Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

ILE KATA FUNUA YA UKAWA YAIBUKIA KWENYE MAKAMPUNI 6 YA KIGENI YA KUCHIMBA MADINI NCHINI

Makampuni ya kimataifa yasiyopungua sita yamesema yanafikiria kupunguza kiwango cha uwekezaji nchini Tanzania, baada ya Rais John Magufuli kutangaza kufanya mabadiliko ya kiuchumi, ikiwemo kuongeza kodi kwa makampuni kutoka nje.

Kwa mujibu wa mahojiano yaliyofanywa na shirika la habari la Reuters pamoja na wakurugenzi wakuu wa makapuni ya kigeni yaliyowekeza nchini Tanzania, kiasi ya makampuni sita yanafikiria mipango mipya kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini, mawasiliano ya simu au usafirishaji kwa kutumia meli. Hiyo yote inatokana na juhudi zinazofanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli kuubadili uchumi wa nchi hiyo.

Makampuni matatu yamesema huenda yakapunguza shughuli zake za uwekezaji kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki, huku makampuni mengine mawili yakisema yanafikiria kutanua zaidi shughuli zake katika nchi jirani na kampuni moja imesema inaandaa mchakato wa kujiondoa kabisa nchini Tanzania. Makampuni hayo yaliombwa kutotajwa majina kwa sababu ya umuhimu wa suala hili na kwa sababu mipango yao hiyo bado haijatangazwa hadharani.

Kampuni moja bado haijatoa msimamo wake jinsi ya kukabiliana na mageuzi hayo ya serikali ya Tanzania, huku makampuni matano yakisema kuwa mipango yao haikuathirika na mageuzi hayo, ikiwemo miradi miwili mikubwa, ule wa kiwanda cha kusindika gesi asilia-LNG wenye thamani ya Dola bilioni 30 na mradi wa kiwanda cha mbolea wenye thamani ya Dola bilioni 3.


Tanzania na uwekezaji wa kigeni

Tanzania inategemea zaidi uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja, kuliko nchi nyingine za ukanda huo, kutokana na ukubwa wa uchumi wake. Mwaka uliopita nchi hiyo ilipokea zaidi ya Dola bilioni 1.5, kwenye uchumi ambao thamani yake ilikuwa chini ya Dola bilioni 45. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Umoja wa Mataifa pamoja na Benki ya Dunia.

Rais wa Tanzania, John Magufuli ambaye amepewa jina la utani ''Tingatinga'' kutokana na miradi yake ya miundombinu na aina ya uongozi wake, alizindua mchakato wa mageuzi yake ya kiuchumi, baada ya kuchaguliwa kuiongoza nchi hiyo mwaka uliopita, akiahidi kuubadilisha uchumi wa nchi hiyo, kuondoa urasimu na rushwa pamoja na kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi.

Mwaka huu serikali ya Magufuli iliongeza kodi katika utumaji wa fedha kwa kutumia simu za mkononi, mabenki, huduma za utalii na zile za usafirishaji wa mizigo. Kodi ya mapato kwa mwaka wa fedha 2014/2015 jumla ilikuwa Shilingi za Tanzania trillioni 9.8 ambazo ni sawa na Dola bilioni 4.5. Kwa mwaka wa fedha 2016/2017, serikali ina lengo la kukusanya kodi ya mapato zaidi ya trilioni 15.1, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 50.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Adolf Mkenda, amesema wameyasikia malalamiko yanayotolewa na milango iko wazi, lakini wanahakikisha kuwa kila mtu analipa kodi anayopaswa kulipa kwa kuzingatia haki. Amesema lazima kuwepo na mageuzi mapya ambayo ni magumu, ili kuufanya uchumi kuwa imara.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Richard Kayombo amesema ongezeko la kodi ya mapato lilihitajika kwa ajili ya kulipia miundombinu mipya nchini humo. Makampuni makubwa ya kigeni ambayo yamewekeza nchini Tanzania ni pamoja na yale ya nishati, uhandisi, mawasiliano ya simu, madini, na usafirishaji kwa kutumia meli.

Source: Reuters Africa

Kama uliikosa Ile habari ya madada poa wa Dar, basi iko hapa kwa ajili yako

Akiwa katika eneo hilo baada ya kukatiza vichochoro kadhaa, alifika eneo la klabu cha pombe za kienyeji, na kuzungumza na mmoja wa wateja waliokuwa wakinywa hapo.

“Hii achana nayo kabisa ni moto wa kuotea mbali. Hebu niikate kidogo uone”, Mzee aliyejitaja kwa jina la Mandela, alimtambia Makonda huku akipiga funda la pomne hiyo ya kienyeji hali inayoonyesha kuwa hakuwa akifahamu kuwa anayezungumza naye ni Mkuu wa mkoa.

Baadaye alienda eneo lenye vibanda vya chumba kimoja kimoja, amabavyo inaelezwa kuwa ni madanguro ambayo hutumika kufanyika biashara ya ukahaba hadi kwa wasichana wenye umri mdogo.

Hata hivyo kila mlango aliojaribu kugonga Makonda, ulikuwa umefungwa na hakuna aliyeitika hodi yake.

” Hawa wakijua watu wa serikali wanakuja hapa basi hufunga biashara zote. sasa na hapa wamefunga, si rahisi kumpata mtu” Kijana mmoja mwenyeji wa eneo hilo alieleza.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shuleya Msingi Tandale Makonda alisema, serikali inafanya mipango ya kupata wawekezaji ili kununua eneo hilo la Uwanja wa Fisi na kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo ili vibanda vyote vivunjwe na kujengwa vitegauchumi. badala ya kuliacha eneo hilo liharibu maisha ya vijana.

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alibisha hodi kwenye mlango mmoja katika banda linalodaiwa kutumiwa kwa biashara ya ukahaba, katika eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo, Tandale Kata ya Manzese, akiwa katika siku ya tisa ya ziara yake mkoani humo leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi. 

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, akimsaidia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kubisha hodi kwenye mlango mmoja katika banda linalodaiwa kutumiwa kwa biashara ya ukahaba, katika eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo, Tandale Kata ya Manzese. 

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alichunguza kwa makini bia ili kuthibitisha kama muda wake wa matumizi bado haujapita. Makonda alisema, kuna taarifa kwamba wafanya biashara za vileo katika Uwanja wa Fisi wamekuwa wakiuza viwaji hadi vilivyokwisha mda wake wa matumizi.

 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Salum Hapi, alimpatia maelezo Makonda baada ya kufika eneo la Uwanja wa Fisi, Tandale, kata ya Manzese.

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alizungumza na wateja wa pombe za kienyeji kwenye kilabu cha pombe hizo kilichopo Uwanja wa Fisi, alipofanya ziara katika eneo hilo leo

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliondoka kwenye eneo la Uwanja wa Fisi baada ya kujionea mambo mbalimbali katika eneo hilo.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka ulimwenguni, ingia hapa kujua nani anaongoza

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka ulimwenguni ambapo mpaka sasa Argentina ndio inayoongoza duniani.


Kwa upande wa Afrika Senegal ndio vinara na ipo nafasi ya 33 ulimwenguni, huku wakifuatwa na Ivory Coast katika nafasi ya pili ambapo wanafungana na Tunisia kwenye Nafasi hiyo na nafasi ya 36 ni Misri na wapo nafasi ya 34 ulimwenguni.

Viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza vyazidi kuongezeka nchini.Soma zaidi hapa


Viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza vyazidi kuongezeka nchini.Soma zaidi hapo chini kisha washirikishe na wenzio.

Asilimia kubwa ya wanawake tunapenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi

Asilimia kubwa ya wanawake tunapenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi. Lakini tunapotambua kwamba wameshaoa hushangaa sana na huumia na kusema wanaume wote ni mbwa tu.

Wanaume sio mbwa ni sisi wenyewe ndio tumeshindwa kufanya uchunguzi. 

Tulishaambiwa kwenye kila mafanikio ya Mwanaume nyuma yake Kuna mwanamke. Na wewe unataka Mwanaume mwenye mafanikio unategemea nini???

Huyo sio mumeo mtarajiwa huyo ni mume wa mtu Fulani Ni agharabu sana kukutana  na Mwanaume anayejiweza akawa single, either uwe shareholder au unyanganye share ya mwanamke mwenzio kitu ambacho sio busara.

Mume wako yupo anahangaika kutoka kimaisha anapigania ndoto zake. Huenda yuko shule, shambani, dukani au anabeti kimsingi yupo anapigania kutoka Kimaisha.

Anakusubiri tu wewe umpe support na back-up ya kutosha mtafute huyo uanze nae chini na sio kukimbilia waume za watu.

Ajali iliyotokea eneo la Msikitini yasababisha foleni kubwa kwa wakazi wa Mbagala

Kitendo cha kutokea ajali maeneo ya Maikitini eneo ambalo liko katikati ya Mrongani na Mission wilaya ya Temeke kumesababisha foleni kubwa sana kwa watumiaji wa barabara ya Kirwa Road.

Ambapo folen ya kutoka mjini kwa walio fangulia imeanzia Bandari na kuishia eneo la Mission. Magari yanayotoka mjini kuelekea Mbagala rangi tatu yakifika Mtongani yanatumia barabara ya magari yanayotoma mbagala kuelekea mjini na kwingineko.
Na kwa wale wanaotoka Mbagara kuelekea maeneo ya mjini, kama Tandika, Buguruni, Ubungo nk, foreni yao imeanzia Zakhem hadi Mission. 

Zoezi la kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu linaendelea, habari kamili iko hapa

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, ambaye anaongoza timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama, kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu.

Amekamata shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kukifuma kiwanda bubu kinachotengeneza konyagi  na Smirnoff feki maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam.


Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia 'spirit' ambayo inachanganywa na gongo.


Pia katika zoezi hilo wameweza kukamata chupa tupu na zilizojazwa pombe, vizibo, pamoja na vifungashio.


Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na polisi mpaka sasa.

Wananchi katika mji mkuu wa Seoul Korea Kusini wanaandamana wakishinikiza Rais wao, ajiuzulu

KOREA KUSINI: Wananchi kwa maelfu katika mji mkuu wa Seoul wanaandamana wakishinikiza Rais wa nchi hiyo, Park Geun-hye ajiuzulu.

Rais Park Guen Hye, anatuhumiwa kwa kuwa na uhusiano wa karibu na baadhi ya watu, wanaokabiliwa na shtaka la kujaribu kuibia Serikali fedha nyingi kupitia kampuni kadhaa za taifa hilo.

KILA MTU ANAENDESHA CHOMBO CHAKE JINSI ANAVYOJUA YEYE MWENYEWE, EBU TAZAMA HII


Ajali hii ilitomea kituoni kabisaa, eneo la Kizuiani Mbagala.
Gari namba T 602 DGT ndilo lililo sababisha ajali maeneo hayo.
Gari tajwa ndio iyo hapo inayoonekana kwa upande wa kushoto. Na mwenye bajaji alikuwa akidai bajaji yake haikuwa na break nzuri.
Na gari namba T 436 DFM iyo daladala unayoiona hapo upande ww kulia ilikuwa imepaki kituoni bila shida yoyote.
Baada ya gari tajwa hapo picha ya juu yake hii ilikuja bajaji yenye namba MC 495 AEQ nayo ikawa inaingia kituoni kabla haijasimama ndipo olipoingia ole daladala tajwa hapo mwanzoni kabisa mwa habari hii kisha kusababisha ajali hii.
Mabishano galichukua mda mwingi kama dakika 10 hivi, na mwenye bajaji akiwa ni mtu mwenye uremavu wa miguu alikuwa na wenzake wawili nakufanya idadi ya watu kwenye bajaji ole kuwa na jumla ya watu watatu.
Mwenye iyo daladala unayoiona hapo kushoto kwako alikuwa akidai yeye amegongwa na mwenye bajaji wakati yeye ndiye aligeingia vibaya kituoni na kumgonga mwenye bajabi kisha mwenye bajaji kujibamiza kwa ole daladala ya kulia.

Raia wa China achana noti ya Shillingi elfu moja akiita Toilet Paper, habari kamili iko hapa.

Mida hii, maeneo ya Mikocheni B, Baraka plaza, raia wa China amechana noti ya Shillingi elfu moja akiita Toilet Paper.

Huyu jamaa alichukua Bajaji kwenda sehemu fulani. Maelewano ikawa ni Shilingi 4000. Lakini akatoa shilingi 2000. Mwenye babaji alipouliza ni kwa nini, akasema hiyo siyo sehemu ya 4000. Kwa hiyo anampa 2000. Mwenye Babaji akakataa kupokea.


Matokeo yake mchina huyo akachana hela na kumtupia akisema take your toilet paper. Basi raia waliokusanyika wakamzuia huyu mchina kuondoka na kuita Polisi.

Mida hii Polisi wamemchukua na kuelekea naye kituo cha Polisi Oysterbay


                           Aachiwa huru

Wanajamvi, yule mchina Aliyechana shilling 1000 na kuiita toilet paper ameachilliwa huru mchana baada huu, baada ya kukaa Polisi takribani masaa matatu tu.

Kwa waTanzania hii ni tusi kubwa sana. Iwe je Polisi wa Hoysterbay wamuachilie huyu mchina wakati watu wanaofanya makosa madogo barabarani wanaswekwa ndani?

Tazama picha tano za tukio la kuungua kwa ghala la Saba Spare Parts Mwenge

Kutoka hapa nilipo naona moshi mkali. Kwa mujibu wa watu waliopo eneo la tukio, wanasema moto unawaka jirani na chuo cha Tumaini kampasi ya Mwenge.


Kinachoungua ni ghala linalomilikiwa na Saba Spare Parts linateketea kwa moto muda huu. Zimamoto wamefika na wanaendelea na uokoaji.


Tazama picha zote za tukio hili la kuwaka kwa moto kwenye eneo hili.

Endelea kutazama pocha zote za tukio hili

Mtoto Happiness Josephat (6) aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza betri moyoni (JKCI), amefariki dunia.

Mtoto Happiness Josephat (6) aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza betri moyoni katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), amefariki dunia.

Mama mzazi wa Happiness, Elitruda Malley amesema Happiness alifariki dunia ghafla juzi mchana. 

Alisema   Jumapili, mtoto huyo alikuwa mzima na walikwenda kanisani kutoa sadaka ya shukrani kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa mambo aliyowatendea na wakarudi nyumbani salama. 

“Jana tumeamka vizuri lakini ghafla hali yake ilibadilika akaanza kulalamika kuwa anajisikia vibaya, tukamkimbizia Hospitali ya Selian hapa Arusha lakini tukiwa njiani alifariki dunia,” alisema. 

Elitruda alisema kifo cha mwanawe kimemhuzunisha mno na  daima atamkumbuka. 

“Alikuwa tayari amesharudi shuleni, alikuwa akiniambia kuwa atasoma kwa bidii ili ndoto yake ya kuwa daktari bingwa itimie aweze kusaidia watu wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali,” alisema. 

Hata hivyo, alisema maziko ya Happiness yanatarajiwa kufanyika leo huko Mbulu mkoani Manyara. 

Mkurugenzi wa JKCI, ambako Happiness alifanyiwa upasuaji, Profesa Mohamed Janabi amesema taarifa hiyo imemshtua ikizingatiwa mtoto huyo alikuwa anaendelea vizuri. 

“Sikuwa na taarifa, nitawasiliana na mama yake   tujue hasa shida gani ilitokea, maana zipo sababu nyingi labda alipita jirani na mitambo ya umeme au simu, hizo ni sehemu hatarishi kwa mtu aliyewekewa betri kwenye moyo,” alisema. 

Happiness alifanyiwa upasuaji huo wa historia nchini Julai 15, mwaka huu katika Taasisi ya JKCI wa kuwekewa betri maalumu kwenye moyo ambayo kitaalamu inaitwa ‘pacemaker’. 

Kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimtibia mtoto huyo, wakati alipopekekwa hospitalini hapo, mapigo yake ya moyo yalikuwa 20. 

Walisema  hali hiyo kwa mtoto si ya kawaida kwa vile  anapaswa kuwa na wastani wa mapigo 60 hadi 100 kwa umri wake. 

Mtoto Happiness alizaliwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi hali hiyo huwakumba watu wazima. 

Moja ya ndoto za mtoto huyo ambayo alinukuliwa akiisema ni kuwa daktari bingwa wa kutibu magonjwa mbalimbali.

Ushauri wa bure kwa mabinti wenye malengo na mtazamo mzuri juu ya ndoa, ingia hapa

Leo nimeona nije hadharani hapa kutoa ushauri kwa mabinti wa makamo (30+yrs) ambao huenda kwa sababu za hapa na pale hawajafanikiwa kuingia kwenye ndoa wala kuwa na mahusiano yanayoashiria kuanzisha familia hivi karibuni. 

Msingi wa mada yangu umetokana na mabinti kadhaa ninao kutana nao mara kwa mara maeneo mbali mbali kuwa na vilio karibu sawa. 

Wakati nafanya kazi Taasisi fulani Dsm, kuna dada nilizoena nae kiasi cha kunisimulia baadhi ya mikasa ya kimahusiano na changamoto anazopitia. 

Binti huyo mwenye miaka zaidi ya 30 alipitia magumu ikiwa ni pamoja na kutoa mimba kadhaa baada ya kutoona mwelekeo wa waliompachika, kuamua kugharamia mahusiano kwa kumuhudumia kila kitu mwanaume, kulazimika kubadili dini mara kadhaa kwa ajili ya mwanaume Ki uficho bila wazazi wala ndugu zake kujua. 

Yote hayo aliyafanya ili kuwaridhisha wanaume angalau aitwe Mke wa fulani!! Lakini cha ajabu alikuwa anaambulia patupu 

Si huyo tu, wako wengi wa namna hiyo na ambao wana visa tofauti tofauti lakini mwisho wake huishia kupata machungu na maumivu sababu ya mahusiano. 

Ni kweli, ndoa ina heshima yake. Ndoa humfanya mtu aongezeke thamani katika jamii. Hilo halipingiki. 

Pamoja na ukweli huo mtamu, lakini kuna ukweli mwingine ambao huenda watu hawaupendi kwamba sio wote wenye bahati ya kuwa na ndoa imara au hata hiyo ya kulega lega!! Wapo wengi wanamaisha yao mazuri na hawana hawaishi katika ndoa na wala hawajawahi kuolewa achilia mbali kutambulisha mchumba nyumbani. 

Kuna mabinti wengi wanahangaika sana na wanateswa sana na mahusiano. 

Unakuta Binti mzuri, mrembo, umri mkubwa tu wa kuweza kujiamlia mambo na nzuri zaidi Mungu kamjalia kazi nzuri na anauwezo wa kukabiliana na majukumu yanayohitaji pesa. Cha ajabu kutwa nzima anamaliza pesa zake kumgharamia mwanaume. 

Binti huyo huyo akishika ujauzito akili hulalia upande wa kutoa eti kisa hajaolewa na anatamani sana aolewe kwani karibu rafiki zake na wadogo zake wameolewa tena kwa mbwe mbwe na michango ya harusi anatoa kila mwezi!! 

Ushauri wangu ni mmoja tu, huna haja ya kuteseka wala kusononeka! Kama uwezo wa kulea unao!! Una kazi ya kukuingizia kipato, unauhakika mwanao hatokosa huduma za msingi kutoka kwako, acha kuteseka! Ruhusu moyo wako kukubali uhalisia kuwa si kila mwanamke ameandikiwa kupata watoto ndani ya ndoa. Watoto wana thamani kuliko hata hiyo ndoa unayo ng'ang'ania. 

Nafahamu kuna haja za mwili za hapa na pale. Lakini ukishakuwa na maisha yako na unajitambua na kufahamu uhalisia wa maisha yako, hautashindwa kuzitimiza na kuendelea ku-control maadili ya nyumba yako! 

Ni hayo tu wapwa zangu, wakuchukua achukue na wakupuuza hashikiwi fimbo! 

Wakamatwa wakidaiwa kujihusisha na ulaji wa nyama za watu, zaidi bofya hapa

Serekali ya kenya imewakamata baadhi ya watu ambao inasadikiwa wamekuwa wakijihusisha na ulaji wa nyama za watu 


watuhumiwa hao wamekutwa na badhi ya viungo vya watu wanaodaiwa kuuwawa kwa lengo la kufanywa kitoweo.

Majina ya wasanii watakaowania tuzo za EATV yatajwa, bofya hapa kuyaona

Awamu ya kwanza ya kutaja majina ya wasanii watakaowania tuzo za EATV kwa mwaka huu wa kwanza yametajwa Jumanne hii. 

Kwa kuanzia yametajwa majina ya wasanii kutoka katika vipengele viwili kati ya kumi vilivyopo kwenye tuzo hizo huku zoezi hilo likitarajiwa kufanyika kwa siku nne ambapo litakamilika Ijumaa hii ya Novemba 11. 

Hii ni orodha ya wasanii waliotajwa kwenye vipengele hivyo. 

Mwanamuziki bora chipukizi 

Man Fongo 
Feza Kessy 
Ruky Baby 
Mayunga 
Bright 

Muigizaji bora wa kiume 

Saidi Ali – Ndugu wa mume 
Meya Shabani – Profile 
Daudi Tairo (Duma) – 
Salim Ahmed (Gabo) – Safari ya Gwalu 
Dotto Matotora – Likwacha Lala

Matokeo ya kura zenu juu ya Donald Trump na Hillary Clintoni ni kama ifuatavyo

Shukurani za dhati kwako wewe shabiki wetu wa Tanzania ulieitikia wito wa kushiriki katika zoezi la kuchaguwa kati ya Donald Trump na Hillary Clinton, nani ungependa awe rais ajaye wa Marekani.


Matokeo ya kura zenu ni kama ifuatavyo:
Tanzania
Donald Trump: 39.6%
Hillary Clinton: 60.4%
Mataifa mengine ya dunia:
Donald Trump: 31.2%
Hillary Clinton: 86.8%

Mtoto wa marehemu Samweli Sitta aeleza ugonjwa uliosababisha kifo cha baba yake

Ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume umetajwa kuwa ndio chanzo kilichopelekea kifo cha Spika Mstafuu wa Bunge la Tanzania, Samwel John Sitta. 

Mtoto wa marehemu Samwel Sitta, Benjamin Sitta ambaye ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni alisema kuwa baba yake alifariki kutokana na saratani ya tezi dume ambayo ilikuwa imesambaa mwilini kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea. 

Samwel Sitta alifarika alfajiri ya jana nchini ujerumani alipokwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu ikiwa ni kwa mara ya pili kwenda nchini humo baada pia ya kwenda India kwa ajili ya matibabu. 

Wataalamu wa afya wameeleza kuwa ugonjwa huu huwaathiri zaidi wanaume wengi wenye umri kuanzia miaka 60. Aidha, wameeleza kuwa tezi dume hupatikana chini ya kibofu cha mkojo na imezungukwa na mirija ya mkojo. 

Mbali na watu wenye umri kuanzia miaka 60, watu wengine walioko kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu ni pamoja na wanaume kutoka Afrika (Weusi), wanaume ambao kwenye familia zao kuna historia ya ugonjwa huu. 

Saratani hii hupelekea maumivu makali ya mifupa kwenye nyonga, mapajani na kiunoni, uume kushindwa kufanya kazi, kupungua uzito, uchovu, kichefuchefu, baadhi ya sehemu za mwili kushindwa kufanya kazi. 

Kuna vipimo vya aina tatu vya saratani ya tezi dume ambapo, vipimo vya kwanza ni vile ambavyo hufanyika kuangalia kama mtu ana ugonjwa huo, vipimo vya pili hufanyika kuthibitisha kama ni saratani ya tezi dume au ni uvimbe tu, na vipimo vya tatu hufanyika kuangalia madhara yaliyosababishwa na ugonjwa huo. 

Matibabu yake hufanyika ambapo mgonjwa akiwahi hospitali, tezi hizo huondolewa ili kuizuia saratani kusambaa zaidi mwilini, huweza pia kupatiwa tiba ya miozi, dawa. 

Inashauriwa na wataalamu wa afya kuwa, kwa wanaume wote wenye umri kuanzia miaka 50 wafanye vipimo ili kuweza kufahamu kama wana saratani ya tezi dume au la.

MAAFISA POLISI WARUHUSIWA KUVAA HIJABU KAZINI, ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali ya Scotland imeidhinisha vazi la hijabu na kulijumuisha kwenye sare za maafisa wa polisi wa kike wa Kiislamu ili kuongeza idadi yao katika idara hiyo. 

Mkuu wa idara ya polisi nchini humo Phil Gormley, ametoa maelezo na kubainisha furaha kubwa kwa kutangaza uamuzi huo, na kufahamisha nia yao kutaka kusaidiana na maafisa wa Kiislamu katika suala la usalama wa taifa. 

Muungano wa maafisa wa polisi wa Kiislamu SPMA nchini humo pia ulitoa maelezo na kufahamisha kwamba uamuzi huo utaweza kuimarisha mahusiano bora kati ya jamii za Scotland na jumuiya ya Kiislamu. 

Mkuu wa SPMA Fahad Bashir alisema, ''Uamuzi huo uliochukuliwa na serikali ni sahihi. Tunapata faraja kuona nchi yetu ikichukuwa hatua muhimu kama hizi zenye mwelekeo mzuri.'' 

Hapo awali, maafisa waliokuwa wakiruhusiwa kuvaa hijabu walikuwa ni wale waliohudumu kwa miaka zaidi ya 15 na wanaoshikilia nyadhifa za juu. 

Katika mwaka 2001, sare rasmi za polisi zilitambulishwa ambapo hijabu pia ilijumuishwa.

Master Jay aeleza kilichomfanya kuacha kazi ya mziki, ingia hapa kujua zaidi

Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna muziki pasipo kuwa na watayarishaji wa muziki – lakini wao ndio wamekuwa wakiongoza kuishi maisha ya chini zaidi. 

Akiongea na kipindi cha Ladha 3600 ya EFM, mtayarishaji mkongwe wa muziki hapa nchini Master Jay amesema kuwa kwa Bongo ni maproducer wachache wenye maisha ya kwendana na hadhi yao. 


“Kati ya maproducer wanaoishi maisha mazuri hapa mjini ni mimi na Hermy B,” amesema Jay.

Master ameongeza kuwa yeye alishtuka mapema ndio maana akaamua kuachana na kazi hiyo kutokana na kutoona faida na kazi hiyo wakati huo huo akiwa na familia inayomtegemea.

Samsang yawataka wateja wake kurudisha mashine milioni 3 za kufulia wakidai zinalipuka

Samsung imewataka wateja wake kurudisha takribani mashine milioni 3 za kufulia zinazodaiwa kuwa zinaweza kulipuka wakati zikifanya kazi.

Mwezi Septemba kampuni hiyo ya Korea Kusini ilitangaza kurudishwa kwa simu za Samsung Galaxy Note 7 ambazo ilidaiwa kuwa zinalipuka wakati wa kuchajiwa.

Kampuni ya vifaa vya umeme ya Samsung yatangaza kurudishwa kwa takribani mashine milioni 3 za kufulia kwa kuwa kuna taarifa za kuwa mashine hizo zinaweza kulipuka wakati zikifanya kazi.

Mwezi Septemba kampuni hiyo ya Korea Kusini ilitangaza kurudishwa kwa simu za Samsung Galaxy Note 7 ambazo ilidaiwa kuwa zinalipuka wakati wa kuchajiwa.

UJUMBE WA ODAMA KWA MASHABIKI ZAKE NIMEKUWEKEA HAPA USIUKOSE

Katika safari ya maisha lazima kukutana na watu wa aina hii kamwe usikate tamaa. Pambana na mtangulize Mungu.

1:Niwale Unao Waamini kugeuka kuwa Maadui licha ya pendo uliowaonyesha kuugeuza chuki na Misaada Uliowapa wakakuchimbia na shimo la kukuangamiza hawatakumbuka chochote chema ulichowatendea bali kutafuta ubaya wako na kukuhukumu.

Wakati walikua nayo nafasi ya kukuuliza na kukuchunguza sababu uliwapenda na kuwaheshimu. Fahamu kua ni rahisi sana (rafiki kua adui).

2:Mtu wapili atakae Kushangaza ni yule usiemjua wala hukuwahi muona lakini akakuhifadhi nyakati za shida bila Kujiuliza wewe ni nani na kwanini anakusaidia ila basi tu, akakutoa katika shimo ulilotupwa na ulio waita Marafiki bila ya kujali kama utamgeuka hata yeye.

Usichoke kutenda wema kwani siku zote nguvu yetu yakujiamini hutokea kwa wasiotujua ndio huona Karama iliyo ndani yetu sababu wale wanaotufahamu husoma zaidi madhaifu yetu na husahau kuangalia nguvu iliyo ndani yetu usiogope.

Niwakati wako sahihi wakusema maumivu tena basi angalia nani unamwita RAFIKI na kwanini JE nii aina ya RAFIKI unaemuhitaji je atakutambulisha vyema mbele ya wasio kujua??? Muda wa kuamka na kufanya maamuzi sahihi.

Mawaziri walioteuliwa na Rais Magufuli wanaogopa kumweleza ukweli kuhusu hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi.

Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamesema uchumi wa nchi unayumba, huku mawaziri walioteuliwa na Rais Dk. John Magufuli wanaogopa kumweleza ukweli kiongozi huyo kuhusu hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi.

Kutokana na hali hiyo, wamesema ipo haja kwa Serikali kujitafakari na mipango yake mingi ambayo imekuwa na ugumu katika utekelezaji wake.

Akichangia hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa ya 2017/18 na Mwongozo wa Kuandaa Bajeti, iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango bungeni jana, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alisema hotuba ya waziri huyo haina jipya ila imerudia mambo yaliyopita ya mwaka 2015/16, huku akihisi nchi hii ni ya watu wa hali ya juu pekee.

Alisema kuwa Waziri Mpango alitakiwa kuichambua ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia (WB) Oktoba 20, mwaka huu ambayo inaonyesha uchumi wa nchi umezidi kuporomoka hadi kushika namba 139 duniani.
Bashe alisema kilichowasilishwa na Waziri Mpango ni tofauti na hali halisi ya maisha ya kawaida ya wananchi waliopo mitaani.

“Waziri wa Fedha usirudie uliyoyafanya 2016/17, nalisema kwa sababu angalia vitabu vyake hapo, nchi hii si ya Executive Only (si ya watu wakubwa pekee). Unakuja na kitu kilekile, eti eneo la kimkakati Kurasini, huku unataka kuua Kariakoo ili Wachina watumie ile nafasi.


“Jamani hatuwezi kwenda hivyo, boresheni Kariakoo ili mruhusu hawa waswahili walipe kodi, tuacheni kabisa dhana mbaya.


“…Sijui kwa kuwa wewe hukuomba kura na hujui hali ngumu iliyopo mitaani, vijijini fedha hakuna halafu unakuja hapa kusema tunatekeleza. Waziri wa Fedha asipochukua tunayomshauri, tuna jukumu la kuungana bila kujali itikadi zetu humu ndani bungeni,” alisema Bashe.

Alisema ni lazima waziri aangalie sheria za nchi kama zinavutia wawekezaji wote na si wa nje peke yao.


“Ninashangaa sana katika taarifa ya waziri, anasema mazingira na hali ya hewa itakuwa nzuri huku taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zinasema kuna ukame. Leo hali ya hewa kwa nchi jirani unasema ni nzuri si kweli, kwa 2017/18 nchi zinazotuzunguka zina hali mbaya ya chakula na hata taarifa ya TMA inasema hivyo,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Solwa, Ahmed Salum (CCM), alisema hivi sasa kuna tatizo la mzunguko wa fedha katika jamii, huku akishangazwa na kauli ya Waziri Mpango ya uchumi kuimarika.


Alisema anashangazwa na taarifa ya kuimarika uchumi, japo bado kuna matatizo ya uchumi, ikiwamo upande wa wawekezaji wanaokuja nchini.


Mbunge huyo alisema hakuna kituo kimoja kwa ajili ya kuhakikisha wawekezaji hawasumbuliwi, lakini bado kuna tatizo Kituo cha Uwekezaji (TIC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao hukaa na nyaraka muda mrefu bila kufanya uamuzi.

Jela Mwaka Mmoja kwa Kumdhalilisha Mama Yake Mzazi, bofya hapa kujua zaidi

Mwanaume mkazi wa Ilala, Siwema Seif (40) amehukumiwa na Mahakama ya Mwanzo ya Ilala kwenda jela mwaka mmoja kwa kumtolea lugha ya matusi na kumdhalilisha kimwili, Zainab Ramadhan ambaye ni mama yake mzazi.

Akisoma hukumu mahakamani hapo jana, Hakimu wa Mahakama hiyo, Matrona Luanda alisema ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji, ulionesha kukosa shaka na kumtia hatiani mshitakiwa.

Shahidi huyo alisema siku ya tukio mshitakiwa alifika nyumbani kwao akaomba chakula akajibiwa kuwa kuna wali na mshitakiwa akasema hataki wali bali anataka ugali na mama akamjibu asingeweza kupika ugali na kumsisitiza Siwema ale wali.

Zainab alisema baada ya majibizano hayo, mshitakiwa alimtukana matusi ya nguoni mama yake, huku akisema hawezi kumzaa na kumkashifu kwamba hana sehemu ya kumzalia huku akitishia kumwua akiahidi kumtoa roho ndipo amjue yeye ni nani.

Kwa mujibu wa Zainab, alipoona ugomvi na matusi umezidi aliingia chumbani mwake, na ndipo mlalamikaji akamfuata na kumtukana huku akitishia kumwingilia kinyume cha maumbile.


“Baada ya hapo mshitakiwa alinivamia na kunidhalilisha kimaumbile kwa mikono yake,”alisema.

Baada ya ushahidi wa mama huyo dhidi ya Siwema, Mahakama ilitoa nafasi kwa kijana huyo kujitetea na Mahakama ikamtia hatiani.

Mwendesha mashitaka Blanka Shao alisema kwa kuwa japo mshitakiwa alikuwa mkosaji wa mara ya kwanza, kitendo alichokifanya ni cha kifedhuli tena haonyeshi kujutia, alishauri apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake.

Hakimu Luanda alimhukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa kitendo alichomfanya mama yake mzazi.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 9 Ilala, mtaa wa Sophia Kawawa, nyumba namba 10.

Ujio wa Lebo ya msanii Alikiba, wasanii maarufu wapewa shavu, ingia hapa kujua zaidi

Imekuwa ni kama fashion sasa kwa wasanii wa Bongo Fleva kwa kila mmoja kutaka kuwa na lebo yake, ukiachilia mbali wale ambao walikwisha tangulia kwenye mambo hayo na lebo zao zikafanya poa.


King Kiba amesema kuwa yuko katika maandalizi ya kurudi rasmi katika suala hilo la kusimamia wasanii (Kuanzisha Lebo) na tayari kuna wasanii ambao amekwisha fanya nao mazungumzo na watakuwepo chini ya
lebo hiyo.


“Me record lebo ninayo muda mrefu, lakini sikuifanya matangazo, lakini kuna wasanii ambao nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi narudi tena najipanga upya kama unavyomuona Abby Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea kufanya kazi zingine,

Abdu Kiba pia ametoa ngoma hivi karibuni lakini haijafanya vizuri lakini ngoma ijayo itakuwa ni ya mimi na yeye. Pia kuna msanii mwingine ambaye watu hawajawahi kumsikia, pia kuna wakina Jokate, kina Dalila na wengine kibao tu ambao wapo chini ya Lebo
yangu.”

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top