Kukiwa kumesalia wiki mbili kabla ya marudio ya uchaguzi mkuu Zanzibar wakaazi wa maeneo ya michenzani na walio karibu na maeneo hayo wamekumbwa na hofu kubwa baada ya bomu kulipuka usiku wa kuamkia leo na kuzua tafrani kubwa.
Bomu hilo ambalo hadi sasa halijathibitishwa kama ni la kivita au la kutengenezwa hapa nchini limelipuka katika eneo la Maskani ya CCM ya Kisonge na kuharibu Kontena kubwa la Maskani hiyo na kupasua vioo vya madirisha ya baadhi ya nyumba za maendeleo za michenzani ,hata hivyo hakuna mtu aliyeumia na kulipuka kwa bomu hilo na Kontena hilo lilikuwa tupu.
ITV ilifika katika eneo hilo na kushuhudia askari wa upelelezi wa jeshi la polisi wakiwa katika harakati za upelelezi na kukusanya vitu amabvyo huenda vikawa vinahusiana na kulipuka kwa bomu hilo,mmoja wa kijana aliyejitambulisha kwa jina la Shababi Said Mtamanya amedai kuwoana baadhi ya watu wakiwa na gari dogo lawazi wengine wakiwa wamefunika nyuso zao katika eneo hilo la Kontenna na baadaaye kuondoka kwa mwendo wa kasi.
Wakti polisi wakiendelea na uchuguzi wao makamu wa pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi alifika katika eneo hilo na kukagua na kuangalia athari za kulipuka kwa bomu hilo ambapo akizungumza na itv amesema seriklai inalaani kitendo hicho amabacho kinahatarisha amani ya nchi h uku akiahidi serikali itaendelea kuhakikisha hali ya amani na utulivu inaendelea.
Naibu mkurugenzi wa upelelezi na makosa ya jinai Zanzibar kamishna msaidizi Salum Msangi akiongea na ITV amesema polisi imeshaanza kazi yake kwa asilimia 70 na kutoa onyo kali.
Hili ni tukio la kwanza la Ulipuaji wa mabomu kwa mwaka 2016 wakati Zanzibar ikijiandaa kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwakaa huu.