Wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu hatma ya uchaguzi mkuu wa Burundi unaotarajia kufanyika mwezi ujao kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea kupinga kugombea tena kwa Rais Pierre Nkurunziza..headlines zimerudi tena nchini humo.
Makamu wa Rais wa nchini hiyo Gervais Rufyikiri ametoroka nchini humo na kudaiwa kimbilia Ubelgiji baada ya kupinga hatua ya Rais wa nchi hiyo kuwania muhula wa tatu akiungana na makamishna wa tume huru ya uchaguzi na jaji mmoja wa mahakama ya kikatiba.
Licha ya msemaji wa serikali kukanusha madai hayo na kusema kuwa Rufyikiri amesafiri nje kwa ziara rasmi ya kikazi lakini mwenyewe baada ya kuhojiwa na Televisheni ya France24 amesema ameondoka baada ya kuhofia maisha yake kufuatia kumpiga Rais huyo kuwania kwa muhula wa tatu ambapo ni kinyume na sheria.
Burundi imeingia katika mgogoro wa kisiasa tangu rais Nkurunziza atangaze nia ya kuwania muhula wa tatu kuongoza nchi hiyo huku maelfu ya watu wakikimbia nchi hiyo kwa kuhofia maisha yao.