Mwenyekiti wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mh.Rais Dr,John Pombe Magufuli ameongoza wakuu wa nchi hizo kuzindua ujenzi wa barabara ya km 234.3 inayoanzia Arusha hadi Holili nchini Kenya na kuwataka kutumia rasilimali zilizopo kuimarisha na kuboresha maisha ya wananchiumaskini badala ya kuimarisha misingi ya kisiasa.
Akizungumza katika hafla hiyo Mh.Rais Magufuli amesema kimsingi mahitaji ya wananchi katika nchi zote ni kupata maendeleo na sio siasa hivyo wasiogope kufanya maamuzi yenye maslahi ya wengi na amewataka wananchi wa maeneo itanapotekelezwa miradi ya maendeleo ukiwemo wa barabara kutoa ushirikiano.
Aidha amesema kwa upande wake hatamuonea huruma mtu yeyote anayetumia rasilimali ama madaraka yake kuwajinufaisha wakati walio wengi wanateseka na kwamba amejitolea muhanga kwa ajili ya wamilioni ya watu maskini wanaoteseka.
Kwa upande wake rais Uhuru Kenyeta na Yoweri Museven wa Uganda wamesema umaskini unaowaandama wananchi katika nchi nyingi zikiwemo za Afrika Mashariki unachangiwa na udhaifu wa viongozi na watendaji wa serikali na licha ya kumpongeza rais Magufuli kwa kuanza kushughulikia tatizo hilo wamesisitiza umuhimu wa viongozi kubadadilika.
Awali katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dr.Richerd amesema na balozi wa Japan nchini Masahalu Yoshida wamesema ujenzi wa miundombinu ya barabara unaendelea kurahisisha mawasiliano kwa nchi wanachama huku mwakilishi wa Benk ya dunia akisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuishirikisha na kuiwezesha sekta binafsi katika ujenzi wa miundimbinu.