Idadi ya wahandisi waliosajiliwa nchini imeongezeka kutoka 6,868 na kufikia 15,364 katika kipindi cha miaka 10. Kati ya wahandisi hao 15,364, wahandisi wazalendo ni 13,901 na wa kigeni 1,463.Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi,
Steven Mrope, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam juzi.
Mhadisi Mrope alisema katika kipindi hicho, jumla ya kampuni za
ushauri wa kihandisi 279 zilisajiliwa na kati ya hizo, 201 ni ya
kizalendo na 78 za kigeni.
Aidha, alisema idadi ya wahandisi washauri ni 459 ambapo kati yao, 356 ni wazalendo na 103 wageni.
“Bodi imeendelea kutembelea na kukagua hali ya uhandisi katika
halmashauri zote Tanzania bara, ukaguzi huo umewezesha halmashauri
nyingi kutambua umuhimu wa kuajiri wahandisi na kuwatumia katika miradi
ya ujenzi,” alisema Mrope.
Alisema hiyo pia imewezesha idadi ya wahandisi katika halmashauri kuongezeka kutoka 129 mwaka 2003 hadi kufikia 508 mwaka 2015.
“Ingawa idadi hiyo ya wahandisi bado ni ndogo, lakini ni dhahiri ubora wa kazi katika halmashauri umeongezeka,” alisema.
Aliongeza kuwa Bodi imefanikiwa pia kuongeza idadi ya wahandisi
wataalam wanawake kutoka 20 waliosajiliwa mwaka 2011/12 hadi 80
waliosajiliwa mwaka 2013/14 mpaka kufikia 176 kwa sasa.
Aliongeza kuwa baada ya mabadiliko ya Sheria, Bodi imeanza kusajili
mafundi sanifu ambao ndiyo wasaidizi wakuu wa wahandisi na mpaka sasa
mafundi sanifu 157 wamesajiliwa. Mhandisi Mrope alisema moja ya majukumu ya Bodi ni uendelezaji wa
taaluma ya kihandisi ili kufanya wahandisi waende sambamba na mabadiliko
ya kisayansi na kiteknolojia.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies