Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye, wakati wasanii mbalimbali wakitumbuiza katika
uzinduzi huo, alikuwa aliwapiga vijembe vyama vinavyounda na Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwamba vimebeba makapi akidai kuwa wanadhani
watangia Ikulu.
Nape alikuwa akimaanisha makapi ni waliokuwa makada wa CCM ambao
wamekihama chama hicho kwa nyakati tofauti na kujiunga upinzani kama
Chadema, na NCCR- Mageuzi na CUF.
Miongoni mwa makada hao walitimkia Ukawa ni waliokuwa mawaziri wakuu,
Edward Lowassa (Chadema) na Frederick Sumaye (NCCR-Mageuzi).
Baada ya Lowassa kujiunga na Chadema, aliteuliwa kuwania urais
akiwalisha Ukawa wakati Sumaye juzi baada ya kuhama CCM alisema
amekwenda kuimarisha upinzani.
Naye Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Makongoro Nyerere,
aliponda makada wa CCM waliohamia upinzani wakiwamo Mawaziri Wakuu wa
zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye. ambaye aliwahi kuwa
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara tangu mwaka 2007 hadi 2012, alidai kuwa
Sumaye siyo mkweli kwani alipokuwa CCM alinukuliwa akisema iwapo chama
hicho kitamteua Lowassa kugombea urais kwa angekihama.
“Wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea urais Sumaye alisema hiki
chama mkimpa Lowassa, atahama chama kwa kuwa tunamweshimu Sumaye
hatukumpitisha Lowassa, lakini bado amehama na kwenda kumkumbatia
fisadi,” alisema.
Alisema pale ambako mtu hazumgumzi ukweli anaitwa mwongo, hivyo kauli
yake hiyo Sumaye hana tofauti na mwongo kwani katika kipindi cha miaka
kumi iliyopita aliingia katika kinyang’anyiro cha urais na alifika tano
bora, lakini kura hazikutosha badala yake zikatosha za Kikwete.
Alisema miaka kumi baadaye Sumaye ameingia katika kinyang’anyilo cha
urais bahati mbaya hakuingia katika tano bora, lakini cha kushangaza
anaanza kuishukutumu CCM kwamba ni chama kibaya
“Mnaufahamu mchezo wa chandimu, ambao huchezwa na vijana tu na mzee akiingia akija anataka nini?alihoji na kuongeza;
“Sumaye kaingia katika mchezo huu wa chandimu mwenyewe, tutamsema.”
Mbali na Sumaye na Lowassa, wapinzani wengine waliohama CCM na
kuiunga na upinzani ni wagunge waliomaliza muda wao wa Kahama, James
Lembeli; Viti Maalum, Ester Bulaya; Arumeru Magharibi, Ole Medeye;
Segerea, Dk. Makongoro Mahanga na wa Sikonge, Said Mkumba.
Wengine ni wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Arusha, Onesmo Ole Nangole;
Singida, Mgana Msindai na Shinyanga, Khamis Mgeja pamoja Mwenyekiti wa
zamani wa Dar es Salaam, John Guninita.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies