Hii ni nafasi nzuri ya kuleta mabadiliko, kuhamasisha vijana na kuwasaidia kujijenga kibiashara endelevu na ninapenda kuwapongeza Airtel kwa ajili ya mpango huu," alisema Mulamula.
Bwana Mulamula aliahidi kufanya kazi kwa karibu na Airtel pamoja na jopo la washauri katika kuhakikisha wanachagua na kuwapa mafunzo walengwa wa Airtel Fursa ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kuweza kutumia techonologia ya habari yaani ICT kama nyenzo muhimu itakayowawezesha kuleta ufanisi katika shughuli zao za uzalishaji na kiuchumi.
Akiamini kuwa vijana watakaofaidiaka na Airtel fulsa watahamasisha na kuongoza katika kuleta mabadiiko kwenye jamii zao huku akihakikisha mpango huu unakuwa na mafanikio makubwa kwa walengwa na kuwa na mvuto kwa vijana wengine .
Mhandisi Mulamula ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama (ICT) Business Incubator (DTBi) kwa ajili ya ujasiriamali katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), analeta uzoefu wa kutosha katika mpango huu wa Airtel fursa kwenye nyanja ya ujasiriamali na kukuza biashara zinazoanza.
Yeye ni mshauri na mwalimu kwa wajasiriamali. Amekuwa akisaidia kuinua vipaji vya watu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na katika mkutano wa kimataifa wa ujasiriamali nchini Moscow, Durban na Nairobi kwa ajili ya maonyesho ya Afrika.
Pia ni Mjumbe wa Bodi ya Demeter nchini Boston USA na pia Mjumbe wa Bodi ya XPrize nje ya California, Marekani.
“Mpango huu unatafuta vijana wenye kiu, nguvu na utayari wakupata wanachokiamini na kukihitaji, wenye uwezo wa kuzipitia changamoto na kufikia matarajio waliojiwekea na wakati huohuo kubadilisha maisha yao” aliongeza.