Habari za leo mpenzi msomaji wa tovuti yetu karibu katika muendelezo wetu wa kupeana taarifa mbalimbali kuhusu mimea tiba na afya kwa ujumla.
Ikiwa leo ni Jumatatu ya Oktoba 19, 2015 napenda tuzungumzie mapesheni, tunda hili mara nyingi wengi hupendelea zaidi kulitumia kwa kutengenezea juisi ili kuleta ladha nzuri zaidi na amahakika limekuwa likichangia kuleta ladha nzuri kwenye juisi.
Mmea wa mpesheni kwa kawaida hukuwa kwa kutambaa, hivyo katika ukuaji wake ni muhimu kuweka miti ili uweze kusaidia kukua vizuri.
Mapesheni yanasifika kwa kuwa na virutubisho bora kwa afya ya binadamu ikiwemo vitamin A, C, B2, B6, na E, flavonoids, pectin pamoja na madini ya chuma.
Aidha, mapesheni yanauwezo mzuri katika kupunguza maumivu ya mishipa ya fahamu na maumivu ya tumbo la hedhi, huku ikisaidia sana kutibu matatizo ya wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo na hali ya kuzubaa kwa wazee na watoto.
Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa, wajawazito na watoto wachanga wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotumia tunda hili, hii ni kutokana na katika majaribio ya utafiti huo walibaini matunda hayo yanauwezo wa kusababisha uchungu na kusababisha watoto kuzaliwa kabla ya wakati, lakini pia huweza kusababisha usingizi hivyo si vizuri kutumiwa na madereva.