Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imeweka historia na kujenga heshima ya taifa kwa kuweza kuandikisha
wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mfumo wa BVR kwa
mafanikio makubwa na kuyashangaza mataifa makubwa duniani.
Katika kufanikisha hilo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) vimetajwa kuwashawishi wanachama na wafuasi wake kwa kiwango kikubwa kujiandikisha katika BVR.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kufuatilia Masuala ya Uchaguzi Tanzania (TEMCO), ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Kufuatilia Masuala ya Uchaguzi, Dk Benson Banna, alisema Dar es Salaam jana kuwa Nec inastahili pongezi kubwa kwa hatua hiyo.
Alisema utafiti uliofanywa na Temco kwa kupitia vituo 8,398 vya
uandikishaji ambavyo ni asilimia 80.5 ya vituo vyote, umedhihirisha kuwa
kazi hiyo ilifanyika kwa ukamilifu kwa wananchi wengi kupata nafasi ya
kujiandikisha huku asilimia 64 ya vituo vikizidisha hadi muda wa kufunga
katika kuwawezesha wananchi kujiandikisha.
Kwa hatua hiyo, Dk Banna alisema NEC imefuta aibu kwa Taifa, kutokana
na mataifa mbalimbali ya nje kubeza uwezo wa nchi katika kufanikisha
uandikishaji huo kabla ya kuanza na kwamba sasa kama Taifa, Tanzania
imeanza kuonesha uwezo mkubwa wa kujitegemea katika uendeshaji wa
shughuli za uchaguzi.
“Hili lazima nilisema wazi, ni
aibu kwa mataifa makubwa kufadhili shughuli za uchaguzi maana kitendo
hicho ni hatari kwa nchi kuweza kujiamulia mambo yake na kukuza
demokrasia ya kweli, hivyo Nec wanastahili pongezi,” Dk Banna.
Akielezea mlolongo mzima wa uandikishaji, mwanazuoni huyo alisema,
Temco katika ufuatiliaji wake huo ilibaini kasoro mbalimbali ikiwemo
fedha kutolewa kidogo na kwa kuchelewa hatua iliyofanya tarehe ya kuanza
kwa uandikishaji kuchelewa na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Alisema pia wakati tathimini ya awali ilikuwa ni kuhitajika kwa
visanduku vya BVR zaidi ya 15, 000, serikali ilikataa pendekezo hilo na
kusema visanduku vinavyohitajika ni 14,000, lakini hata hivyo havikuweza
kununuliwa badala yake vilinunuliwa visanduku 8,000 tofauti na ushauri
wa Nec ambayo ilishauli kiwango cha chini kiwe visanduku 10,000