Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WALIOPATA AJALI WAKATI WA KUCHUMA KARAFUU ZANZIBAR KULIPWA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia shirika lake la biashara la ZSTC imeanza kuwalipa fidia  wanananchi ambazo wakati wa uchumaji wa karafuu  walipata ajali ya kuanguka na  kuumia wakati wa uchumaji wa karafuu akiwemo mmoja aliyefariki katika zoezi hilo.

Zoezi hilo la kuwalipa wananchi hao lilifanyika afisi kuu ya  ZSTC hapa zanzibar ambapo mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo la Taifa  la biashara Maalim Kassim Seleman alikabidhi fedha  milioni 11.5 kwa waathirika hao na kusisitiza kuwa serikali imetenga fedha maalum  ambazo zinatokana na mauzo ya karafuu kufidia malipo inapotokezea ajali na zoezi hilo awali lilisitishwa  lakini sasa serikali imelirejesha tena.

Kwa  upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo   amezitaka familia kuacha mara moja mtindo wa kuwatumia watoto wadogo katika zoezi la uchumaji wa karafuu kwakuwa ndiyo waathirika wakubwa na  kusisitiza sheria hairuhusu watoto wadogo kufanya kazi.

Naye mmoja ya mwananchi ambaye familia yake imeathirika katika zoezi hilo Mwadini Ally mbali ya kuishukuru serikali kwa msaada huo ambao hawakuutarajia  amekiri kuwa wamefanya makosa kuwatumia watoto wadogo kuchuma  karafuu.

Katika zoezi hilo wananchi hao saba akiwemo mmoja  aliyepokea  kwa niaba ya marehemu aliyefariki walipokea fedha taslimu huku familia ya marehemu ikipokea shilingi milioni tano,shirika hilo la biashara latoa ofa kwa sasa hunuua karafuu kilo moja shilingi 14,000.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top