Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
leo ni siku ya Jumapili nyingine tena napenda tufahamishane kuhusu hizi faida kadhaa za tende pamoja na umuhimu wake.
Tende ni tunda ambalo linaongoza kwa kuliwa sana katika kipindi cha mfungo na ndiyo tunda pengine kuliko tunda lingine.
Pamoja na kutumika sana katika kipindi hiko pia lina ladha nzuri mdomoni, huku likisheheni madini na vitamini lukuki na hivyo kuwa na faida nyingi kiafya.
Ulaji wa tendo humsaidia sana mhusika kupata kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili.
Pia ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo kumsaidia mhusika kuondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia.
Tende pia husaidia kuupatia nguvu mwili na kukuondoa uchovu, hii ni kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’.
Hali kadhalika tende ina madini aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini hayo husaidia kuimarisha mishipa ya fahamu.
Pamoja na hayo tende pia huwasaidia wale wenye matatizo ya ugonjwa wa anemia, (kupungukiwa damu) wanapotumia tende huweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi.
Tende vile vile huimarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).
Nachoweza kusema ni kwamba kuna faida nyingi za tende na unaweza kuila tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizi 10 na nyingine.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.
Share habari hii kadri uwezavyo.
Filed Under:
AFYA
on Sunday, November 22, 2015