MINI SHOP CHETA
(TCRA), has fined two radio stations
Kutoka CHETA KAZOLE kwenda VIKINDU GETINI ni 6.749Km Pekee.
Ila panaonekana kuwa mbali kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo ikiwemo ubovu wa barabara, ukosefu wa umeme, hospital/ Zahanati nk.
KAZOLE: MKOMBOZI WA NYATI CEMENT INDUSTRY NI BARABARA YA VIKINDU GETINI KUPITIA KAZOLE, CHETA, MAGODANI, MWASONGA HADI KIMBIJI.
Kimbiji kuna muwekezaji wa kiwanda cha Nyati cement ambapo katika utoaji wa huduma yake kwa watanzania hulazimika kutumia barabara ya Kibada uku Kigamboni ili kusafirisha cement kutokea Kimbiji hadi mjini.
Lakini kuna barabara ambayo ni fupi sana kuliko ile anayoitumia muwekezaji uyo wa kiwanda cha Nyati Cement kwa sasa.
Barabara iyo fupi inayozungumziwa ni ile inayoanzia Vikindu Getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji na kuunganisha maeneo mbali mbali ya katikati ambayo ayajatajwa.
Kuimarika kwa barabara hii ya Vikindu Getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji kutampunguzia muwekezaji huyu adha ya usafirishaji wa Cement yake na kumuongezea nguvu ya kuzalisha cement nyingi zaidi.
Pia kuimarika kwa barabara hii ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji kutatoa fursa kwa wakazi wa maeneo tajwa kukua kibiashara, kiuchumi ata kisiasa nk.
Kwa sasa barabara hii ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji ipo kama unavyo iona kwenye picha hapo juu na chini.
Pia wakazi wa maeneo tajwa wanapata shida sana katika kusafiri, ambapo kutoka Vikindu getini hadi Kazole magenge 20 ni umbali wa dakika 15 hadi 20 ila kila abiria hutozwa Tsh. 500 na mwanafunzi tsh. 200 hadi tsh. 250.
Huku Noah zinazoanzia Vikindu getini kwenda hadi Magodani zikipitia Kazole magenge 20 pamoja na Cheta kila abiria anatozwa Tsh. 1,000 ukiwa ni umbali wa kama dakika 30 hadi 35 tu.
Izo bei za nauri hutozwa kipindi cha kiangazi ila ikifika masika nauri upanda hadi mara 4, wakazi wa Kazole ulipa tsh. 2,000 na wakazi wa Cheta na Magodani ulipa tsh. 4,000 na Boda boda uwa ni kati ya tsh. 5,000 mpaka tsh. 10,000
Lakini mbali ya nauri kuwajuu namna hiyo japo sio viwango elekezi kutoka SUMATRA, bado kuna changamoto ya uchache wa magari yanayotoa huduma, kwaiyo tunamuomba Mhe. Rais Magufuri na serikari yake kupitia wizara ya ujenzi walitazame swala hili kwa jicho la tatu.
Habari zaidi kuhusu Kazole, Cheta na Magodani zisome kupitia hapo chini.
Barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu kufanyiwa ukarabati.
WAKAZI WA CHETA WANATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI NA KANISA
CHETA TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI, KANISA NA VIWANJA VYA MICHEZO.
![]() |
CHETA TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI, KANISA NA VIWANJA VYA MICHEZO. |
![]() |
CHETA TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI, KANISA NA VIWANJA VYA MICHEZO. |
![]() |
CHETA TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI, KANISA NA VIWANJA VYA MICHEZO. |
Kauli ya mhe.Zitto Kabwe juu ya mbunge wa Mtama Nape Nnauye kuondolewa kwenye uwaziri iko hapa
Nape ni shujaa wa kizazi chetu" Zitto Kabwe.
KITUO CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI KUAMISHIWA MKURANGA, INGIA HAPA.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa wilaya za Mkuranga na Temeke, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Moja ya hatua alizowashauri kuchukua ni pamoja na kuhamisha kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutoka Temeke hadi Mkuranga.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na viongozi wa wilaya hizo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafua njia za kuondoa msongamano huo.
Amesema kwa sasa hakuna namna ambayo wataweza kuondoa msongamano huo zaidi ya kuhamishia kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini wilayani Mkuranga.
Waziri Mkuu amesema eneo la Mbagala kwa sasa lina msongamano mkubwa ambao ni lazima Serikali ichukue hatua za haraka za kuuondoa.
“Ikiwezekana mabasi ya mikoa ya kusini yaishie Mkuranga, hivyo shirikianeni kutafuta eneo la kujenga kituo kikubwa cha kisasa cha mabasi,” amesema.
Amesema kituo hicho watakachokijenga kiwe na uwezo wa kuhudumia mabasi yote yatokayo mikoa ya kusini na kituo cha Mbagala kiwe cha daladala za kawaida.
Pia Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kutawezesha kuongeza mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.
Aidha Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kwenda kujadiliana katika vikao vya mabaraza ya Madiwani juu ya mkakati huo na kisha kumpelekea taarifa ifikapo Februari 15 mwaka huu.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Bw. Filberto Sanga amesema wazo hilo ni zuri na wilaya yake ina maeneo ya kutosha kujenga miundombinu hiyo.
“Ni kweli wilaya ya Temeke imeelemewa kwa maana ya maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maendeleo na haina pa kupumulia zaidi ya Mkuranga , hivyo tupo tayari kushirikiana nao,” amesema.
Wakati huo huo, Bw. Sanga ameiomba Serikali itakapoanza awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi ufike hadi Mkuranga mjini badala ya kuishia Vikindu.
Amesema kwa sasa wilaya yake ina viwanda 67 ambavyo kati yake vipo vinavyofanya kazi na vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, hivyo mabasi hayo yatarahisisha usafiri kwa wafanyakazi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva amesema amefurahishwa sana na mawazo hayo ya kuhamisha kituo cha mabasi cha Mbagala kwani katika vitu vilivyokuwa vinamnyima usingizi ni pamoja na msongamano wa mabasi na wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo hilo.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV, AYO TV na Global TV kusitisha huduma zao za TV
Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James Kilaba tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.
“Kwa mujibu wa section 13 (1) of the electronic and postal communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano,” imesema barua hiyo.
Wamiliki wa mitandao hiyo Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi na Abdallah Mrisho wameeleza kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe hazijawekwa.
“Global TV ipo tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili kama zingekuwepo na kwa sababu bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi chini ya uangalizi wakati tunasubiria kanuni hizo mpya,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa Global Publishers.
Ankal Michuzi na Millard Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja watatu hao wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi ya kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa.
Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa kushughuliwa ataporejea wiki ijayo.
“Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii,” alisema Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.
Ayo TV, Michuzi TV na Global TV ambazo zina watazamaji wengi ndani na nje ya nchi, ni TV mtandao pekee zilizoitikia mwito wa TCRA kati ya vituo mtandao takriban 51 vilivyopata barua hiyo.
Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii
Gwajima: Lengo la kikao hiki cha leo ni kuwajulisha Maaskofu wenzangu kwamba ni nini kimetokea
Gwajima: Sijawahi kunywa Pombe wala sijawahi kuvuta sigara, Mimi nlikuwa mgonjwa hadi nlipookoka nikawa mchungaji moja kwa moja. Kama sijawahi kuvuta sigara siwezi kuwa natumia madawa ya kulevya.
Gwajima: Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media?
Gwajima: Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii.
Gwajima: Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi;
1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi
2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa Kimya.
Gwajima: Nani anatakiwa kuniita mimi kama Askofu Mkuu Polisi? Ni Polisi sio Makonda. Makonda anajiona kama Mkuu wa Wakuu wa Mikoa yote na Mawaziri wote.
Gwajima: Sio desturi ya rais hata kidogo eti awatenge Mawaziri wake eti aongee na Makonda. Rais alikuwa anampongeza makonda kwa sababu kafanya Vizuri. Makonda anaujasiri na anajituma hivyo rais kumpongeza ni halali. Makonda anaweza kuwa Kiongozi Muu siku zijazo kama akiondoa baadhi ya Hitilafu.
Gwajima: Makonda angeweza kunipigia simu au Kuwagiza Polisi wakaniletea samasi au kuniita.
Gwajima: Nia ya Makonda ni kutaka jina la Gwajima liharibike. Kama Gwajima hafanyi na hajihusishi na Madawa ya kulevya watu wa Usalama wanajua. Nmefanya hii kazi ya Uchungaji kwa Miaka 20.
Gwajima: Si kweli kwamba makonda anatumwa na Rais Magufuli, rais ana tabia ya kupongeza saa nyingine anapiga simu Clouds kupongeza pale wanapofanya Vizuri.
Gwajima: Sisi tunamuunga mkono Mheshimiwa rais hata kama kwenye uchaguzi hatujamuunga mkono, Lakini kwa kuwa amechaguliwa yeye tunamuunga mkono
Gwajima: Naamin Makonda hajajificha kwenye "Usukuma" wake.
Gwajima: Namuomba rais amkanye Makonda. Chuki zake binafsi za mtu mmoja mmoja asiziingize kwenye system ya Serikali, ni hatari sana

Gwajima: Makonda ni Mchapakazi lakini Mambo ya Utawala hawezi, namuomba rais amtafutie kazi nyingine, nashauri umtafutie kazi nyingine, sio umfukuze.
Gwajima: Chini yangu kuna Maaskofu 125. Kesho wataogopa nao watasemwa
Gwajima: Kuna siku Paul Makonda, Sitta na Mwakyembe walikuja kanisani kwangu hata CD ninazo na alihutubia hapa kwenye Madhabahu akinisifia sana, Leo ni kitu gani kimemfanya anichafue?
Gwajima: Je ikiwa Gwajima hahusiki, itakuwaje?
Gwajima: Mimi nlikuwa mkali sana juu ya utawala wa awamu ya nne. Miaka kwa miaka Tembo walikuwa wanakufa na hakuna hatua zilizokuwa zinachukuliwa.
Gwajima: Kuna Kipindi Ridhiwani Kikwete aliwapeleka Mahakamani Dr. Slaa akitaka wakanushe habari kuhusu utajiri wake unaotokana na Madawa ya kulevya, hiyo kesi sijui iliishia wapi.
Gwajima: Nani anamtumia Makonda?
Gwajima: Makonda ana nia ovu juu yangu na juu ya Wakristo. Anataka kuwaaminisha watu kwamba wokovu haupo.
Gwajima: Mimi nataka kununua ndege nyingine ili nianzishe chuo cha ndege, mbona sipongezwi kwa hilo?
Gwajima: Jambo hili alilofanya si sawa na si sahihi.
Gwajima: Wabunge wamepiga kelele juu ya jambo hili, sisi wananchi tusio na sehemu ya kuongea tufanyeje?
Gwajima: Namfahamu rais Magufuli, hawezi kumpendelea kwa kuwa ni mtu wa kwao (Msukuma). Rais anawapenda watu wote anawapenda Mawaziri wote na watendaji wote wa Serikali. Naamin rais hajamtuma Makonda.
Gwajima: Nguvu katika mikono isiyo sahihi ni hatari sana.
Gwajima: Juzi kati tulikuwa na mechi kati ya maasikofu na viongozi, Mimi nlikuwa namba kumi yeye namba 09. Alikuwa ananiangalia macho baya sana mamcho alikuwa ananiangalia nayo nmekuja na helcopter ni macho ya chuki sana. Mimi, Makonda, kamanda Sirro Spika wa Bunge tulikuwa tunamechi si angenikamata hapo?
*Kuna watu walikuwa wanauza madawa ya kulevya, katika uongozi huu wale walikuwa wanauza madawa ya kulevya wamebadili majina na wanafanya biashara nyingine. Walikuwa na jina B sasa wamebadilisha jina.
Mh.Paul Makonda awataja wakubwa 65 leo wafike kituo cha polisi cha Dsm siku ya Ijumaa
Anasema anaingia awamu ya pili ya mapambano ambayo siyo nyepesi,anasema itakuwa na mawimbi mengi!.
1.Yanaingizwa kutoka Pakistan kwa meli,ikishapakia mzigo wanachukua madawa kwenye mifukonya sukari inawekwa kwenye mapipa!
Meli zikikaribia kufika mapipa hutupwa huko Zanzibar,Tanga na Bagamoyo yakiwa na GPRS,baadae hurudi walipoyatupa na kuyachukua na huyasafirisha mpaka Mtwara na baadae Afrika kusini!.
2.Kwa kutumia maghari yanayoaguswa kutoka nje,
3.Ni kwenye meli za mafuta
4.Ni wale wenye maeneo yao ya kupack mizigo!
Wengine huwatumia akina dada ,hawa hupewa dolla elfu tano ili ziwasaidie kuingia China.
Waliotajwa leo wafike kituo cha polisi cha dar es salaam siku ya Ijumaa kwa mahojiano ni pamoja na.
1.Mmiliki wa slipway
2.Mmiliki wa Yatchclub
3.Idd Azan
4.MMI Wine
5.Freeman Mbowe
6.Mwinyi Machapta
7.Mr Halfizi
8.Yusuph Manji
9.Mchungaji Gwajima
10.Wamiliki wote wa clubs na Cassino
11.Mzee Kiboko wa Mbezi chini
12.Rose ambaye anaishi Ghana
Jumla wapo 65 wanaotakiwa kuripoti polisi Ijumaa.
KAMA ULIKUWA UJAFANIKIWA KUYAONA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YA MWAKA 2016 BOFYA HAPA
Shule zilizoingia 10 bora Kitaifa.
Feza Boys Sec School – Dar es Salaam
St. Francis Girls Sec School -Mbeya
Kaizirege Junior Sec School – Kagera
Marian Gilrs Sec School – Pwani
Marian Boys Sec School- Pwani
St. Aloysius Girls Sec School – Pwani
Shamsiye Boys Sec School – Dar es Salaam
Anuarite Girls Sec School- Kilimanjaro
Kifungilo Girls Sec School- Tanga
Thomas More Machrina Sec School – Dar es Salaam
Shule za Dar es Salaam zilizoshika nafasi 10 za mwisho.
Kitonga Sec School
Nyeburu Sec School
Mbopo Sec School
Mbondole Sec School
Somangila Day Sec School
Kidete Sec School
BOFYA HAPA KUONA MATOKEO SASA
Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60
Rais Magufuli leo ametengua rasmi uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu, bofya hapa ujifunze kitu
EWURA imeridhia ombi la TANESCO la kupandishwa kwa bei ya umeme
TANESCO imetimiza agizo la Rais Magufuli la kukipatia umeme kiwanda cha Bakhresa
TANESCO imetimiza agizo la Rais Magufuli la kukipatia umeme kiwanda cha kusindika matunda mali ya mfanyabishara, Said Salim Bakhresa kabla ya muda wa miezi miwili waliyopewa kukamilisha kazi hiyo.
Rais alitoa agizo hilo Oktoba 6, 2016 alipokuwa anazindua kiwanda hicho kilichopo Mwandege, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
ILE KATA FUNUA YA UKAWA YAIBUKIA KWENYE MAKAMPUNI 6 YA KIGENI YA KUCHIMBA MADINI NCHINI
Makampuni ya kimataifa yasiyopungua sita yamesema yanafikiria kupunguza kiwango cha uwekezaji nchini Tanzania, baada ya Rais John Magufuli kutangaza kufanya mabadiliko ya kiuchumi, ikiwemo kuongeza kodi kwa makampuni kutoka nje.
Kwa mujibu wa mahojiano yaliyofanywa na shirika la habari la Reuters pamoja na wakurugenzi wakuu wa makapuni ya kigeni yaliyowekeza nchini Tanzania, kiasi ya makampuni sita yanafikiria mipango mipya kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini, mawasiliano ya simu au usafirishaji kwa kutumia meli. Hiyo yote inatokana na juhudi zinazofanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli kuubadili uchumi wa nchi hiyo.
Makampuni matatu yamesema huenda yakapunguza shughuli zake za uwekezaji kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki, huku makampuni mengine mawili yakisema yanafikiria kutanua zaidi shughuli zake katika nchi jirani na kampuni moja imesema inaandaa mchakato wa kujiondoa kabisa nchini Tanzania. Makampuni hayo yaliombwa kutotajwa majina kwa sababu ya umuhimu wa suala hili na kwa sababu mipango yao hiyo bado haijatangazwa hadharani.
Kampuni moja bado haijatoa msimamo wake jinsi ya kukabiliana na mageuzi hayo ya serikali ya Tanzania, huku makampuni matano yakisema kuwa mipango yao haikuathirika na mageuzi hayo, ikiwemo miradi miwili mikubwa, ule wa kiwanda cha kusindika gesi asilia-LNG wenye thamani ya Dola bilioni 30 na mradi wa kiwanda cha mbolea wenye thamani ya Dola bilioni 3.
Tanzania na uwekezaji wa kigeni
Tanzania inategemea zaidi uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja, kuliko nchi nyingine za ukanda huo, kutokana na ukubwa wa uchumi wake. Mwaka uliopita nchi hiyo ilipokea zaidi ya Dola bilioni 1.5, kwenye uchumi ambao thamani yake ilikuwa chini ya Dola bilioni 45. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Umoja wa Mataifa pamoja na Benki ya Dunia.
Rais wa Tanzania, John Magufuli ambaye amepewa jina la utani ''Tingatinga'' kutokana na miradi yake ya miundombinu na aina ya uongozi wake, alizindua mchakato wa mageuzi yake ya kiuchumi, baada ya kuchaguliwa kuiongoza nchi hiyo mwaka uliopita, akiahidi kuubadilisha uchumi wa nchi hiyo, kuondoa urasimu na rushwa pamoja na kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi.
Mwaka huu serikali ya Magufuli iliongeza kodi katika utumaji wa fedha kwa kutumia simu za mkononi, mabenki, huduma za utalii na zile za usafirishaji wa mizigo. Kodi ya mapato kwa mwaka wa fedha 2014/2015 jumla ilikuwa Shilingi za Tanzania trillioni 9.8 ambazo ni sawa na Dola bilioni 4.5. Kwa mwaka wa fedha 2016/2017, serikali ina lengo la kukusanya kodi ya mapato zaidi ya trilioni 15.1, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 50.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Adolf Mkenda, amesema wameyasikia malalamiko yanayotolewa na milango iko wazi, lakini wanahakikisha kuwa kila mtu analipa kodi anayopaswa kulipa kwa kuzingatia haki. Amesema lazima kuwepo na mageuzi mapya ambayo ni magumu, ili kuufanya uchumi kuwa imara.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Richard Kayombo amesema ongezeko la kodi ya mapato lilihitajika kwa ajili ya kulipia miundombinu mipya nchini humo. Makampuni makubwa ya kigeni ambayo yamewekeza nchini Tanzania ni pamoja na yale ya nishati, uhandisi, mawasiliano ya simu, madini, na usafirishaji kwa kutumia meli.
Source: Reuters Africa
Kama uliikosa Ile habari ya madada poa wa Dar, basi iko hapa kwa ajili yako
Viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza vyazidi kuongezeka nchini.Soma zaidi hapa
Viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza vyazidi kuongezeka nchini.Soma zaidi hapo chini kisha washirikishe na wenzio.
Asilimia kubwa ya wanawake tunapenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi
Zoezi la kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu linaendelea, habari kamili iko hapa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, ambaye anaongoza timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama, kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu.
Amekamata shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kukifuma kiwanda bubu kinachotengeneza konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam.
Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia 'spirit' ambayo inachanganywa na gongo.
Pia katika zoezi hilo wameweza kukamata chupa tupu na zilizojazwa pombe, vizibo, pamoja na vifungashio.
Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na polisi mpaka sasa.