Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

UNAJUA KWA NINI WAGANGA WANAWEZA KUWASAIDIA WATU KUWA MATAJIRI WAKATI WAO NI MASIKINI?? BOFYA HAPA KUJUA MBINU ZAO

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Unajua Kwa Nini Waganga Wanaweza Kuwasaidia Watu Kuwa Matajiri Wakati Wao Ni Masikini? Soma Hapa Ili Uweze Kutumia Mbinu Hiyo.

Karibu msomaji kwenye mfululizo huu wa makala za uchawi na mafanikio. Kama tulivyoona wiki iliyopita ni kweli kwamba kuna watu ambao wanapata mafanikio makubwa kwa kutumia uchawi. Ila mafanikio yale hayaletwi na uchawi bali imani ya mtu husika.

Wiki hii tutajadili kwa nini waganga wanaweza kuwapatia watu wengine dawa au mbinu za kuwa matajiri wakati wao ni masikini? Na pia tutaangalia jinsi ambavyo unaweza kutumia mbinu hizi wanazotumia waganga bila ya wewe kuwa mchawi na ukafikia mafanikio makubwa.

Kila mmoja wetu anaelewa kwamba kuna watu wanakwenda kwa waganga na wanasaidiwa kupata utajiri. Japokuwa utajiri huu haudumu, lakini angalau wanaupata kwa kiwango fulani.

Wakati waganga hawa wanawasaidia watu kuweza kujenga magorofa, wao bado wanakaa kwenye vibanda vya nyasi. Sasa kwa nini wao wasingetumia uchawi wao na kuwa matajiri zaidi ya hao wateja wao? Ina maana wao hawapendi utajiri huo?

Mbinu za waganga kuwasaidia watu kupata utajiri. Watu wanaokwenda kwa waganga ili kupata utajiri au mafanikio yoyote hupewa masharti ambayo ni magumu kwa kiasi fulani. Na watu hawa huambiwa wakivunja masharti hayo tu utajiri wao unaisha mara moja.

Ni masharti haya ambayo humjengea mtu nidhamu kubwa sana na kumfanya aweze kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko wengine ambao wanafanya anachofanya. Kwa mfano mganga anamwambia mtu kila siku aamke asubuhi na mapema sana na apasue nazi barabarani ndio aende kwenye biashara zake.

Kupasua nazi hakuna uhusiano wowote na mafanikio yake ila kuamka asubuhi na mapema kila siku ina msaada mkubwa kwenye mafanikio yake. Hivyo mtu huyu atafuata masharti haya kila siku na hata kama kuna siku hajisikii itambidi afanye tu kwa sababu ameshaaminishwa akiacha atafilisika.

Sasa wewe ambaye huna sharti la aina hii siku ukiwa hujisikii vizuri unalala, siku nyingine unachelewa na hivyo kushindwa kufikia mafanikio makubwa. Masharti mengine kama kutokufanya starehe, kutokunywa pombe, kuvaa nguo moja na mengine mengi yanapelekea mtu kupunguza matumizi na kupata muda mwingi wa kufikiria kazi au biashara yake.

Masharti mengine yanayotolewa na waganga ni kumfanya mtu aweze kuondoka kwenye woga wake(comfort zone). Kila mmoja wetu kuna vitu fulani anaogopa kufanya, lakini vitu hivi ndio vinaweza kumletea mafanikio.

Ili kukuondolea woga huu mganga anamfanya mtu afanye jambo kubwa sana ambalo litamuondolea woga kabisa. Kwa mfano mtu anaambiwa aue, kwa kuona kwamba ameweza kuua mtu, inamfanya mtu asizuiwe na kitu chochote.

Kikubwa ambacho mganga anamsaidia mtu ni kumjengea utaratibu ambao lazima kila siku ataufuata na pia kumjengea nidhamu binafsi na hivyo kuweza kufanya jambo hata kama hajisikii kufanya. Na hili ndio hitaji kubwa la kuweza kufikia mafanikio.
Kwa nini waganga hawawezi kutumia mbinu hii wenyewe.

Kwa sababu wanajua inavyofanya kazi na pia hawana mtu wa kuwajengea imani hiyo kubwa kwao wenyewe.

Kwa nini watu baadae hufilisika?
Wengi hufilisika baadae kwa sababu wanapopata mafanikio wanasahau kutumia yale masharti waliyopewa na pia imani yao inakuwa imewekwa kwenye vitu fulani(mfano hirizi) badala ya kuwa kwao wenyewe. Ufanyeje ili uweze kutumia mbinu hii kufikia mafanikio.

Cha kwanza kabisa lazima ujijengee nidhamu binafsi.(Mwezi huu kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunajifunza jinsi ya kujijengea nidhamu binafsi, karibu ujifunze). Jiwekee masharti yako ambayo utayafuata kila siku na hakikisha unayafuata.

Kwa mfano weka utaratibu kwamba kila siku utakuwa unaamka saa kumi asubuhi, kuipanga siku yako na kisha kujisomea kidogo. Baada ya hapo unawahi kwenye eneo lako la kazi au biashara na kuanza kazi zako mapema. Pia unaweza kujiwekea utaratibu kwamba kila mteja au mtu yeyote unayekutana naye kwenye siku husika atajisikia vizuri kukutana na wewe.

Fuata masharti haya kila siku na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako na shughuli zako. Kwa hiyo mpaka sasa una mbinu mbili za uhakika za kufikia mafanikio ambazo ni pamoja na;

1. Una uwezo mkubwa uko ndani yako, ila unatakiwa kuwa na imani kubwa sana kwamba unaweza kupata kile unachotaka.(tulijifunza wiki iliyopita)

2. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na masharti(rituals) na uwe na utaratibu wa kufanya kila siku(routine). Vitu hivi jiwekee mwenyewe na vifuate kila siku kwenye maisha yako.

Ukiweza kufanya mambo hayo mawili ni lazima utafikia mafanikio makubwa. Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio. Kumbuka unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana bila ya kutumia uchawi au kwenda kwa mganga, uchawi kamili upo kwenye kichwa chako. Anza kuutumia sasa.

Chanzo: Jamii Forum 
Endelea kutembelea Mutalemwa Blog.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top