kujiua.

NI VIBAYA HOUSE GIRL KUOLEWA NA BABA MWENYE NYUMBA? BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Ivi ni vibaya House girl kuolewa na baba mwenye nyumba?

Ndugu msomaji wa Mutalemwa Blog, karibu kwenye makala hii maalumu, nimeamua kuandika habari hii ili kujaribu kupunguza mifarakano kwenye familia zetu especially familia zenye wafanyakazi wa ndani wanaojulikana kama house girl.

Katika mada hii Mutalemwa Blog imekuwa ikikutana na maswali mengi sana ambayo mda mwingine yalikuwa yakituchanganya hata sisi wenyewe katika kuwajibu wahusika, maswali haya malanyingi yalikuwa yakiulizwa na akina mama.

Na kwa upande wa akina baba maswali yao sio mengi ukilinganisha na akina mama, sasa napenda nianze kwa kusema mambo yafuatayo ili wote twende sawa.

WAJIBU WA MWANAUME KATIKA FAMILIA: Mwanaume anawajibu wa kutimiza mahitaji yote ya msingi katika familia yake, moja ya majukumu hayo ni pamoja na kutoa pesa za matunzo ya familia yake kadri ipasavyo, kuonyesha upendo wa dhati kwa mama pamoja na watoto wake, na mambo mengineyo nk.

WAJIBU WA MWANAMKE KATIKA FAMILIA: Mwanamke ndiye mtendaji mkuu wa familia kwa upande wa nyumbani ukiachilia mbali ya kwamba baba ndiye kichwa cha familia, mwanamke anamajukumu mengi kwa upande wa nyumbani moja ya majukumu yake ni pamoja na kupika chakula cha familia, kufua nguo za mumewe pamoja na nguo za watoto, kuakikisha nyumba pamoja na eneo linaloizunguka nyumba ni safi, kuonyesha upendo wa dhati kwa mumewe pamoja na watoto wake, nk.

                  Picha kutoka maktaba

Ndugu msomaji wa makala hii, nadhani mpaka hapo tayari umeisha anza kupata mwanga kuhusu jibu la swali la makala yetu, sasa twende kuona wajibu wa mfanya kazi wa ndani kama house girl.

House girl wajibu wake ni kuakikisha anafanya usafi wa kuizunguka eneo la  nyumba kwa nje na kufanya usafi huo kwa upande wa ndani kwa baadhi tu ya maeneo ya nyumba hiyo pamoja na kuwaogesha watoto, kufua nguo za watoto, na kufanya kazi ndogo ndogo za nyumbani.

House girl hatakiwi kufanya usafi chumbani kwa mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kufua au kupiga pasi nguo za mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kumuandalia chakula au chai mume wa mama mwenye nyumba, nk.

Sasa ukiona house girl anafanya kazo zote nilizosema kuwa hatakiwi kuzifanya pindi awapo nyumbani kwako, ukiwa kama mama mwenye akili timamu jua kabisa tayari umeamua kumuletea mumeo mke mdogo na pia usipige kelele wala kulaumu maana jitihada zote za kumuandaa mke mwenzio umezifanya wewe mwenyewe.

Ushauri wangu kwenu akina mama na akina dada nikwamba, hatukatai kuwa wafanyakazi wa ndani hawafai, ila jitaidi mfanyakazi wako awe na mipaka ya kazi, mwanaume anaamua kumuoa house girl kwa sababu yeye amechukua majukumu yote ya mama mwenye nyumba, sasa wewe mama usianze kumtupia maneno mtoto wa watu pamoja na mumeo maana yote hayo umeyataka wewe mwenyewe.

Kama umependa makala hii tafadhali Share na wenzio wajifunze kitu. Endelea kutembelea tovuti zetu zifuatazo kwa kubofya kwenye jina la tovuti husika.

1. (TAZAMA LINE)      2. (MIKOA YETU)
           


HUU NI UJUMBE MAALUMU KWA AKINA DADA, ILA NA AKINA KAKA MNAWEZA KUUPITIA


Mimi sina mengi sana ya kuongea zaidi ya kukutakia usomaji mzuri na utafakari mzuri baada ya kumaliza kusoma habari hii.

Endelea kutembelea Mutalemwa Blog tukujuze zaidi kila habari inayotufikia 

SIMU YA MKONONI UTENGENEZWAJI WAKE NI MATESO KWA BINADAMU, ZAIDI BOFYA HAPA

Upande mchafu wa simu yako ya mkononi. Wanaharakati wa haki za kibinadamu wanailaumu sekta ya utengezaji simu kwa kupuuzia ukiukaji wa haki za kibinadamu unaofanywa katika makampuni ya simu nchini China na kwenye machimbo ya madini nchini Congo.

Simu ya mkononi inaweza kuwa chombo kizuri cha mawasiliano lakini utengenezwaji wake una siri kubwa ya mateso ya kibinaadamu.

Yanayoendelea nyuma ya sekta hiyo ya kisasa na inayokua ni unyanyasaji wa wafanyakazi, au madini yaliyojaa matone ya damu kutoka maeneo yenye machafuko. Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa shirika la SETEM linalojumuisha mashirika 10 yasiyo ya kiserikali yanayoendesha kampeni ya maonyesho mbadala yenye taswira ya kukuza maadili.

Ni makampuni machache tu miongoni mwa washiriki katika kongamano hilo la simu ulimwenguni yaani Mobile World Congress (MWC) ambayo yameonyesha simu zao za kisasa “The Fairphone 2” ambayo kampuni ya Uholanzi inajaribu kuitengeneza kwa kuzingatia maadili.

Kulingana na meneja wa utangamano na umma, Daria Koreniushkina, kufuata mikondo ambayo madini ya kuunda simu hufuata si rahisi.

Mkondo huo hujumuisha zaidi ya wahusika mia moja duniani, na kwa kila madini yanayotumika hupitia hatua zisizopungua tano. Hivyo ni changamoto kubwa kuhakikisha kila hatua ni salama. Zaidi soma kupitia habari hii kwa {KUBOFYA HAPA}

UNAJUA KWA NINI WAGANGA WANAWEZA KUWASAIDIA WATU KUWA MATAJIRI WAKATI WAO NI MASIKINI?? BOFYA HAPA KUJUA MBINU ZAO

Unajua Kwa Nini Waganga Wanaweza Kuwasaidia Watu Kuwa Matajiri Wakati Wao Ni Masikini? Soma Hapa Ili Uweze Kutumia Mbinu Hiyo.

Karibu msomaji kwenye mfululizo huu wa makala za uchawi na mafanikio. Kama tulivyoona wiki iliyopita ni kweli kwamba kuna watu ambao wanapata mafanikio makubwa kwa kutumia uchawi. Ila mafanikio yale hayaletwi na uchawi bali imani ya mtu husika.

Wiki hii tutajadili kwa nini waganga wanaweza kuwapatia watu wengine dawa au mbinu za kuwa matajiri wakati wao ni masikini? Na pia tutaangalia jinsi ambavyo unaweza kutumia mbinu hizi wanazotumia waganga bila ya wewe kuwa mchawi na ukafikia mafanikio makubwa.

Kila mmoja wetu anaelewa kwamba kuna watu wanakwenda kwa waganga na wanasaidiwa kupata utajiri. Japokuwa utajiri huu haudumu, lakini angalau wanaupata kwa kiwango fulani.

Wakati waganga hawa wanawasaidia watu kuweza kujenga magorofa, wao bado wanakaa kwenye vibanda vya nyasi. Sasa kwa nini wao wasingetumia uchawi wao na kuwa matajiri zaidi ya hao wateja wao? Ina maana wao hawapendi utajiri huo?

Mbinu za waganga kuwasaidia watu kupata utajiri. Watu wanaokwenda kwa waganga ili kupata utajiri au mafanikio yoyote hupewa masharti ambayo ni magumu kwa kiasi fulani. Na watu hawa huambiwa wakivunja masharti hayo tu utajiri wao unaisha mara moja.

Ni masharti haya ambayo humjengea mtu nidhamu kubwa sana na kumfanya aweze kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko wengine ambao wanafanya anachofanya. Kwa mfano mganga anamwambia mtu kila siku aamke asubuhi na mapema sana na apasue nazi barabarani ndio aende kwenye biashara zake.

Kupasua nazi hakuna uhusiano wowote na mafanikio yake ila kuamka asubuhi na mapema kila siku ina msaada mkubwa kwenye mafanikio yake. Hivyo mtu huyu atafuata masharti haya kila siku na hata kama kuna siku hajisikii itambidi afanye tu kwa sababu ameshaaminishwa akiacha atafilisika.

Sasa wewe ambaye huna sharti la aina hii siku ukiwa hujisikii vizuri unalala, siku nyingine unachelewa na hivyo kushindwa kufikia mafanikio makubwa. Masharti mengine kama kutokufanya starehe, kutokunywa pombe, kuvaa nguo moja na mengine mengi yanapelekea mtu kupunguza matumizi na kupata muda mwingi wa kufikiria kazi au biashara yake.

Masharti mengine yanayotolewa na waganga ni kumfanya mtu aweze kuondoka kwenye woga wake(comfort zone). Kila mmoja wetu kuna vitu fulani anaogopa kufanya, lakini vitu hivi ndio vinaweza kumletea mafanikio.

Ili kukuondolea woga huu mganga anamfanya mtu afanye jambo kubwa sana ambalo litamuondolea woga kabisa. Kwa mfano mtu anaambiwa aue, kwa kuona kwamba ameweza kuua mtu, inamfanya mtu asizuiwe na kitu chochote.

Kikubwa ambacho mganga anamsaidia mtu ni kumjengea utaratibu ambao lazima kila siku ataufuata na pia kumjengea nidhamu binafsi na hivyo kuweza kufanya jambo hata kama hajisikii kufanya. Na hili ndio hitaji kubwa la kuweza kufikia mafanikio.
Kwa nini waganga hawawezi kutumia mbinu hii wenyewe.

Kwa sababu wanajua inavyofanya kazi na pia hawana mtu wa kuwajengea imani hiyo kubwa kwao wenyewe.

Kwa nini watu baadae hufilisika?
Wengi hufilisika baadae kwa sababu wanapopata mafanikio wanasahau kutumia yale masharti waliyopewa na pia imani yao inakuwa imewekwa kwenye vitu fulani(mfano hirizi) badala ya kuwa kwao wenyewe. Ufanyeje ili uweze kutumia mbinu hii kufikia mafanikio.

Cha kwanza kabisa lazima ujijengee nidhamu binafsi.(Mwezi huu kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunajifunza jinsi ya kujijengea nidhamu binafsi, karibu ujifunze). Jiwekee masharti yako ambayo utayafuata kila siku na hakikisha unayafuata.

Kwa mfano weka utaratibu kwamba kila siku utakuwa unaamka saa kumi asubuhi, kuipanga siku yako na kisha kujisomea kidogo. Baada ya hapo unawahi kwenye eneo lako la kazi au biashara na kuanza kazi zako mapema. Pia unaweza kujiwekea utaratibu kwamba kila mteja au mtu yeyote unayekutana naye kwenye siku husika atajisikia vizuri kukutana na wewe.

Fuata masharti haya kila siku na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako na shughuli zako. Kwa hiyo mpaka sasa una mbinu mbili za uhakika za kufikia mafanikio ambazo ni pamoja na;

1. Una uwezo mkubwa uko ndani yako, ila unatakiwa kuwa na imani kubwa sana kwamba unaweza kupata kile unachotaka.(tulijifunza wiki iliyopita)

2. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na masharti(rituals) na uwe na utaratibu wa kufanya kila siku(routine). Vitu hivi jiwekee mwenyewe na vifuate kila siku kwenye maisha yako.

Ukiweza kufanya mambo hayo mawili ni lazima utafikia mafanikio makubwa. Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio. Kumbuka unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana bila ya kutumia uchawi au kwenda kwa mganga, uchawi kamili upo kwenye kichwa chako. Anza kuutumia sasa.

Chanzo: Jamii Forum 
Endelea kutembelea Mutalemwa Blog.

MAMBO 13 YA KUDUMISHA MAHUSIANO YAKO EWE MWANAMKE, YAKO HAPA BOFYA KWENYE PICHA


1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubutu wako.

2. Mwanamke anaemuheshimu mumewe ni mwanamke bora ambae kila mwanaume angetamani kuwa nae.

3. Tabia yako na misimamo yako ndio itakayomfanya mumeo ajute au afurahie kukuoa wewe.

4. Kuwa mke bora inakubidi uwe vizuri katika maarifa ya kutawala hasira zako na sio kuwa mtu wa kulipiza visasi.

5. Kuwa kiongozi huko kazini kwako lakini kuwa mtu wa kunyenyekea nyumbani kwako kwa mumeo. Hiyo ni busara.

6. Usiweke mashindano na mumeo, mpe hongea na mtie moyo kwa kila hatua anayopiga katika maisha.

7. Kuwa na ubinadamu, sio kosa dogo tu mumeo amefanya ukatamani kulipiza kisasi. It won't help u!

8. Kuwa mkarimu, kila mwanaume anamuheshimu mwanamke mkarimu na mwenye msimamo.

9. Usijaribu kumpa adhabu mumeo ya kumnyima chakula cha usiku kitandani, hii itamlazimu kutafuta chakula nje ya ndoa.

10. Hakuna kitu kibaya kama utakubali kuwa ulikosea kama kweli ulikosea. Kuwa mrahisi kukubali kama kweli ulikosea. Na omba radhi pale inapobidi.

11. Jiandae kumsamehe  mumeo pale anapokosea kwa maana mke atoae msamaha kwa mumewe ni mke mwema tofauti na yule aliejaa visasi.

12. Tengeneza maamuzi ya kuwa mke mwema, pasina kuwa na hofu yoyote na Mungu atakubariki.

13. La mwisho na la muhimu tambua kwamba mwanamke aliejaliwa umbo zuri na sura nzuri pasina maarifa kichwani anafaa kwa usiku mmoja, lakin yule mwenye maarifa na ufahamu yeya afaa kwa maisha yote!

NOBODY IS A TOTAL FAILURE IF HE DARES TO TRY TO DO SOMETHING

Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope. They caught a new vision and began to dream again.
Are you facing tough times today?  Overwhelmed? I invite you to take a walk with me. Let me tell you about survivors and how you can be one too! In the process your life will become a light for someone else's pathway.

The path is called "The Possibility Thinking Path." I've been preaching it for years. It has never let me down. It has never let anybody down. It never quits on us. We may quit the path, but the path keeps right on going on to happiness, health and prosperity.

WASANII WANAMALIZWA NA KITU HIKI HAPA, SOMA ZAIDI UJUE


kinacho wamaliza wasanii wa bongo ni hiki hapa
Kullu nafsin zaikatul maut! Huo ni mstari katika kitabu kitakatifu cha Quran unaomaanisha kila nafsi itaonja mauti. Wimbi la vifo vya wasanii linazidi kuitingisha tasnia ya burudani Bongo. Ndani ya kipindi kifupi cha miaka michache iliyopita, tumeshuhudia wasanii wengi wa filamu na muziki, maarufu na wasio maarufu, wakipoteza maisha kwa sababu mbalimbali.

 
Marehemu Recho Haule enzi za uhai wake. Wataalamu wa afya akiwemo Dk. Mandai A. Mandai wa hospitali ya Temeke ambaye alitaja sababu zinazosababisha wasanii wengi kufariki: 1. KUKOSA TABIA YA KUPIMA AFYA MARA KWA MARA, Wasanii wengi wa Kibongo hawana utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara. Wengi huenda hospitali wakiwa tayari wanaumwa na matokeo yake, hata yale maradhi ya kawaida ambayo yangeweza kutibika mapema na kupona, yakiwemo malaria, kifua kikuu na mengineyo, huwasababishia vifo. 

2. MTINDO WA MAISHA Mtindo wa maisha ya mastaa wa Kibongo unashangaza sana. Wengi wanakesha kwenye kumbi za starehe wakinywa pombe kali, kuvuta sigara na kufanya ngono, jambo ambalo ni hatari kwa afya zao huku wakisahau kabisa kumcha Mungu wao. 
Wengi hawapati muda wa kutosha wa kulala na kupumzisha miili yao, hawali chakula bora wala hawafanyi mazoezi ya mwili, matokeo yake, wakipatwa na maradhi hata yale ambayo ni ya kawaida, kinga za miili yao zinakuwa chini na kusababisha wapoteze maisha.

Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake. “Ili mwili wa binadamu uwe na afya bora, mtu anapaswa kulala kwa saa zisizopungua nane kila siku, kunywa maji mengi, kula chakula bora, kufanya mazoezi na kuepuka matumizi makubwa ya pombe na uvutaji sigara,” Dokta A. Mandai wa Hospitali ya Temeke ameliambia Ijumaa. 

3. MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA Hili ni janga lingine linalowapukutisha wasanii wengi Bongo. Albert Mangwea ‘Ngwair’, Langa Kileo, Aisha Madinda, Malick Ahmed ‘Mack 2B Simba’, Ahmed Ally Upete ‘Geez Mabovu’ na wengine wengi, ni miongoni mwa wasanii ambao kwa namna moja au nyingine, vifo vyao vimechangiwa kwa kiasi kikubwa na madawa ya kulevya. 
Bado idadi ya wasanii wengine wanaoendelea kutumia madawa hayo hatari ni kubwa na kama jitihada za haraka hazitatumika kuwanusuru, huenda nao wakapitia njia hiyohiyo (japo hatuombei itokee). 

4. AJALI ZA BARABARANI Dairekta maarufu na msanii wa filamu Bongo, George Tyson, kifo chake kilisababishwa na ajali ya gari na kuacha simanzi kubwa kwenye tasnia ya filamu. Hali kadhalika msanii Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, naye maisha yake yalikatizwa na ajali mbaya ya gari iliyotokea Muheza, Tanga.Naye Abuu Semhando, aliyekuwa mpiga drums wa Bendi ya Twanga Pepeta, alifariki kwa kugongwa na gari akiwa anaendesha pikipiki, maeneo ya Mbezi Beach.

JIHADHARI, HAYA NI MAZINGIRA KISHERIA AMBAPO ALIYEKUUZIA ARDHI ANAWEZA KUDAI TENA UMILIKI NA AKAUPATA

Kisheria yapo  mazingira  ambapo  mtu  aliyeuza  ardhi  anaweza  kuidai tena  ardhi  ileile  aliyouza kutoka kwa mnunuzi na  akaipata. Na  hapa  haijalishi  kama  mnunuzi  ameiendeleza  ardhi  kwa  kiasi  gani au  amebadilisha hati na kuingia  jina  lake  na  vitu  vingine  kama  hivyo. 

Sheria  imetoa  haki  hii  kwa  muuzaji  hasa  iwapo  masharti  katika   mkataba  wa  mauziano  yamevunjwa. Kwa  kawaida  kila  mkataba  wa  mauziano  ya  ardhi  huwa  na  masharti  ambayo  hupaswa  kutekelezwa na  kila  upande. Masharti  haya  huwa  ni  ya  msingi  na  hupaswa  kutekelezwa  vilevile  kama  ilivyokubaliwa.

Kuvunjwa/kukiukwa  kwake  hutoa  haki  kwa  muuzaji  kuchukua  tena  kilicho  chake yaani  kujirejeshea  umiliki  wa  ardhi. Na  hii  mara nyingi  husababishwa  na  kuingia  mikataba  kiholela  bila  kupata  ushauri  au  kusimamiwa  na  wanasheria ambao hupanga masharti  haya  kwa ufundi  usio na madhara. Hapa  chini tutaona  jambo  hili hufanyikaje  kisheria.

1.MUUZAJI  KUJIMILIKISHA  TENA  ARDHI  BAADA  YA  KUUZA.

Sehemu  ndogo  ya  tatu,  kifungu  cha 73 – 76 cha  Sheria  ya Ardhi   ndivyo  vifungu  katika sheria  ya  ardhi  vinavyoeleza  kwa  urefu  namna  ya  kujimilikisha  tena  ardhi  baada  ya  kuiuza. 

 Kifungu  cha  73  kinaanza  kwa  kusema  kuwa.   mkataba  wa  mauziano  ya  ardhi  unapokuwa  umekamilika   na  mnunuzi  ameshakuwa  mmiliki  wa  ardhi  aliyonunua,  muuzaji  anaweza  kujitoa  katika  mkataba  huo   pale  ambapo  mnunuzi  atakiuka  au  kwenda  kinyume  na  masharti  au  makubaliano  katika  mkataba  huo. Maana  iliyo katika  kifungu hiki  ni  kuwa  tayari mkataba  umekamilika,  na mnunuzi  amemiliki  lile  eneo iwe  nyumba, shamba  au  kiwanja . 

Na  amemiliki  kwa  kiwango  kuwa  mpaka hati/leseni  ya  makazi/ofa n.k   tayari  ina  jina  lake,  lakini  kuna  mambo  aliahidiana  na yule  aliyemuuzia  na  bado  hajayatekeleza  mpaka  sasa. Basi  huyu  aliyemuuzia  ana  haki ya  kudai  umiliki  au  kuchukua  tena  ile  ardhi. Anachukuaje  ile  ardhi  tutaona  hapa  chini.

2.  SABABU  ZA  KUJIREJESHEA  UMILIKI  BAADA  YA  KUUZA.

Sababu  kubwa za  kisheria  za  muuzaji  kujitoa  katika  mkataba  na  kujirejeshea  umiliki  ni  kutokufuatwa  kwa  masharti  au  makubaliano  yaliyo  katika  mkataba  wa  mauzo( sale  agreement).  

Kwa  mfano  kutomaliziwa  kwa hela . Unakuta  mnunuzi  ameahidi  kuwa  atamalizia  kiwango  cha  hela  kilichobaki  ndani  ya  miezi  mitatu  tangu  siku  ya  kusainiwa  kwa  mkataba. Muda  huo  unafika  mpaka  unapita mnunuzi  hataki  kulipa  hela  na  tayari  anamiliki  eneo. Au  ni  ardhi  ya kijiji  na  ameahidi  kuiendeleza  ndani  ya muda  fulani  lakini  bado  hajafanya  hivyo na  muda  umepita sasa.  Haya  ndio  mazingira na kwa  ufupi  hii  huhusisha  kutotekelezwa  kwa yale  aliyoahidi  mnunuzi   katika  mkataba  wa mauzo si  lazima  yawe hayo  tu  niliyotaja.

SERIKALI YA PUNGUZA TOZO YA ARDHI KWA ASILIMIA 50% LEO

Ndugu mdau wangu napenda kukujuza jambo muhimu sana juu ya kupungua kwa tozo ya ardhi kwa asilimia 50 ya thamani ya ardhi husika.
 Habari hii imetolewa na mhe. William Lukuvi ambaye ni waziri wa ardhi, nyumba na makzi kutoka makao makuu ya nchi mjini Dodoma jana.
Habari kamili inapatikana hapa hapa, kumsikiliza mhe.Lukuvi alichokisema

                                              |>>BOFYA HAPA<<|

HAIJAWAI KUTOKEA KWA WATOTO KUWA NA KIPAJI KAMAHIKI

Mtoto huyu anakipaji cha ajabu sana, maana sijawai kuona wala kusikia mtoto mwenye uwezo kama wa mtoto huyu. Ebu mtazame kwanza kwenye video yake hapo chini kisha share kwa marafiki zako.


Share kwa marafiki zako kama hautojari.

  


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    

In order you follow me just click one of the Icon Button above.

JIFUNZE JAMBO JIPYA KUTOKA KWENYE KITABU KITAKATIFU

Siku zote hakuna kitu kikubwa na chenye thamani kubwa kama kitabu cha Mungu, kwaiyo basi leo nakuletea kitabu kitukufu cha Mungu, ili uweze kujifunza kitu kipya.


Waweza kushare habari hii kwa marafiki zako wote nawao wajifunze kitu kipya kutoka hapa.
  


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    

In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top