Licha ya Rais Magufuli kuwasisitiza TANESCO kuepukana na mikataba ya "ajabu ajabu" na kulitia Taifa na shirika hasara,bado TANESCO mwezi Desemba walisaini mkataba wa miaka 15 na kampuni ya Symbion,na baada ya "agizo" hilo la Rais wakati akifungua mitambo ya umeme wa Gas wa Kinyerezi
Hali hiyo imefikia Tanesco kuamua "kusitisha" aina yoyote ya mahusiano ya kimkataba na kampuni ya Symbion,hivyo kuifanya Symbion kuchukua hatua zaidi za kuipeleka Tanesco Mahakamani.Kila mwezi Tanesco hulipa karibu shilingi bilioni 36 kwa makampuni ambayo imeingia nayo mkataba wa kuzalisha umeme,malipo hayo ni kwa ajili ya 'Capacity Charge" kitu ambacho huliingiza Taifa na shirika lenyewe hasara kubwa na kuongeza mzigo wa malipo kwa wananchi wa chini
Wakati Tanesco ikichukua maamuzi hayo chini ya "influence" ya Rais,wao Symbion wanasema hawautambui msimamo huo mpya wa Tanesco kwani Desemba mwaka wa jana 2015,Symbion na Tanesco walishaingia kwenye mkataba wa miaka 15 wa Symbion kuliuzia Shirika la Umeme Tanzania kiwango cha umeme.
Management ya Symbion imechukuwa hatua ya kuifikisha Tanesco mahakamani ili kuishinikiza iweze kuendelea na mkataba huo ambao Symbion ingemuuzia Tanesco umeme kwa miaka 15.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies