Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara),
hawajalipwa mishahara ya miezi mitatu kati ya miezi sita waliyokuwa
wakiidai mamlaka hiyo.
Wafanyakazi hao hawajalipwa mishahara ya Januari, Juni na Julai, mwaka huu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), Patrick Nyakeke, alisema baadhi ya wafanyakazi hawajalipwa mishahara ya kuanzia Januari hadi Mei, mwaka huu
“Wafanyakazi zaidi ya 1,500
bado hawajapewa mishahara ya miezi ya Januari, Juni na Julai huku
wengine wakiwa wanaudai uongozi wa Tazara mishahara ya miezi mitano
pamoja na malimbikizo mengine,” Nyakeke.
Aidha, alisema mishahara ya Januari na Juni, mwaka huu, utalipwa na
Menejimenti ya Tazara na wa Julai mwaka huu, unatarajiwa kulipwa kupitia
Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ya 2015/16 iliyotengwa na serikali.
Hata hivyo, alisema baada ya wafanyakazi kuuhoji uongozi wa mamlaka
hiyo kuhusu suala hilo, walielezwa kuwa watalipwa mishahara na
malimbikizo ya fedha za likizo kupitia makusanyo ya Tazara ya Januari
hadi Julai, mwaka huu.
Nyakeke alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo, serikali
imetenga Sh. bilioni 30 ili kuhakikisha wafanyakazi wanaondokana na adha
ya kusotea mishahara.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies