Wengi wetu tunapenda sana kunywa maji ya baridi hasa katika joto kali na maji haya ya baridi kwa wakazi wa jiji kama la Dar es Salaam ndio huona yanawafaa zaidi kutokana na joto linalopatikana kwenye jiji hilo.
Ni ukweli usiopingika kuwa unywaji maji ya baridi huleta faraja zaidi kwa mhusika, hivyo si jambo la kushangaza mtu kuhitaji maji ya namna hiyo kila mara baada ya mlo.
Licha ya kwamba maji ya baridi ni mazuri zaidi, lakini nayo yana madhara yake kiafya, moja ya madhara ya maji ya baridi ni pamoja na kudhorotoshe mfumo wa umeng'enyaji chakula tumboni.
Kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya lishe wanasema kwamba mtu anapokunywa maji ya baridi mara baada ya kula chakula, maji hayo huchangia kuganda kwa mafuta yaliyomo kwenye chakula.
Kutokana na kitendo hicho basi hupelekea usagaji wa chakula kwenda pole pole sana na hivyo huweza kumuingiza mhusika kwenye matatizo ya ukosefu wa choo 'constipation'.
Hata hivyo, imeonekana kisayansi kuwa kunywa maji ya baridi baada ya chakula ni hatari pia kwa afya ya moyo tumbo na mwili mzima kwa ujumla. Hivyo kama wewe ni mzoefu wa kutumia maji ya baridi ni vyema ukaanza kuepukana nayo taratibu kumbuka kwamba afya ya mwili wako hujengwa na unachokula na kunywa leo.