Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, imemhukumu Ofisa
Mhifadhi Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Richard Nchasi,
kulipa faini ya Sh. 900,000 au kwenda jela miaka mitatu baada ya kukutwa
na makosa matatu.
Hukumu hiyo ilisomwa na Hakimu Mkazi, Juma Hassan, juzi baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia mshtakiwa hatiani kwa makosa hayo matatu.
“Kati ya makosa manne, mahakama
imemtia hatiani mshtakiwa kwa makosa matatu ya kutumia nyaraka kwa
lengo la kumdanganya mwajiri kwa kutoa hati za uwindaji wa wanyama,” Hakimu Hassan.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilisema upande wa Jamhuri umeshindwa
kuthibitisha shitaka la kuisababishia wizara hiyo hasara ya Dola 1,860
za Marekani (sawa na Sh. 2,976,000).
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies