Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WAKAZI WA MKOA WA KAGERA WAMLILIA RAIS MAGUFULI JUU YA UNUNUZI WA MELI MPYA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameombwa na baadhi ya wananchi mkoani Kagera kutimiza ahadi yake aliyoitoa ya kununua meli mpya itayotumia Ziwa Victoria kutoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo  kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza ili waweze kuondokana na hadha ya usafiri wa majini wanayokumbana nayo kwa sasa baada ya meli za Mv. Serengeti na Mv. Victoria zilizokuwa zikitoa huduma hiyo kusimamishwa kutokana na ubovu uliokuwa ukihatarisha usalama wa mizigo na abiria.

Baadhi ya wananchi hao ambao hutegemea zaidi huduma usafiri wa majini kusafirisha mizigo yao na kusafiri pi ambayo hutolewa na kampuni ya Taifa ya huduma za meli, wakizungumza na ITV wakiwa kwenye eneo la bandari ya Bukoba wamesema hatua ya kusimamishwa kwa  huduma ya usafiri wa meli kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza kuwa imewaathiri sana kwa kuwa kwa sasa mizigo yao mingi wanaisafirisha kwa kutumia njia ya barabara jambo linalowagharimu fedha nyingi, wamesema meli za Mv. Serengeti na Mv. Victoria hazifai kutoa huduma ya usafiri hata zikifanyiwa matengenezo.

Kwa upande wake, Afisa wa kampuni ya Taifa ya huduma za meli katika bandari ya Bukoba, Mathias Mathew akizungumza amesema meli ya Mv. Serengeti itaanza kutoa huduma baada ya kufanyiwa ukarabati, amesema meli ya Mv. Serengeti ambayo ni meli pekee iliyokuwa ikitoa huduma ya usafiri kati ya bandari ya Mwanza na Bukoba ilisimamishwa kutoa huduma ya usafiri Machi 21, mwaka huu kutokana na ubovu jambo ambalo limeitia hasara kampuni hiyo zaidi ya shilingi zaidi ya milioni 432 kwa kuwa kila juma ilikuwa ikiingiza zaidi ya shilingi milioni 36.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top