Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
upande wa Zanzibar, umesema unaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa CCM
Taifa, Jakaya Kikwete kwamba CCM imejiandaa kushinda na kushika dola kwa
sababu inao uzoefu wa kuongoza nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya UVCCM eneo
la Gymkanna mjini hapa, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Zanzibar, Shaka Hamdu
Shaka alisema hotuba iliyotolewa na Mwenyekiti huyo wa CCM wakati wa
kuwapokea wagombea wa chama hicho kuchukua fomu kutoka Tume ya Uchaguzi
NEC katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, imewavunja moyo wapinzani kwa
kiasi kikubwa.
Shaka alisema CCM haibabaishwi na uamuzi wa kuhama kwa waliokuwa
viongozi wake mbalimbali kwani tangu mwaka 1957 wakati wa harakati za
kudai uhuru viongozi wa vyama vya TANU na ASP walikuwa wakihama vyama hivyo na kwenda upinzani.
“Tunaipongeza hotuba ya
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewaambia ukweli wapinzani
kwamba CCM imejiandaa kushinda katika uchaguzi mkuu kwa sababu inao
viongozi safi wenye uwezo wa kuongoza dola,” alisema.
Aidha Shaka alitumia nafasi hiyo kusema kwamba UVCCM ipo imara huku
ikiwaunga mkono wagombea wa CCM wa nafasi mbali mbali ikiwemo ya urais
wa muungano.
Alisema umoja wa vijana katika mchakato wa wagombea wa nafasi ya
urais wa muungano haukuwa na mgombea unayemuunga mkono, isipokuwa
wanachama wenyewe walikuwa huru kutafuta mgombea wanayeona anafaa.
“Mchakato wa kuwania nafasi ya
urais wa muungano umemalizika na sasa tunaye mgombea John Magufuli na
mgombea mwenza Samia Suluhu. Hao ndiyo wagombea tunaowaunga mkono UVCCM
katika harakati za kuwania urais wa muungano,” alisema.
Alisema mgombea aliyepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM, John Magufuli
pamoja na mgombea mwenza Samia Suluhu ni viongozi wenye uwezo mkubwa wa
kuongoza nchi ambao walipata kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi