Sijui kama hii habari umeisha ipata lakini limetokea tukio baya huko Mbagala jijini Dar. Inasemekana askari walikuwa wanaelekea lindo benki ya CRDB MMBANDE. Waliofanya shambulizi wanadaiwa kuondoka na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.
======== UPDATE: ========
Waliofariki ni askali mwenye namba
1. E5761 CPL YAHAYA
2. F4660 CPL HATIBU NA
3. G9544 PC TTITO.
Inasemekana ni katika tukio la UVAMIZI WA BANK CRDB MBANDE mnamo saa 19:30HRS usiku na uku ikisemekana SMG moja wameondoka nayo majambazi hao.
Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa ni dereva. Majambazi hayakuingia ndani ya bank, uku Gari la Polisi aina ya (Leyland Ashok) likiharibiwa kwa risasi.
Habari kutoka katika ukurasa rasmi wa Instagram wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba amethibitisha kupoteza maisha kwa Askari Polisi Wanne na Raia wawili.
Mmoja wa majeruhi ni mfanyabiashara wa upande wa pili wa tawi la benki yalikotokea mauaji. Waziri awatembelea majeruhi na kusema wanaendelea vizuri.
Na Taarifa ya Kamanda Sirro kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi inasema hivi
Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa jumla ya askari wake wanne wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya majambazi kuvamia tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande, wilayani Temeke, Dar es Salaam.
Akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha Redio One Stereo leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema watu kadhaa wamekatawa na msako unaendelea ili kuwapata waliotekeleza unyama huo.
Sirro amesema taarifa kutoka eneo la tukio zinaonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na baada ya kufanya mauaji hao, walivamia kituo cha polisi cha Mbande kisha wakavunja stoo na kuchukua sare ya askari na silaha.
Akielezea namna tukio hilo lilivyotokea, Kamanda Sirro amesema wahalifu hao walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana lindo katika taasisi hiyo ya fedha na kuibuka ghafla na kuanza kurusha risasi.
Kwa mujibu wa Sirro, gari la polisi limechakazwa kwa risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia na ndiye aliyeweza kutoa taarifa na maelezo ya namna tukio lilivyofanyika.
“Watu kadhaa wamekamatwa na tunaendelea na msako. Tunawataka wakiwa hai au wafu,” amesema Kamanda Sirro huku akiwataka watu kujihadhari na yeyote anayejitambulisha kwao kuwa ni askari bila kuonesha kitambulisho.
Ameendelea kusema kuwa baada ya operesheni ya kukomesha mtandao wa wahalifu kama hao na wengine kukimbilia nchi jirani, masalia wameanza kujikusanya na kutekeleza matukio ya mauaji huku askari wakilengwa.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies