Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

TAKRIBANI WATU 100 WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA NDEGE

Takriban watu 100 wameuawa baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka mapema leo katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.

Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa tayari miili 49 imepatikana katika eneo la ajali.

Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.

Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules 130 ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 113 ilipoanguka. Tukio la ajali hii lilitokea siku ya jana mida ya mchana.

AMEAMUA KUVAA VIATU VYA KIKE LENGO NI KUTEST MAUMIVU YAO

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Brandon Cohen, mkazi wa mji wa Los Angeles huko Marekani ametoa kali ya mwaka baada ya kuamua kuvaa viatu vya kike ili kupima ni kiasi gani Wanawake wanapata maumivu wavaapo aina ya viatu hivyo.

Brandon Cohen aliamua kutenga siku maalumu kuvaa viatu hivyo vijulikanavyo kama High heels, baada ya kusikia malalamiko kwa wanawake wengi kwamba viatu hivyo vinawaumiza.

“Nilitaka kufahamu ni kwa nini Wanawake wengi wanalalamika kwamba viatu hivi vinawaumiza, na kwa nini sasa wanavivaa?”, alisema na kuhoji Brandon Cohen.

Bhuku akiwa amevaa viatu vya kike Brandon Cohen, siku hiyo aliavaa viatu hivyo na kuendelea na ratiba yake kama kawaida, ambapo alitoka kwenda kazini, kutembea mitaani, kuendesha gari na kwenda kwenye maduka mbalimbali ya shooping ambapo alipata changamoto ya watu wengi kumuangalia kwani ilionekana ni kitu cha ajabu kwa mwanaume kuvaa viatu vya kike.

“Changamoto nyingine niliyoipata ni kwamba kila nilipopita nilisikia minong’ono watu wakisema kwamba mimi ni shoga, kuna wakati nililazimika kuegesha gari mbali kidogo na maeneo ya maegesho ili kukwepa watu”, alisema Brandon Cohen.

Brandon Cohen alisema pamoja na yote hayo lakini aligundua kwamba wanawake wanapata maumivu makali sana wavaapo mavazi hayo, lakini wanapenda kuvaa viatu hivyo sababu wanapendeza na watu watu hupenda kuona wanawake wakiwa kwenye vazi la viatu hivyo.

“Siwezi kurudia kuvaa viatu hivyo tena kwani nimeumia sana, haya maumivu ni makali sana”, alimalizia Brandon Cohen ambaye alivaa viatu hivyo kwa saa 12 tu kwani maumivu yalimzidi.

HABARI ZOTE MUHIMU ZILIZOJIRI NCHINI TANZANIA LEO

MTANZANIA
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Katavi imemuhukumu mwalimu mstaafu wa shule ya msingi  Mpanda Ndogo , Rashid  Ndogo mwenye miaka 65 kifungo cha maisha jela baada ya kumbala mjuu wake wa miaka mitano na kumuharibu vibaya sehemu zake za siri.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili za mashtaka na utetezi.
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashtaka alidai mahakamani kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba mwaka jana majira ya saa 2 na nusu usiku nyumbani kwake katika kijiji cha Majalila.
Siku hiyo mshatakiwa alidaiwa kumbaka mjuu wake wakati amelala chumbani akiwa na mtoto wa mshtakiwa ambaye alishugudia baba yake akitenda kosa hilo la kinyama.
Siku ya tukio mke wa mshatakiwa alimwaga mume wake kuwa amekwenda kufunga zizi la mbuzi lililokuwa jirani na nyumbani kwao na mumewe kutumia mwanya huo kuingia chumbani kwa mjuu wake na kuanza kumbaka huku mwanaye akishuhudia.
Mshakiwa alikamatwa na majirani siku hiyo na kupelekwa kituo cha Polisi ambapo alifunguliwa mashtaka huku mjukuu wake akikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu.

MTANZANIA
Jeshi la Polisi Dar  limebaini mabaki ya mwili wa mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion, Anna Mizinga aliyeuawa Desemba mwaka jana na kutupwa kwenye shimo la choo cha shule yake.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema  mabaki ya mwili huo yalibainika Juni mwaka huu na tayari watu watatu wanashikiliwa na Polisi wakidaiwa kufanya unyama huo.
Akifafanua juu ya tukio hilo Kova alisema  Februari mwaka huu mtu mmoja alitoa taarifa polisi juu ya kupotea kwa mmiliki huyo tangu Desemba mwaka jana saa 11 jioni na hakuonekana tena.
Alisema mmiliki huyo alindoka nyumbani kwake na gari dogo aina ya Verosa akiwa na mtu mmoja ambaye naye ni miongoni mwa watuhumiwa wanaoshikiwa na jeshi hilo na abada ya taarifa hiyo walifungua jalada la uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.
Alisema mtuhumiwa wa kwanza alikamatwa Uchira, Moshi na kuwataja wenzake.

“Katika mahijiano mmoja alisema yeye na marehemu waliondoka hadi shuleni kwake na walipofika walivamiwa na watu wapatao wanne na kuanza kupigwa, lakini yeye alifanikiwa kutoroka na kujificha katika uzio wa shule, na aliwaona watu hao wakiendelea kumpiga mama huyo na kisha kumtupa katika shimo la choo kisha kutokomea na gari lake kusikojulika” Kova.

Watuhumiwa hao wanaendele kuhojiwa ili kupata undani wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo.

MTANZANIA
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amemaliza safari yake ya kusaka wadhamini katika Mikoa yote ya Tanzania na kujikusanyia zaidi ya wadhamini laki 8.
Lowassa alianza safari ya kusaka wadhamini Juni 4 baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na jana amehitimisha safari yake hiyo katika Mkoa wa Morogoro.

Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za CCM, kada anayewania kugombea Urais, anatakiwa kuwa na wanachama waliomdhamini 450 kutoka Mikoa 15 ikiwemo mitatu kutoka Zanzibar.

Katika baadhi ya Mikoa ambayo Lowassa alipata wadhamini wengi ni pamoja na Dar es salaam, Arusha, Morogoro, Pwani, Iringa, Mbeya, Ruvuma , Kilimanjaro, Tanga na Singida.

MWANANCHI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha kwa muda uandikishaji wa wapigakura katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani hadi hapo itakapotangazwa.
Uandikishaji huo unaofanywa kwa teknolojia inayochukua alama na taswira za mpigakura ‘Biometric Voters Registration’ (BVR)) ulipangwa kuanza Julai 4 hadi 16 kwa Dar es Salaam na Juni 25 kwa Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba alisema jana kuwa kazi hiyo imeahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa vinavyotumika kuandikisha wapigakura.
Alisema vifaa vilivyokuwa vinakusudiwa kutumika Dar es Salaam bado vinatumiwa katika mikoa ambayo wananchi wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.
“Mwitikio umekuwa mkubwa ndiyo maana tumeamua kusogeza mbele tarehe ili wamalizie huku tukiendelea kusubiri vifaa. Tunataka vikija tuishambulie Dar es Salaam kwa kipindi kifupi,”  Mallaba.

Mallaba alisema tarehe ya kuanza tena kwa kazi hiyo kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani itatangazwa na NEC baada ya kupata vifaa kutoka mikoa itakayokuwa imekamilisha uandikishaji.
“Ninaomba wananchi wafahamu kuwa mwezi uliokuwa umepangwa na NEC kukamilisha zoezi hilo utabaki kuwa Julai. Tarehe tu ndiyo itabadilika,” alisema na kusisitiza kuwa wanataka uandikishwaji kwa jiji hilo uwe wa kipekee ukiwa na vifaa vya kutosha kutokana na idadi kubwa ya watu. Aliwataka wananchi wote wa mikoa hiyo miwili kuwa watulivu wakati huu.
Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika alisema NEC imedhihirisha hoja aliyowahi kuitoa bungeni kwamba Bunge liahirishwe ili wajadili suala hilo kwa dharura.
“Kuna udhaifu mkubwa kwa upande wa NEC na Serikali kuhusu BVR… hata baada ya madai kwamba umerekebishwa lakini ukweli ni kwamba hali ni tete hata katika maeneo mengine ambayo uandikishaji unaendelea,” Mnyika.
Alieleza kuwa Dar es Salaam ndiyo itakayoamua mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kutoka na idadi kubwa ya wapigakura.
Alidai kwamba kubadilishwa huko kwa ratiba kutatoa mwanya kwa CCM ambayo ilishasema kupitia kwa Nape Nnauye kuwa inajiandaa kufunga goli la mkono kufanya hujuma.
bus
MWANANCHI
Mahakama ya Mkazi Kisutu jana ilishindwa kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa milioni 207 kutoka kwenye akaunti ya  madeni ya nje EPA kutokana na mshtakiwa wa tatu kulazwa katika hospitali ya Muhimbili, kitengo cha wagonjwa wa akili.
Hukumu ya kesi hiyo inayowakabiliwa makada watatu wa CCM, Rajabu Maranda na wenzake wanne, sasa itasomwa kesho kutokana na kulazwa kwa mtuhumiwa huyo, Iman Mwakosya ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha madeni ya nje cha benki kuu ya Tanzania.
Wengine kwenye jopo hilo ni Ignas Kitusi na Eva Nkya.
Mahakama itaandika barua kwa hospitali ya Muhimbili kabla ya Julai Mosi kwa ajili ya kupata taarifa kama mshtakiwa huyo anaweza kuelewa mwenendo wa kesi ili waweze kusoma hukumu.

NIPASHE
Magonjwa yasiyoambukiza yakiwamo ya kisukari, moyo na saratani, yanazidi kuongezeka kwa kasi na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha vifo duniani kote.
Aidha, inakadiriwa kuwa kisukari pekee kimeathiri maisha ya watu takribani milioni 371 duniani kote huku asilimia 80 ya idadi hiyo ikiishi katika nchi zenye uchumi wa kati na maskini.
Nchini Tanzania, takribani watu tisa kati 100 wana ugonjwa wa kisukari na kwamba mtu mzima mmoja kati ya watatu, ana tatizo la shinikizo la juu la damu.
Kaimu Mkurugenzi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Hauson Rweumbiza, alisema wakati wa semina ya siku moja iliyowashirikisha waandishi wa habari wa kutoka vyombo mbalimbali.
Lengo la semina hiyo lilikuwa ni kuzungumzia magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
Alisema gharama ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza duniani kote ni mabilioni ya dola na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa rasilimali finyu zilizopo.
“Kwa mwaka 2010, Shirika la Afya Duniani lilikadiria kuwa jumla ya gharama zinazohusiana na kisukari zilifikia Dola bilioni 378 duniani kote na kiasi hicho cha fedha kinaweza kufikia Dola bilioni 490 ifikapo mwaka 2030, alisema.
Naye Mratibu kutoka Taasisi ya Kisukari hapa nchini, John Gadina, alisema utafiti uliofanyika mwaka 2012, ulionyesha kuwa asilimia tisa ya Watanzania waligundulika kuwa na kisukari huku Wilaya ya Temeke ikiongoza.
Alisema ugonjwa huo umewakumba vijana na watu wenye umri mkubwa na kwamba serikali mpaka sasa imefikia kutoa huduma hiyo kwa asilimia 75 ambapo kila palipo na hospitali panakuwa na kitengo cha kutoa huduma za ugonjwa huo.
Alisema sababu ya Wilaya ya Temeke kuwa na wagonjwa wengi imetokana na ulaji kwa wingi wa vyakula vya nazi, chapati, wali pasipo kufanya mazoezi.

JAMBOLEO
Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii, kuwa kuanzia kesho na keshokutwa kutakuwa na uhaba wa mafuta kwenye vituo vya kuuza mafuta.
Kauli hiyo ya kukanusha imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage wakatia kijibu swali lililoulizwa na Job Ndugai jana Bungeni, Dodoma.
Ndugai alimtaka Waziri kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa ambazo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kaunzia kesho kutakua na tatizo la upatikanaji wa mafuta na kusababisha shughuli nyingi kusimama.
Mwijage alisema taarifa ambazo wanazo kama Wizara ni kuwa hifadhi ya mafuta ipo ya kutosha na kuwa uhaba wa mafuta hauwezi kutokea kwa kuwa wana uhakika kuwa mafuta yapo ya kutosha.
Alisema hata yeye ameonakwenye mitandao ya kijamii na sasa wanafuatilia ili kujuab chanzo cha taarifa hizo ni nini.
lisema iwapo kuna msambazaji au mfanyabiashara atajaribu kufanya hivyo kanuni kanuni na sheria zilizopo zitatumika kuhakikisha wahusika wanawajibishwa.

HABARILEO
Walimu wawili wapya wa Shule ya Msingi Sang’ang’a kata ya Pemba tarafa ya Inchugu wilayani Tarime, mkoani Mara wanashikiliwa nchini Kenya kwa kosa la kuingia nchini humo bila kuwa na kibali.
Walimu hao wawili ambao ni Ahedius Orio kutoka mkoa wa Kilimanjaro na mwenzake Elias Nandi kutoka Lindi wanashikiliwa na polisi nchini Kenya walipokwenda nchini humo kwa matembezi.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Sweetbard Njewike alithibitisha kukamatwa kwa walimu hao wawili wapya wa shule ya msingi Sang’ang’a iliyopo umbali wa kilometa moja kutoka mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Kamanda huyo alisema walimu hao katika kipindi hiki cha likizo, mwishoni mwa wiki waliamua kwenda kutembelea kijiji jirani cha Nyametaburo Kipimo ambacho kiko upande wa Kenya.
Alisema wakati wakiwa kijijini hapo walikutwa na Polisi wa nchi hiyo na kuwapeleka, kituo cha Polisi na Uhamiaji cha Isebania kuwahoji ambapo ilidaiwa waliingia nchini humo bila ya kufuata taratibu za kuwa na vibali vya kuingia nchini humo.
Tumewasiliana na wenzetu wa nchini Kenya ambapo wamedai kuwapeleka mahakamani kujibu shitaka la kuingia nchini humo bila vibali na wanatakiwa ndugu zao ama marafiki wakawadhamini huku juhudi za kuwasaidia walimu hao zinafanyika ili waweze kuachiliwa,Njewike.
Awali habari zilizotangazwa na vyombo vya habari vya Kenya, ikiwemo televisheni na redio za Citizen zilitangaza kuwa walimu hao walidaiwa kuwakusanya na kuwashawishi vijana wakiwemo kutoka Tanzania na Wakenya kujiunga na vikundi vya kigaidi vya al Shabaab.

MUSTAFA COLONEL ACHUKUA HEADLINE MITANDAO

Baada ya video kama za ‘Nishike’ ya Sauti Sol na ‘You guy’ ya P Unit kufungiwa, headlines za sasa zimeangukia kwa Mustafa Colonel ambaye ni siku za karibuni tu alishikwa na Polisi kwa madai kuwa kwenye hii video kuna Mwanamke ambaye ni nyumba ndogo ya kigogo flani hivyo picha alizopigwa hazitakiwi kuvuja.
 Colonel
Baada ya hayo video ilipotoka kwa ubishi bila picha kufutwa, imefungiwa kuonyeshwa kwenye TV za Kenya kwa sababu imevuka mipaka ya kuzingatia maadili.

PICHA ZA GARI JIPYA LA KIFAHARI KUTENGENEZWA AFRICA

150629164316_kantanka_640x360_bbc_nocredit
Ukipita barabarani ni kawaida kukutana na majina ya magari yaliyozoeleka kama Toyota, BMW, Benz, Suzuki, Honda… Hayo yote ni magari ambayo viwanda vyake viko nje ya Africa.
150629164416_kantanka_640x360_bbc_nocredit
Lakini ninayo good news kwamba huenda tukakutana na brand za magari yanayozalishwa hapahapa Afrika na ni magari ya kifahari kabisa ambayo unaweza kufananisha na Benz na BMW!

150629164510_kantanka_640x360_bbc_nocredit
Gari hii imetengenezwa Ghana, inaitwa Kantanka 4×4.. pichaz zake kuanzia inavyoanza kutengenezwa mpaka ilivyokamilika ziko hapa.

150629164138_kantanka_640x360_bbc_nocredit
150629164230_kantanka_640x360_bbc_nocredit
_83931119_83931118
Kan
Bei ya hii gari ni kama Pound 14,000 (Ukiileta kwenye Tshs. ni Milioni 43)

WATU 16 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA MLIPUKO NDANI YA MSIKITI

Mlipuko mkubwa uliotokea ndani ya msikiti wa Al-Sadeq jijini Kuweit nchini Kuweit wakati wa swala ya Ijumaa wiki iliyopita ulisababisha watu 16 kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye tukio hilo.
Innalillahi wainnailaihi raj'uun
Tumuombe Mwenyezi Mungu awajaalie wale wote waliopoteza maisha katika kadhia hii waingie peponi IN SHA ALLAH, tuseme amiin.

MAKAMU WA RAIS NCHINI BURUNDI ATOWEKA NCHINI KWAKE

Wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu hatma ya uchaguzi mkuu wa Burundi unaotarajia kufanyika mwezi ujao kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea kupinga kugombea tena kwa Rais Pierre Nkurunziza..headlines zimerudi tena nchini humo.

Makamu wa Rais wa nchini hiyo Gervais Rufyikiri ametoroka nchini humo na kudaiwa kimbilia Ubelgiji  baada ya kupinga hatua ya Rais wa nchi hiyo kuwania muhula wa tatu akiungana na makamishna wa tume huru ya uchaguzi na jaji mmoja wa mahakama ya kikatiba.

Licha ya msemaji wa serikali kukanusha madai hayo na kusema kuwa Rufyikiri amesafiri nje kwa ziara rasmi ya kikazi lakini mwenyewe baada ya kuhojiwa na Televisheni ya France24 amesema ameondoka baada ya kuhofia maisha yake kufuatia kumpiga Rais huyo kuwania kwa muhula wa tatu ambapo ni kinyume na sheria.

Burundi imeingia katika mgogoro wa kisiasa tangu rais Nkurunziza atangaze nia ya kuwania muhula wa tatu kuongoza nchi hiyo huku maelfu ya watu wakikimbia nchi hiyo kwa kuhofia maisha yao.

BREAKING NEWS: MAJAMBAZI YAVAMIA NA KUPORA TAWI LA NMB MKURANGA

Benki ya NMB Tawi la Mkuranga Limevamiwa na majambazi na kupora fedha nyingi ambazo zilikuwa zimefikishwa kwenye benki hiyo na gari maalum.

Bado hatuna thamani halisi ya pesa zilizoporwa kwa maana watu ni wengi na kila mmoja anaongea lake, huku wengi wao wakiwalaumu maaskari kwa kuwa tukio hilo limetumia zaidi ya nusu saa.

MALIKI MARUPU ADHAMINIWA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU

Marupu adhaminiwa na wanafunzi
Katika hatua nyingine, mgombea mwingine, Maliki Marupu amesema amelazimika kutumia mkoa maalumu wa vyuo vikuu kupata wadhamini ili kukwepa changamoto ya fedha za kuzunguka katika mikoa mbalimbali.

Marupu ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu Mzumbe alilieleza Mwananchi jana kuwa anatarajia kukamilisha idadi ya wadhamini 450 kwenye Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro.

Alipoulizwa kama haoni kuwa kwa kutumia mkoa huo wa vyuo vikuu pekee atakuwa amekosa sifa kwa kushindwa kutembelea mikoa mingine 14 zaidi inayotakiwa, Marupu alisema hata hao wanafunzi wanaunda mkoa wa vyuo vikuu kuna mikoa yanayotoka, hivyo haoni shida kumdhamini.

Marupu, mwenye umri wa miaka 34, alisema endapo angefuata mikoa ya kijiografia ingekuwa shida kwake kutokana na kukosa fedha.

Alisema katika mzunguko wake alipata changamoto za watu walioko katika ofisi za wilaya wakisubiri kudhamini wagombea kwa malipo ya Sh20,000 au 30,000, hivyo akaamua kuwakwepa na kudhaminiwa na wanafunzi wenzake.

Mwanafunzi huyo alisema licha ya kukamilisha idadi ya wadhamini, atakwenda nyumbani kwao Ukerewe kutafuta baraka za wazee kabla ya kuwasilisha fomu zake Dodoma.

Makada nane warejesha fomu
Jumla ya makada wanane wamerudisha fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais, huku Boniface Ndengo akisema amekumbana na tatizo la kuombwa fedha na wanachama kwa ajili ya wamdhamini.

Wengine waliorejesha fomu jana ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani.

Akizungumza mjini hapa mara baada ya kurejesha fomu hizo, Ndonge alisema katika mchakato wa kukusanya wadhamini amebaini wananchi wa kawaida nao ni zao la rushwa.

“Unafika mahali wananchi wanakataa kukudhamini kwa sababu hauna pesa ya kuwapa. Mimi niliwaambia sina fedha ila ninataka kuwatumikia. Waliniambia mbona fulani katoa kiasi fulani wewe hutoi,”alisema.

Alilalamikia makada wenzie waliochukua fomu kuandikwa mara nyingi katika vyombo vya habari na wengine kutopewa nafasi. Ndonge alisema alifanikiwa kupata wadhamini 602 katika mikoa 20 aliyoenda.

Katika hatua nyingine, Waziri Chikawe aliwaomba msamaha waandishi wa habari kuwa hataweza kuzungumza nao kutokana na kukimbilia majukumu mengine.

Kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho mwisho wa kuchukua fomu na kurudisha ni Julai 2 saa 10:00 jioni. Kazi hiyo ilianza Juni 3.

EDWARD LOWASSA AVUNJA REKODI MKOANI ARUSHA APATA WADHAMINI KIBAO

Lowassa avunja rekodi
Mkoani Arusha, Edward Lowasa ameendelea kuvunja rekodi ya idadi ya watu wanaojitokeza kumdhamnini baada ya kupata wadhamini 120,392 jana.

Rekodi hiyo ya Arusha imezipiku ile iliyowekwa na mkoa ya Iringa alikodhaminiwa na wanachama 58,562.

Mbunge huyo wa Monduli aliwasili jijini Arusha saa 9:00 alasiri na kupokelewa kwa mbwembwe zilizoambatana na nyimbo mbalimbali za wasanii kadhaa nchini. Lowassa aliongozana na mkewe Regina na viongozi kadhaa wa CCM.

Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Lowassa alifanyiwa maombi rasmi na wazee wa kimila wa jamii ya Wamaasai, maarufu kama Malwaigwana.

Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha, Isaack Joseph alisema waliomdhamini waziri huyo mkuu wa zamani ni wanachama hai kutoka wilaya zote saba za kichama mkoani Arusha.

Kwa CCM, mkoa wa Arusha una wilaya za Arusha Mjini, Karatu, Longido, Monduli, Ngorongoro, Arumeru Mashariki na Arumeru Magharibi.

KAMPUNI YA EXCELLENTCOM TANZANIA LIMITED YATELEKEZA MINARA 292

Minara 292 ya mawasiliano iliyojengwa na Kampuni ya Simu ya Excellentcom Tanzania mwaka 2008, imetelekezwa bila kutoa huduma yoyote, JAMHURI linaripoti.

Baada ya kuitelekeza kwenye viwanja ambavyo baadhi vina makazi ya wamiliki wa ardhi hiyo, kumefanya kampuni hiyo sasa kudaiwa mamilioni ya shilingi ya kodi za pango la eneo.

Kampuni ya Excellentcom Tanzania Limited ilisajiliwa kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Septemba 13, 2006 ikiwa na wanahisa wawili — Jitco Limited ikiwa na hisa 3,500 na Excellentcom Systems hisa 6,500.

Mara baada ya kusajiliwa, kampuni hiyo ilianza mchakato wa kusimika minara yake ya mawasiliano mwaka 2008 kwa kuingia mikataba ya pango na wananchi wanaomiliki maeneo ambayo minara hiyo imejengwa, lakini imeshindwa kutimiza masharti ya mikataba hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika ambazo JAMHURI imezipata, Excellentcom kwa sasa imeshindwa kuiendeleza sambamba na kulipa kodi za pango kulingana na mikataba hiyo na kufunguliwa kesi za madai na wananchi hao.

Helena Mafita, mkazi wa Mtaa wa Litapwasi, Chang’ombe Uwanja wa Taifa, Temeke jijini Dar es Salaam anasema kwamba kwa sasa hakuna walinzi wanaolinda minara hiyo iliyojengewa mitambo pamoja na jenereta kubwa.

Nyumbani kwa Helena mitambo hiyo imefungwa kwenye pointi ya longitudo nyuzi 039.26935 latitudo nyuzi 06.85363 kiwanja namba 28 ambako aliingia mkataba wa kampuni hiyo kwa miaka 20 kuanzia Agosti 15, mwaka 2008.

Katika mkataba huo ambao Helena alikuwa analipwa Sh 300,000 kwa mwezi ungefika ukomo Agosti 14, 2028. Helena anadai kuwa hajalipwa na kampuni hiyo tangu mwaka 2010 na kila anapofuatilia ofisi za Excellentcom, Mikocheni, hafanikiwi kuwaona wahusika baada ya kuelezwa kuwa “ofisi hiyo haipo kwa sasa hapo.”

Hali hiyo ilimfanya Helena aende kwa wanasheria ili kufuatilia haki (pango) yake kwa njia ya mkondo wa sheria ambako sasa amewakodi mawakili wa Kampuni ya CERW. Katika barua hiyo ya Novemba 18, 2013 yenye Kumb. Na. CERW-ADV/HELENA/2013/01, mawakili hao waliandika,

“Tumeelezwa na mteja wetu Helena Mafita, ulipojengwa mnara wa mawasiliano ya simu Dar 134 kwamba umechelewesha malipo ya kodi hadi Oktoba 19, 2010. Alikuwa anakudai limbikizo la Sh. 7,800,000 kwa mnara wa mawasiliano,”

inasema sehemu ya barua ya mawakili hao iliyosainiwa na C.E.R. William, ambayo gazeti hili imeona nakala yake. 

Wakili William, anayemtetea Helena, anasema pia mteja wake aliamini kwamba angelipwa deni lake mara baada ya kampuni hiyo kumwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Jitco na Excellentcom, lakini deni lake halikulipwa na hakuna kinachoendelea hadi sasa.

Anasema kwa sasa deni hilo limeongezeka na kufikia zaidi ya Sh. 14 milioni ikijumuishwa na deni la nyuma na wanahisa hao hawajalipa na kuzidi kumletea usumbufu mdai huyo.

Wakili William anaeleza kusikitishwa kwake akisema kitendo hicho cha kutolipwa mteja wake na kuwaondoa walinzi bila kuwapa taarifa yoyote “si (kitendo) cha kiungwana kwa kuwa wameamua kukaa kimya na kukiuka makubaliano ya mkataba kama unavyosema. 

“Mteja wetu ametuelekeza tukuandikie barua hii kuutaka uongozi wa kampuni umlipe malimbikizo yake kwa haraka na Sh. milioni 10 ikiwa ni gharama za usumbufu wa kimwili na kisaikolojia alioupata kwa mshtuko kwa kutokulipwa deni lake hadi sasa,”

inasema sehemu ya barua hiyo. Anasema, barua hiyo kwa uongozi wa kampuni hiyo ya simu, ilitoa notisi ya siku 30 tangu tarehe iliyoandikwa kulipa deni hilo kwa mteja wao, sambamba na gharama za usumbufu na kwamba iwapo watakaidi kufanya hivyo wameelekezwa kufungua madai dhidi ya wahusika na matokeo yake hakuna utekelezaji wowote.
Mbali ya Helena, mtu mwingine aliyeilalamikia Kampuni ya Excellentcom ni Stephen Mafuru ambaye amefungiwa mitambo hiyo ya mawasiliano nyumbani kwake kiwanja Na. 5 kilichopo mtaa wa Maili Sita, Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Mtambo huo umefungwa Longitudo nyuzi 37.27111 na Latitudo nyuzi 03.32786. Katika mnara huo uliojengwa kwenye ukumbi wa mita 15 za mraba, Mafuru anasema kwamba mara ya mwisho kulipwa fedha ilikuwa ni 2011 kiasi cha Sh milioni 4.8

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, alipoulizwa kama anafahamu taarifa za Kampuni ya Excellentcom iliyotelekeza mitambo yake na kushindwa kulipa kodi ya pango kwa wateja walioingia nayo mikataba, anasema wao hawahusiki na minara ya kampuni nyingine na kwamba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wanaweza kuwa na majibu sahihi.

Naye Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Innocent Mungy, alipolizwa na JAMHURI kuhusu Kampuni ya Simu ya Excellentcom anasema walitoa matangazo muda mrefu kwamba hawana leseni kutoka Mamlaka hiyo.

Anasema suala la kujenga miundombinu ya kampuni za simu katika maeneo mbalimbali liko chini ya halmashauri za miji au majiji inapojengwa minara hiyo, kulingana na utafiti wa kitaalamu wa kampuni husika. 

KIJANA MMOJA AKATWA MKONO KISA ASITUMIE MITANDAO YA KIJAMII

Matumizi ya mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram ni kitu ambacho kimeshika chati sana kwa sasa duniani, vijana wameonekana kuwa waathirika wakubwa wa matumizi ya mitandao hii.

Kijana Little Wang ambaye umri wake ni miaka 19 huko China aliona njia pekee ya kukomesha tabia yake ya kupenda kutumia laptop na simu kuingia mtandaoni ni kujikata mkono wake, alipoona hali haimwendei sawa aliita taxi impeleke Hospitali ambapo hakuna aliyejua kinachoendelea nyumbani kwao, aliacha ujumbe kwamba ametoka kwenda Hospitali na angerudi muda mfupi baadaye.

Madaktari walimfanyia operation kuunga mkono huo huku wakiwa na matumaini kwamba baadae utaweza kufanya kazi kama ilivyokuwa mara ya kwanza kabla hajaukata. 
Mama yake Little alisononeshwa na kitendo hiki na kusema hakutegemea mtoto wake angeweza kujifanyia ukatili wa aina hii.

SERIKALI YA MAREKANI YATOA DOLA BILION 30 KWA AJILI YA KUTUNZA MAZINGIRA

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya dola Bilioni 30 kwa ajili ya Kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini.

Hafla ya kutiliana saini ilifanyika jana, Seronela mkoani Arusha ambapo waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress walisaini makubaliano ya dola 2milioni kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya ujangili n anyingine milioni 14.5 kwa ajili ya uhifadhi.

Balozi huyo wa Marekani Mark Childress, alimwelezea Nyalandu, kuwa ni mwanasiasa jasiri na makini asiyeogopa kusema ukweli hata kama unaumiza.

Balozi Childress amesema waziri huyo ni tofauti na wanasiasa wengine na kwamba, ujasiri wake katika utendaji unapaswa kuungwa mkono. Kauli ya Balozi huyo imetokana na uamuzi wa Nyalandu kuweka hadharani idadi ya tembo waliopo nchini na kueleza bayana kuwa, tatizo hilo bado ni janga kwa taifa. 

“Kwa mwanasiasa mwingine ingekuwa ngumu kutoa taarifa kama ile kwani angeona anajimaliza lakini alilazimika kufanya hivyo ili njia za kutokomeza tatizo hilo ipatikane na sasa marafiki wa uhifadhi tumeamua tupambane pamoja kulaliza tatizo hili”. 

Pia, katika taarifa yake Nyalandu hakusita kueleza kutoweka kwa tembo 10,000 ambao hawakuweza kuonekana wakati wa sensa ya mwaka 2014 iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa.

Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano na uzinduzi wa mradi mkubwa wa kulinda mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini wa PROJECT, ambapo serikali ya Marekani imetoa zaidi ya sh. Bilioni 31 katika utekelezaji wa mradi huo. 

Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Treetops iliyopo ndani ya eneo la Hifadhi ya Wanyamapori inayosimamiwa na jamii (WMA) kwenye Hifadhi ya Taifa ya Tarangire. 

WAZEE WASHUTUSHWA NA MPANGO WA MKUBWA JUU YA KUBEBA RAWAMA 2015

Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM linaundwa na wajumbe sita ambao ni wenyeviti na makamu wenyeviti wastaafu Taifa wa chama hicho.

Nao ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (Mwenyekiti), Makamu Mwenyekiti mstaafu (Tanzania Bara), Pius Msekwa (Katibu); Benjamin Mkapa (Mjumbe); Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume; Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour; na Waziri Mkuu mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), John Malecela.

Habari kutoka vyanzo vya kuaminika zinasema Katibu wa Baraza hilo, Pius Msekwa, tayari ameshaandika barua kwenda kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajab Luhwavi, akimtaka aitishe kikao cha Baraza hilo.

Kwa maelekezo hayo, Baraza la Ushauri la Wazee linatarajiwa kuketi wiki hii, Juni 25. Kwa maelekezo ya Msekwa, waalikwa kwenye kikao hicho, ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Dk. Edward Hoseah, na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman.

Haijajulikana sababu za kualikwa kwa wakurugenzi hao wanaoongoza taasisi nyeti, lakini kuna tetesi kwamba watatakiwa kutoa maelezo, na hata kuthibitisha, tuhuma za kuwapo vitendo vya rushwa miongoni mwa wagombea; huku mlengwa mkuu akibaki kuwa Lowassa.

Kufanyika kwa kikao hicho cha keshokutwa kumekuja baada ya kikao cha awali cha Baraza hilo kugubikwa na utata; hasa baada ya baadhi ya wajumbe kuona mtu aliyekamiwa ni Lowassa.

Kikao cha awali kikiwa na wajumbe watatu pekee, kiliandaa “Tamko la Wazee”; lakini baadaye likawekwa kapuni baada ya mjumbe mmoja kuwasili na kutoa hoja za kutokubaliana na uamuzi huo.

Hoja kubwa ilikuwa kwamba tamko kama hilo lingekuwa na maana zaidi endapo lingekuwa limetolewa na wajumbe wote wanaounda Baraza hilo.

Msukumo wa Mwenyekiti Rais Kikwete Duru za uchunguzi zinaonesha kuwa Mwenyekiti Rais Kikwete, kwa makusudi, amenuia kuwatumia wazee hao kutoa tamko ambalo atalitumia kama ngao kumng’oa Lowassa na wagombea wengine wanaotajwa kuwa ni hatari kwa umoja na mshikamano wa chama.

Inaelezwa kwamba Rais Kikwete anaona itakuwa kazi ngumu na ya lawama kwake, kuongoza mpango wa kulikata jina la Lowassa; hasa kutokana na urafiki wao wa siku nyingi, na hofu ya kisasi endapo mbunge huyo wa Monduli atakuwa rais.

“Anachofanya mwenyekiti ni kuhakikisha anatumia ‘ushauri’ wa wazee kama ngao atakayoitumia kwenye vikao vya CC na NEC kumkata Lowassa,” kimesema chanzo chetu. Chanzo hicho kimeongeza kwamba kwa bahati nzuri wazee wameshang’amua mpango huo, na ndiyo maana kikao cha awali hakikutoka na tamko la moja kwa moja ambalo Msekwa na Malecela walikamia litolewe kwa umma. 

Inaelezwa kuwa mbinu nyingine inayokwenda sambamba na mpango huo ni hii ya kuwapo utitiri wa wagombea urais. “Hawa wagombea urais hujiulizi kwa nini mwaka huu wamekuwa wengi? Iweje wanachama 40 au zaidi wajitokeze kuwania nafasi hii?

“Hili limewezekana kwa sababu kumewekwa mapandikizi. Ndiyo maana unaona wapo wanaotangaza nia hawazunguki mikoani kusaka wadhamini, lakini baada ya siku chache utasikia wanarejesha fomu.

Hao wanatafutiwa wadhamini na vyombo maalum,” kimesema chanzo chetu. Kwenye mpango huo, imekusudiwa kuwa majina mengi ya wagombea “wa kweli” yatakatwa pamoja na yale ya mapandikizi, na mwishowe watakaolalamika ni wagombea “wa kweli”, akiwamo Lowassa.

“Watafanya hivyo ili Lowassa akilalamika, aulizwe ‘mbona wengine waliokatwa hawalalamiki, iweje wewe tu ndiye ulalamike’. Ataulizwa, hivyo na mwisho itaonekana yeye ndiye mwenye nongwa,” kimesema chanzo chetu.

Wakuu wa vyombo vya usalama walioitwa kazi yao kubwa wanayotarajiwa kuifanya ni kuanika “madudu” ya wagombea wote, lakini jicho la pekee likielekezwa kwa Lowassa.

Mnyukano ndani ya Baraza la Wazee Mnyukano ndani ya Baraza la Wazee ni jambo lililo wazi. Dk. Salmin amekuwa hahudhurii vikao hivyo kutokana na kudhoofu kwa afya yake.

Malecela anatajwa kuongoza mashambulizi dhidi ya Lowassa, ukweli ambao unathibitishwa na kauli zake za mwaka jana pale alipoita waandishi wa habari na kumpongeza Paul Makonda, kwa kitendo chake cha kumtukana Lowassa.

Hata hivyo, baadhi ya mambo yenye kuzua utata ni kumuona Malecela akishiriki vikao vya Baraza la Ushauri la Wazee kujadili wagombea, akiwamo mtoto wake, Dk. Mwele Malecela, ambaye ni miongoni mwa waliochukua fomu kuwania urais. 

Dk. Mwele ni miongoni mwa wanaodhaniwa kuwa hawana nia ya dhati ya kuwania urais, lakini yupo ili jina lake likiondolewa, basi Malecela aweze kusema: “Lowassa analalamika nini, mbona hata mimi mtoto wangu jina lake limekatwa”.

“Mzee Malecela hawezi kutenda haki kwa wagombea wengine. Huwezi kutarajia asifu wagombea wengine zaidi ya mtoto wake. Lakini ni huyu huyu ambaye ameshaonesha msimamo mkali dhidi ya wagombea wengine, hasa Lowassa.

Kiungwana ilitakiwa asihudhurie kikao hiki kinachokuja,” kimesema chanzo chetu. Kwa upande wake, Mzee Mwinyi anaonekana kutokuwa na uamuzi wa moja kwa moja. Mara zote amekuwa akiwasikiliza wajumbe kabla ya kufikia uamuzi.

Wanatoa mfano wa kikao kilichopita ambako wazee wawili hawakudhuria, na wa nne alipoingia ukumbini akakuta tayari limeshaandaliwa tamko la kulaani “matumizi ya fedha na rushwa” ambalo kimsingi lilimlenga Lowassa.

Hata hivyo, mmoja wa wazee alipinga mpango huo akisema ilikuwa vyema wajumbe wote, hasa wanaoonekana kuutaka urais kwa dhati, wakajadiliwa taarifa zao.

Hofu ya mzee huyo ilikuwa kwamba kutamka tu fulani ni mtoa rushwa bila kuwa na maelezo ya kujitosheleza, ni sawa na kufanya kazi kama ya magazeti ambayo yamekuwa yakiimba wimbo huo huo bila ushahidi wa moja kwa moja.

“Sisi hatuwezi kufanya kazi kama magazeti yanavyofanya. Tutoe tamko linalofanana na yanayoandikwa kwenye magazeti? Nadhani si vizuri,” amekaririwa mmoja wa wazee hao akiwaeleza wenzake.

Wakati Lowassa akiandamwa, habari zilizo wazi zinaonesha kuwa karibu watia nia wote wamekuwa wakigawa fedha kwa wanachama wanaowadhamini huko mikoani na hata kuwalipa waendesha bodaboda.

Rais mstaafu Karume hakuhudhuria kikao kilichopita. Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na wasaidizi wake zimesema atafanya kila analoweza ili ahudhurie kikao cha Juni 25.

Wazee wanaotajwa kuwa wako mbele kubeba ajenda ya Rais Kikwete ya kumng’oa Lowassa ni Malecela na Msekwa. Wakati Rais Kikwete akipambana kuhakikisha wazee wanakuwa kivuli cha kumwezesha kuchukua “uamuzi mgumu”, 

Taarifa za awali zinasema baadhi ya wazee hao wanapendekeza wagombea urais waachwe wapambane ili hatimaye kura ziamue mshindi. 

Wanaitilia mkazo hoja hiyo kwa kigezo kuwa Sekretarieti na Kamati ya Maadili ya CCM zilichelewa kuwachukulia hatua baadhi ya wanachama tangu mwaka 2010.

Wanaamini kuwa idadi kubwa ya waomba urais wana dosari ambazo kama chama kitasimama kwenye misingi iliyozoeleka ya kuwapata wagombea wake, wengi watakosa sifa.

Watu walio karibu na Rais Kikwete wanasema hata yeye alidhani njia hiyo ingekuwa sahihi, lakini hofu yake ni kwamba kufanya hivyo maana yake ni kumwambia Lowassa ajiandae kuapishwa.

“Mwenyekiti hataki lawama. Aliona kukwepa lawama njia ya kuwaacha washindane kwa kura ingekuwa nzuri. “Lakini baadaye akaja na wazo la kulitumia Baraza la Ushauri akiamini watatoa tamko ambalo maudhui yake yatakuwa yamemlenga moja kwa moja Lowassa, na wahakikishe linasambazwa kwenye vyombo vya habari.

“Anaamini kwa kufanya hivyo kazi yake itakuwa nyepesi. Atatumia hoja ya ‘wazee wameshauri’ ili kumdhibiti Lowassa. Hapo atakuwa amefanikiwa mambo makuu mawili, kwanza ni kumpata rais anayemtaka, na pili ni kukwepa lawama.

Hii ndiyo sayansi itakayotumika. “Mambo yakienda kama ilivyokusudiwa, keshokutwa (baada ya kikao cha Baraza la Wazee) utasikia ‘kauli ya wazee’ ambayo mlengwa ni Lowassa,” kimesema chanzo chetu.

Chanzo hicho kinasema kwamba wazee wameshautambua mpango wa Rais Kikwete wa wao kutumika kubeba lawama, na kwa maana hiyo inawezekana kukawapo ugumu wa kutolewa kwa tamko lililoridhiwa na wazee wote. 

KENYA YAZINDUA ATM ZA MAJI SOMA ZAIDI KUPITIA HAPA LEO

Wananchi wa Kenya sasa wataweza kununua maji safi na salama kwa kutumia kadi maalum kupitia mitambo kama ya ATM.

Kwa muda mrefu wananchi wa Kenya walikuwa wakitegemea maji kutoka kwa wachotaji binafsi ambayo uhakika wake wa usafi na usalama haukuwa na hakika.

Wananchi wanaweza kununua lita ishirini kwa senti hamsini. Mitambo minne imewekwa katika maeneo tofauti jijini Nairobi.

HABARI NJEMA KWA WAPENDA MAENDELEO KUTOKA AIRTEL FULSA

Hii ni nafasi nzuri  ya kuleta mabadiliko, kuhamasisha vijana na kuwasaidia kujijenga kibiashara endelevu na ninapenda kuwapongeza Airtel kwa ajili ya mpango huu," alisema Mulamula.

Bwana Mulamula aliahidi kufanya kazi kwa karibu na Airtel pamoja na jopo la washauri  katika kuhakikisha wanachagua na kuwapa mafunzo walengwa wa Airtel Fursa  ikiwa ni pamoja na kuwasaidia  kuweza kutumia techonologia ya habari yaani ICT kama nyenzo  muhimu itakayowawezesha kuleta ufanisi katika shughuli zao za uzalishaji na kiuchumi. 

Akiamini kuwa vijana watakaofaidiaka na Airtel fulsa watahamasisha na kuongoza katika kuleta mabadiiko kwenye jamii zao huku akihakikisha mpango huu unakuwa na mafanikio makubwa kwa walengwa  na kuwa na mvuto kwa vijana wengine .

Mhandisi Mulamula ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama (ICT) Business Incubator (DTBi) kwa ajili ya ujasiriamali katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), analeta uzoefu wa kutosha katika mpango huu  wa Airtel fursa kwenye nyanja ya  ujasiriamali na kukuza biashara zinazoanza.

Yeye ni mshauri na mwalimu kwa wajasiriamali. Amekuwa akisaidia kuinua vipaji vya watu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na katika mkutano wa kimataifa wa ujasiriamali nchini Moscow, Durban na Nairobi kwa ajili ya maonyesho ya Afrika.

Pia ni Mjumbe wa Bodi ya Demeter nchini Boston USA na pia Mjumbe wa Bodi ya XPrize nje ya California, Marekani.

“Mpango huu unatafuta vijana wenye kiu, nguvu na utayari wakupata wanachokiamini na kukihitaji, wenye uwezo wa kuzipitia changamoto na kufikia matarajio waliojiwekea na wakati huohuo kubadilisha maisha yao” aliongeza.

Airtel Fursa inawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao ni watanzania waishio nchini Tanzania. Vijana hao ni lazima wawe wamiliki wa biashara ndogondogo, wenye hali ya ushindani na kuheshimu biashara zao.

Maelfu ya vijana watapata mafunzo kupitia warsha mbalimbali na kupatiwa vitendea kazi vitakavyo boresha biashara zao.

Hii inajumuisha mafunzo katika usimamizi wa fedha, mikopo, faida za kuwa na akaunti ya benki na usimamizi wa biashara kwa ujumla 
Wanaotaka kujiunga wanapaswa kutuma ujumbe mfupi kwenda 15626 ukiambatanishwa na taarifa zifuatazo;-

jina, umri,aina ya biashara, mahali na namba ya simu. Airtel Fursa pia inakaribisha mapendekezo ya vijana wenye vigezo husika. 

Maombi yanaweza kutumwa pia kwa njia ya barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com  au tovuti ya Airtel.

Maombi yaambatanishwe na jina, umri, aina ya biashara, mahali, namba ya simu na sababu ya kusaidiwa kibiashara.

RITTA NGOWI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS MWAKA HUU

Mwananmke mwingine  ambaye ni kada wa CCM, Ritta Ngowi amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu jana makao makuu ya CCM mkoani Dodoma Ngowi alisema akifanikiwa kuwa rais  ataanzisha kituo kikubwa cha kuwahudumia wastaafu, walemavu, wasiojiweza na vijana.

Kingine atakachofanya ni kuendeleza mazuri yaliyofanywa na marais waliopita, lakini zaidi akiweka mkazo kwenye masuala ya elimu na kukuza uchumi.

Aidha Ritha anafanya ,  idadi ya wanawake waliojitosa mbio za urais kufikia watano kati ya 39 waliochukua fomu hadi sasa.

Kitendo cha mama huyu kuchukua fomu kinaitimisha idadi ya wanawake kufikia watano wengine waliotangulia wakiwa ni pamoja na:

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa (NIMR), Dk Mwele Malecela, Balozi Amina Salum Alli na Monica Mbega.

ALICHOKISEMA MHE.EDWARD LOWASSA ALIPOKUWA MKOANI RUVUMA

Hiki ndicho alichokisema waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa
amesema hana shaka na swala la kukatwa
jina lake katika vikao vya Chama cha
Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama
chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake
kuwa mgombea urais wa Tanzania.

Lowassa aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na wanachama wa CCM na
wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi
kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa
shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM
zaidi ya elfu 52.

"Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977
nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya
kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na
hakuna mgombea atakayeweza kuvunja
rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa
leo anayetaka kukata jina langu anatoka
wapi? anakata kwa sababu gani? 

Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu". alisema Lowassa.

Lowassa aliwasili Mkoani Ruvuma mapema
jana mchana akitokea Mkoani Iringa kwaajili
ya kusaka wadhamini katika mbio zake za
kusaka urais kwa tiketi ya chama hicho,
ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na
kupelekea kufunga barabara kuu ya mjini, hali
iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya paa
la jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze
kuzungumza nao.

STAR WA BARCELONA NEYAMR ATIA URUMA BAADA YA KUFUNGIWA MECHI 4

Barcelona Star Neyamr ambae hivi karibuni amepigwa panga la kukosa mechi nne kwenye Copa America baada ya kitendo cha utovu wa nidhamu alichofanya kwenye mechi.

Licha ya kuwa nje ya uwanja lakini bado anaendelea kuwa supporter mkubwa wa timu yake kwa kukaa jukwaani akishangilia timu yake.

Sasa baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu kujutia kitendo alichokifanya lakini bado ametumia muda mrefu kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa lugh ya kireno jinsi gani anazidi kujutia nafasi aliyoichezea ya kulitumikia taifa lake kwenye soccer. 

WEMA AWEKA SAWA JUU YA SAUTI YAKE INAYOSAMBAZWA MITANDAONI

Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu ambaye ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge wa viti maalumu Singida,amesema anafurahishwa na kitendo cha mashabiki wake kumwigiza sauti akiwa bungeni kwa  kuwa wameonyesha kumkubali kabla hajafika ‘Mjengoni’.

Alisema sauti hiyo inayomuigiza alitumiwa kupitia simu yake na haikumkwaza zaidi ya kufurahia  kwamba watu wengi wanakubali awe bungeni.

“Nafurahi kwa kuwa wengi wameshanipeleka bungeni wakati mimi ndiyo kwanza nipo katika harakati  za kuomba kuchaguliwa kupitia umoja wa wanawake Singida , lakini nafurahia kwa kuwa inaonyesha wengi wananikubali,  ila nikipitishwa kuwawakilisha wana Singida bungeni sitaongea kama walivyonirekodi katika sauti hiyo,” alisema Wema kwa furaha.

MTAZAMO WA WANANCHI JUU YA WAGOMBEA URAIS MWAKA HUU

Wagombea wetu ama watangaza nia tunawapima kwa kipimo gani? Na Je kipimo hicho kina usawa? Tukiacha ushabiki ulio wa wazi ni vigezo gani hasa tunatumia kuwapina?

Tunaposhurutisha Taifa na mgombea tunayemtaka kwa kuaminisha uwezo wa mgombea huku kiukweli tunajua uwezo una walakini je hiyo ni busara?? Na Je rekodi yake kiutumishi ni njema na inaridhisha??

Sizungumzi kwa siasa na vipimo vya majitaka, au hisia na uzushi usio na vithibitisho bali uwazi wa uwezo wa mgombea na uimara wake
Uimara wa mgombea uanze na uwezo wake na wapambe  wake kujihoji kwa dhati na si ushabiki kama kweli mgombea ana uwezo wa kweli kuwa Rais. Kazi hii ya urais ni ya dhamana na majukumu makubwa ambayo inahitaji akili na maarifa ya rais yawe na uwiano wa kufanya mambo kwa usahihi.

Urais ni ubaba  na ni dhamana kubwa sana, kwa kauli, utendaji na maamuzi yake yatalenga na kutolewa kwa umakini, usahihi, busara na hekima.

Urais unahitaji kutumia muda mwingi kufanya tafakari, kuwa na uwezo wa kiakili na kimwili kuhimili ugumu wa kazi na jukumu hili kubwa.

Hivyo tujiulize tunapotaka kuikabidhi kazi hii kwa mgombea fulani, je ni kweli ana uwezo wa kuihimili kazi hii na kuifanya kwa umakini kama inavyotakiwa kufanywa kisheria ??  

Mimi kwa leo sina mengi zaidi ya kusema "tutafakari tunapoelekea october"

BIFU MPYA KATI YA ALIKIBA NA DIAMOND YA CHUKUA SURA MPYA

Vita Saa chache tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar akitokea nchini Marekani kwa shughuli za kimuziki, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ametangaza kile kinachotafsirika kuwa ni vita dhidi ya hasimu wake kwenye anga la muziki huo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.

Ali Kiba alitema cheche Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar, kulikokuwa na uzinduzi wa kampeni ya kupinga vita ujangili, iliyoratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, huku akiwa ni mmoja wa mabalozi sanjari na mlimbwende wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ‘K-Lyin’.

Baada ya shamrashamra za ‘event’ hiyo, haraka sana kama mshale wa Mmakonde, mwandishi wetu alimfuata Ali Kiba, lengo kuu likiwa ni kusikia chochote juu ya ushindi wa Tuzo za Kili ambapo alizoa tano binafsi na moja ya kushirikishwa.

Kiba alisema anaamini alistahili kushinda tuzo zote kwani vigezo na sifa anazo na amejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote anayedhani kuwa ni mfalme wa muziki huo.

Katika mahojiano hayo, mwandishi wetu alimkumbusha Ali Kiba uwepo wa Diamond ambapo kwa haraka sana alimkata kauli mwandishi kwa kusonya na kuweka wazi kuwa miongoni mwa mambo ambayo humpa kichefuchefu, ni pamoja na kusikia jina la Diamond likitajwa mahali popote penye uwepo wake!

“Kaka, sitaki kabisa kulisikia jina hilo, linanipa kichefuchefu, unajua kwa kipindi ambacho nilikaa kimya, nilikuwa nausoma mchezo lakini hakuna aliyeweza kuchukua kiti changu na kuamua kurejea ulingoni kwa kishindo na kuanzia sasa hivi ni mapambano mwendo mdundo,” alisema  Kiba na kuongeza:

“Simaanishi kuwa hakuna msanii mzuri kama mimi, naomba nisieleweke vibaya, wapo lakini siyo huyo dogo (Diamond), muziki ni zaidi ya mbwembwe, niko kikazi na sasa nimedhamiria kweli, kama anaamini yuko fiti, kazi zitaweka wazi ukweli na si drama za kitoto.”

VIPI KUHUSU YEYE NA WEMA?
Mwandishi wetu alitaka kujua kulikoni msanii huyo alimuweka Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Instagram akimmwagia shukrani lukuki na si mtu mwingine?

“Wema amekuwa ni shabiki wangu wa siku nyingi mno, alianza kunipenda kupitia wimbo wangu wa Hands Across the World (kwenye Project ya One-Eight) na kuanzia hapo amekuwa akinipa sapoti kubwa sana, siwezi kukaa naye mbali eti kisa huyo jamaa (Diamond).

“Naamini kwa asilimia nyingi sana hata huu ushindi wangu wa tuzo, umechangiwa na sapoti yake pamoja na wadau wangu wengine,” alisema Kiba.

 AFUNGUKA KUHUSU VIDEO YA MWANA!
Pia, mwandishi wetu alimtaka staa huyo kufafanua madai ya kutoitendea haki video ya Wimbo wa Mwana, ambapo alisema, watu wengi walitarajia aifanye kulingana na mawazo yao ndiyo maana akaamua afanye vile anavyoaamini ingekuwa bora.
“Kila mtu alikuwa ameshatengeneza picha ya jinsi video ya wimbo itakavyokuwa, halafu sifanyi kazi kwa kushindana na mtu, ndiyo maana ilionekana tofauti na mawazo ya wengi, namalizia kwa kusema salamu zimfikie jamaa (Diamond) kuwa mapambano ndiyo kwanza yameanza,” alisema Kiba.

 DIAMOND ANASEMAJE?
Hadi tunakwenda mitamboni, jitihada za kumpata Diamond aweze kuzungumzia vita hiyo iliyofufuka upya hazikuzaa matunda kufuatia simu ya staa huyo aliyekuwa nchini Afrika Kusini kikazi, kuita bila majibu.

 TUJIKUMBUSHE
Kwa muda mrefu sasa, Kiba na Diamond wamekuwa wakiripotiwa kuwa na bifu la chini kwa chini linalotokana kugombania ufalme wa muziki Bongo.

KINDUMBWENDUMBWE SUGU AMFIKISHA MZAZI MWENZAKE KOTINI

Mbunge wa Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ amemfikisha kotini aliyekuwa mkewe,  Faiza Ally akitaka apewe mtoto wao, Shaa (2) ili amlee kwa vile mama yake huyo si mwadilifu.

Aliyekuwa mkewe na mbunge wa mbeya mjini Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’,  Faiza Ally akiwa katika pozi.

Ijumaa iliyopita, saa 2:00 asubuhi, Faiza alipanda kwenye kizimba cha Mahakama ya Mwanzo, Manzese/ Sinza iliyopo Sinza-Makaburini jijini Dar kwa ajili ya kukabiliana na madai hayo.


Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichomwaga ‘ubuyu’ huo, Mheshimiwa Sugu alifikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa na tabia mbaya za mwanamke huyo hasa ya kuvaa nguo zinazomuacha nusu utupu na kupiga picha za aibu, akiamini kuwa, tabia hizo zinaweza kuathiri makuzi ya mtoto huyo.

Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi kirefu, Sugu amekuwa akimvumilia Faiza, lakini hivi karibuni uzalendo ulimshinda baada ya picha zake akiwa amevaa kigauni kifupi na makalio nje kusambaa mitandaoni.


PALIPOKOLEZEA HASIRA
Faiza alivaa kivazi hicho hivi karibuni kwenye hafla ya ugawaji wa Tuzo za Kili Music iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

 SUGU MBELE YA HAKIMU
Akizungumza mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Patrick Vaginga, Mheshimiwa Sugu alidai kuwa mbali na mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kuvaa nusu utupu pia ana mtindo wa kupiga picha zisizo na maadili na kuziweka mtandaoni yeye mwenyewe. Joseph Mbilinyi akionekana kwa mbali katika maeneo ya mahakama.
KUHUSU MTOTO
Sugu alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, pia mwanamke huyo amekuwa na tabia ya kumpiga picha mbaya mtoto wao na kuzimimina humohumo mitandaoni jambo ambalo alisema linamharibu mtoto huyo.

 FAIZA HANA PESA
Mbali na sababu hizo, pia Sugu aliongeza kuwa, Faiza hana kipato kizuri cha kuweza kumlea mtoto na mara kwa mara amekuwa akisafiri jambo ambalo husababisha mtoto huyo kutopata malezi ya mama kwa muda mrefu hivyo kuiomba mahakama impe haki yeye ya kuishi na mwanaye.

 FAIZA AJIBU MAPIGO
Naye Faiza akijibu mapigo katika utetezi wake alisema kuwa, Sugu hafai kumlea mtoto huyo kwa sababu naye ana tabia ya kusafiri kwa muda mrefu hivyo kuishi mbali na mtoto ambapo aliiomba mahakama hiyo isimruhusu baba mzazi huyo kuishi na mtoto kwa kuwa atamharibu.

KESI YAPIGWA KALENDA
Mheshimiwa Hakimu Vaginga akasema kwa vile kesi hiyo ndiyo imeanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza aliiahirisha hadi baadaye mwezi huu ambapo hukumu itatolewa.

 SUGU NJIA YAKE, FAIZA NJIA YAKE
Ijumaa Wikienda lililokuwa mahakamani hapo, liliwashuhudia wazazi hao, kila mmoja akiondoka na njia yake.

KWA NINI FAIZA NI MKE WA SUGU?
Kwa sheria za Kitanzania, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita, hao tayari ni mke na mume kama ilivyokuwa kwa Faiza na Sugu ambao waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.
Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top