Upande mchafu wa simu yako ya mkononi. Wanaharakati wa haki za kibinadamu wanailaumu sekta ya utengezaji simu kwa kupuuzia ukiukaji wa haki za kibinadamu unaofanywa katika makampuni ya simu nchini China na kwenye machimbo ya madini nchini Congo.
Simu ya mkononi inaweza kuwa chombo kizuri cha mawasiliano lakini utengenezwaji wake una siri kubwa ya mateso ya kibinaadamu.
Yanayoendelea nyuma ya sekta hiyo ya kisasa na inayokua ni unyanyasaji wa wafanyakazi, au madini yaliyojaa matone ya damu kutoka maeneo yenye machafuko. Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa shirika la SETEM linalojumuisha mashirika 10 yasiyo ya kiserikali yanayoendesha kampeni ya maonyesho mbadala yenye taswira ya kukuza maadili.
Ni makampuni machache tu miongoni mwa washiriki katika kongamano hilo la simu ulimwenguni yaani Mobile World Congress (MWC) ambayo yameonyesha simu zao za kisasa “The Fairphone 2” ambayo kampuni ya Uholanzi inajaribu kuitengeneza kwa kuzingatia maadili.
Kulingana na meneja wa utangamano na umma, Daria Koreniushkina, kufuata mikondo ambayo madini ya kuunda simu hufuata si rahisi.
Mkondo huo hujumuisha zaidi ya wahusika mia moja duniani, na kwa kila madini yanayotumika hupitia hatua zisizopungua tano. Hivyo ni changamoto kubwa kuhakikisha kila hatua ni salama. Zaidi soma kupitia habari hii kwa {KUBOFYA HAPA}
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies