Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA imeridhia maombi ya shirika la umeme nchini TANESCO la kupandishwa kwa bei ya umeme ambapo Bei hiyo imeongezeka kwa wastani wa asilimia 8.5 tofauti na pendekezo la mwanzo la 18.19% huku watumiaji wa nishati hiyo ambao hawatumii zaidi ya unit 75 kwa mwezi wakiwa hawaguswi na ongezeko hilo.
Kwaiyo basi watumiaji wa umeme wa kawaida manyumbani watalazimika kununua Unit moja kwa Tsh 312 wakati kabla ya ongezeko ili unit moja ilikuwa ikinunuliwa kwa Tsh 292, bei izi zitaanza kutumika rasmi tarehe 01/01/2017 ikiwa ni ongezeko la Tsh 20 kwa kila unit moja.