Kutokana na ripoti hii ya Benki ya Dunia ya Uchumi toleo la nane (8) kwa Tanzania, inaonyesha kuwa ndani ya miaka 10 iliyopita, Uchumi umekua na kufanya idadi ya watu wanaoishi chini ya Dola moja kufikia milioni 12. Bado uwekezaji mkubwa (wa miundo mbinu na Watendaji) unatakiwa kufanywa ili kuboresha maisha ya Watanzania wanaoishi katika maisha duni.
Ripoti hii (miongoni mwa taarifa nyingine), inatoa msisitizo wa umuhimu wa kuwekeza katika Sekta Binafsi kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi na umuhimu wa Serikali kutambua sekta hiyo.
1. Miradi ya Sekta binafsi inatakiwa kuchaguliwa kwa umakini mkubwa kwa misingi ya kiasi cha pesa kinachopaswa kutumika na mvuto wa mradi huo kwa sekta binafsi.
2. Miradi iliyochaguliwa inatakiwa iwe imeandaliwa vema, ikiwa na matumizi sahihi na watu sahihi wa kuiendesha ikiwa pamoja na ushauri na ushiriki wa Wataalam katika miradi hiyo.
3. Miradi inayotolewa bila ushindani wa wadau na uwazi, ina uwezekano mdogo wa mafanikio. Wahisani wanapaswa kushirikisha wadau wengi ili kujenga ushindani wa kuweza kupata watu bora zaidi kuendesha miradi.
4. Kiwango kikubwa cha ushiriki wa serikali ni chambo kikubwa cha kuhakikisha kufanikiwa kwa miradi ya sekta binafsi. Hata hivyo serikali kuingilia katika maamuzi ya miradi hiyo katika ngazi ya chini inachangia kwa uwezekano mkubwa wa miradi hiyo kutokuwa na mafanikio.
5. Miradi iliyopangiliwa vema, ikiwa na mikakati sahihi pamoja na kampeni za kuifikia jamii juu ya kile ambacho mradi huo unafanya inachangia kujenga ufahamu katika jamii na pia maelewano mazuri katika ya serikali na sekta binafsi.
Kufuatilia uzinduzi huo wa Uchumi (8th Tanzania Economic Update: The Road Less Travelled - Unleashing Public Private Partnerships in Tanzania) fuatilia live kupitia live stream channel hii - The World Bank: 8th Tanzania Economic Update on Livestream
Pia unaweza kupata updates ya tukio hili kupitia timeline yetu ya Twitter (Jamii Forums (@JamiiForums) | Twitter) au fuatilia hashtag ya #TzEU8 #TZEconomy.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies