Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekua umemkosea nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake.
Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume humfanyii jeuri na kiburi, akinuna na wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa yako.
Ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba. Asipokutafuta mtafute, asipoongea na wewe ongea naye wewe. Hakunaga mke anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe.
Kunyenyekea hakukugeuzi housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana.
Ujeuri weka pembeni!
ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao
NOTE: Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu. Panapotakiwa hekima na akili zitumie!