Featured

    Featured Posts

Loading...

KWANINI NDOA HAZIDUMU?? MAJIBU YOTE YAKO HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Kwanini ndoa hazidumu?? Majibu yako hapa

Ndoa zina haribiwa na vitu vingi sana ila kwa siku ya leo tutazungumzia juu ya kitu kinachoitwa "USHIRIKINA" kwenye ndoa zetu za kiafrika.

Ushirikina ndani ya ndoa pia ni jambo ambalo kwa kiasi kikubwa sana huchangia ndoa nyingi sana kuvunjika, na kuleta madhara makubwa kwa wale waliofanyiwa ushirikina huo.

Ushirikina huo hufanyiana wao wanandoa wenyewe kwa wenyewe au hufanywa dhidi yao (yaani hufanyiwa na watu baki).

Tukianza na wanandoa wenyewe kwa wenyewe kufanyiana ushirikina, na itatubidi tuangalie pande zote mbili ili kuweka mambo sawa, upande wa wanaume, pia na upande wa wanawake.

Tuanze na upande wa wanawake: Wanawake wengi wamekuwa wakienda mbio kufanya ushirikina wakiwa ndani ya ndoa au wakiwa wameachika, na wakiwa ndani ya ndoa zao huwa wanafanya hivyo kwa malengo mengi miongoni mwa malengo hayo ni pamoja na;

1. Kuwafanya waume wao wazidishe mapenzi zaidi kwao. Kwa dhana zao mbovu kuwa mapenzi huzidishwa kwa kupitia uchawi, ndugu zangu akina mama na akina dada, mapenzi ya kweli na ya dhati hayazidishwi kwa nguvu za giza (uchawi), wala limbwata, ilo mlitambue.

Sio mapenzi ya dhati kwa sababu kinachofanywa ni kuwa mume huyo anavishwa jini ambalo huumfanya imma, apende, achukie, aache, awe mtiifu na mambo mengine kama hayo.

Ila utambue kuwa mapenzi ya kweli huzidishwa kwa kuhurumiana, kuenziana na kustahamiliana katika shida, raha na kusameheana kwa kosa kubwa au dogo na hayo yote ili yapatikane kwenye ndoa yenu lazima mume na mke wote kwa pamoja muwe ni wachamungu.

2. Kuwafanya waume zao kuwachukia wake wengine kama ni ndoa ya wake zaidi ya mmoja, ili aachike au waachike wengine abakie mwenyewe, na hii kutokana na wivu wa kipumbavu, uchoyo, roho mbaya na hasadi walizonazo wenye mioyo yao.

                     Picha kutoka maktaba 

3. Kufanya mume asiwe na maamuzi yeyote katika ndoa yake, badala yake abaki kuwa mtekelezaji tu wa chochote kile atakachoamrishwa na mkewe, kiwe cha halali au cha haramu, kiwe kinawepesi au kinauzito bwana huyo atafanya kwa sababu sio yeye bali anakuwa chini ya nguvu za jini alilovishwa.

4. Anapokuwa mwanamke ameachika lengo kubwa la kufanya ushirikina ni kumfanya mume huyo amrejee, au kumtia matatizo huyo mwanaume ili asiweze kuoa tena, au kila akioa mke mwingine asiweze kudumu naye, au kumfanyia ushirikina wenye kumpunguza nguvu za kiume, au kumuathiri kiuchumi, au kumfanya apate wazimu, au hata kumuua, au kumsababishia matatizo mengi.

Sasa tuangalie ushirikina kwa upande wa wanaume; pia nako huku tunakuta kuwa wanaume nao wanafanya ushirikina katika ndoa zao wakiwafanyia wake wao kwa malengo kama yafuatayo hapo chini.

1. Kumdhibiti mke muovu ili awe mwema. Jambo ambalo halina ukweli wowote kwa sababu njia ya kumuelekeza na kumsaidia mtu si kwa kutumia ushirikina, bali ni kurekebisha ufahamu wake kwa kutumia maneno yenye nguvu ya Mungu.
(Hakuna kitabu cha dini kinacho mruhusu mwanadamu kutenda dhambi au maovu).

2. Vile vile wanaume hufanya ushirikina kwa lengo la kuwafanya wake wawe watiifu zaidi na waogope kuzini nje ya ndoa zao, hufanya vile wakimaanisha kwamba wake zao wakizini tu nje ya ndoa basi waume hao wajue, au wakizini nje ya ndoa zao wagandane na hao waliozini nao, watu wa pwani wanaita/sema “tego”.

3. Pia kama watakuwa wamewaacha hao wake zao hufanya ushirikina kwa lengo la kurudiana nao, au kumhusudu katika mambo mbalimbali kama kumtia maradhi kama vile; kutokwa damu nyingi sehemu za siri, kumfanya asizae, au asiolewe na mume mwingine nk.

Mara nyingi ushirikina kama huu hufanywa na wanaume hao hasa kama ukorofi wao ndio uliopelekea wake zao kudai talaka, au kuachishwa kinguvu, hali ya kuwa wao bado walikuwa wanawahitaji hao wake zao.

Ebu tuangalie ushirikina ambao unakuwa ni dhidi ya wanandoa; ushirikina ambao unakuwa ni dhidi ya wanandoa ni ule ushirikina wa watu wenye husuda wasiotaka kuona ndoa za watu zinadumu, na watu kuishi kwa raha na maelewano.

Na wakati mwingine watekelezaji wa ushirikina wa namna hii ni wanafamilia au wana ukoo kama Baba, Mama, Dada, Shangazi, Mjomba au watu wengine wa nje ya familia na ukoo huo.

Niwakati wako wa kujitafakari ukiwa kama mwana ndoa, je uko upande gani? Na kwa nini umeamua kuwa upande huo?

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top