Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema Tanzania ya sasa inahitaji kiongozi mwadilifu, mzalendo na mchapakakazi kama alivyo mgombea wa CCM, Dk John Magufuli.
Jaji Warioba akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jana Dar
es Salaam, alisema Dk Magufuli ni mchapakazi kweli kweli na hana
masihara anapokuwa ofisini au nje ya ofisi.
“Wote mmemshuhudia akiwa Waziri
wa Maendeleo ya Uvuvi, Ardhi na sasa hivi Ujenzi, amekuwa mchapakazi na
amekuwa anawaelemisha wananchi wazifahamu haki zao,”Jaji Warioba.
Dk Warioba alisema wakati alipokuwa mwenyekiti wa Tume ya Rushwa
wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, alibaini kuwa sekta ya ujenzi
ilikuwa inaongoza kwa rushwa, lakini tangu Dk Magufuli apewe wizara hiyo
hakuna ufisadi tena.
Alisema kama Dk Magufuli angeamua kuchukua hata asilimia moja tu ya
ujenzi wa Daraja la Mkapa, Daraja la Malagarasi au Daraja la Kigamboni
angekuwa tajiri wa kutupa, lakini hakuwahi kujihusisha na vitendo hivyo
vya kifisadi na ndio maana hana utajiri wowote.
“Tumesikia ufisadi wa EPA,
Richmond, Escrow lakini hatujasikia ufisadi kwenye ujenzi na hii
inadhihirisha kuwa Dk Magufuli ni mwadilifu,”Jaji Warioba.
Jaji Warioba alisema mgombea huyo wa CCM ni mkali na hapendi kazi za ovyo ovyo, lakini pia anafuatilia kwa karibu.
Alisema chanzo cha ufisadi ni kutokana na viongozi kuwa karibu na matajiri, jambo ambalo mgombea huyo hana tabia hiyo.
Alisema mgombea huyo hana makundi badala ya
ke kundi lake ni
Watanzania wote hivyo akatoa mwito kwa Watanzania kumpa kura ili aweze
kuwaongoza Watanzania na kuwaletea maendeleo ya kweli.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies