Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MWENYEKITI NA KATIBU WA CCM WAJIUNGA NA CHADEMA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa huo, Isack Joseph, wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ole Nangole na Joseph walifikia uamuzi huo jijini hapa jana na kusema kwa nyakati tofauti wamelazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa utaratibu wa kumpata mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulikiukwa.

Kwa mujibu wa wana CCM hao, wakati wa mchakato huo baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho walikuwa na wagombea wao mifukoni waliotaka wagombee nafasi hiyo.

Ole Nangole aliyejiondoa CCM akiwa kwenye kipindi cha awamu ya pili cha uenyekiti wake, alisema alijiunga CCM mwaka 1977 ambapo alifanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali zikiwamo mwenyekiti wa CCM wilaya kwa miaka kumi.

“Ndugu zangu waandishi wa habari nimewaita leo kuwaambia jambo moja kwamba ninahama CCM kuanzia sasa. Najiuzulu nafasi yangu ya mwenyekiti niliyoitumikia kwa miaka saba na ninajiunga na Chadema kuanzia sasa.

“Nashindwa kuwa na moyo wa chuma wa kuendelea kuwa ndani ya CCM kwa sababu CCM niliyoifahamu tangu enzi za TANU siyo hii ya sasa.

“Kuondoka kwangu kumechangiwa na kikundi cha viongozi wachache kuiongoza CCM kwa mabavu, nguvu na kwa kutumia fedha walizokwapua serikalini.

“Miaka yote tangu nilipojiunga CCM mwaka 1977, sikuwahi kukiona chama hiki kikiendesha mambo yake bila kufuata kanuni na taratibu za vikao kama kilivyofanya wakati wa vikao vya kupitisha mgombea urais mjini Dodoma hivi karibuni.

“Mkutano mkuu wa CCM uliongozwa kwa kukiuka haki na misingi kwa wanachama kwani hata nyinyi mtakumbuka kulikuwa na mchakato wa urais na wagombea 40 walijitokeza akiwamo Edward Lowassa.

“Kwa mapenzi yake Lowassa alivyokitumikia chama na Taifa, wananchi tuliamini mchakato ule kama jina lake lisingekatwa angekuwa mmoja wa wagombea ambao wangefika mbali ndani ya chama.

“Lakini jina lake lilikatwa bila sababu japokuwa sababu tulizijua tangu alipotoka kwenye uwaziri mkuu kwa vile kuliendelea kusambazwa maneno na hujuma za kisiasa dhidi yake kupitia kwa viongozi wa chama na Serikali wakiwamo vijana wadogo waliopewa fedha na madaraka ili wamchafue,” alisema Ole Nangole.

Kwa upande wake, Joseph alimnyooshea kidole Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kumtaka achunge ulimi wake pindi anapowaita Watanzania makapi ndani ya nchi yao.

Joseph ambaye ni Diwani wa Kata ya Monduli Mjini aliyemaliza muda wake na kupita bila kupingwa ndani ya CCM, alisema hakuna Mtanzania aliye makapi kwani wote wana haki ya kidemokrasia ya kuhama vyama kwa jinsi watakavyoona inafaa.

“Watasema mengi na tumeondoka watatuita makapi. Naomba niwaambie, sisi siyo makapi, wakitaka tuzungumze suala la makapi hao wanaosema hivyo wao ndio makapi halisi.

“Sisi Watanzania si makapi kwani tukichambuana kwa suala la makapi na kuangalia wewe umetokea wapi, tutakwenda kusiko. Kwanza aliyesema hiyo kauli yeye ni Msomali. Hivyo tukisema nani ni makapi yeye ndiye makapi halisi anayeishi Tanzania kwani asili yake ni Somalia,” alisema Joseph.

Joseph alitoa kauli hiyo zikiwa ni siku chache baada ya Kinana kunukuliwa na vyombo vya habari akisema wanachama wa CCM wanaohamia Chadema ni makapi.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top