Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya dola Bilioni 30 kwa ajili ya Kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini.
Hafla ya kutiliana saini ilifanyika jana, Seronela mkoani Arusha ambapo waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress walisaini makubaliano ya dola 2milioni kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya ujangili n anyingine milioni 14.5 kwa ajili ya uhifadhi.
Balozi huyo wa Marekani Mark Childress, alimwelezea Nyalandu, kuwa ni mwanasiasa jasiri na makini asiyeogopa kusema ukweli hata kama unaumiza.
Balozi Childress amesema waziri huyo ni tofauti na wanasiasa wengine na kwamba, ujasiri wake katika utendaji unapaswa kuungwa mkono. Kauli ya Balozi huyo imetokana na uamuzi wa Nyalandu kuweka hadharani idadi ya tembo waliopo nchini na kueleza bayana kuwa, tatizo hilo bado ni janga kwa taifa.
“Kwa mwanasiasa mwingine ingekuwa ngumu kutoa taarifa kama ile kwani angeona anajimaliza lakini alilazimika kufanya hivyo ili njia za kutokomeza tatizo hilo ipatikane na sasa marafiki wa uhifadhi tumeamua tupambane pamoja kulaliza tatizo hili”.
Pia, katika taarifa yake Nyalandu hakusita kueleza kutoweka kwa tembo 10,000 ambao hawakuweza kuonekana wakati wa sensa ya mwaka 2014 iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa.
Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano na uzinduzi wa mradi mkubwa wa kulinda mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini wa PROJECT, ambapo serikali ya Marekani imetoa zaidi ya sh. Bilioni 31 katika utekelezaji wa mradi huo.
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Treetops iliyopo ndani ya eneo la Hifadhi ya Wanyamapori inayosimamiwa na jamii (WMA) kwenye Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.