Hatimaye mgogoro wa ardhi wa wakazi wa chasimba,cha hui na cha tembo uliodumu kwa muda mrefu umetatuliwa rasmi na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mh.wilium lukuvi baada ya kufanya mazungumzo na mwekezaji wa kiwanda cha cement na kukubali kuwapa hekta 224 watakazo gawiwa na kupewa hati miliki.
Mh.lukuvi akizungumza katika mkutano na wananchi wa cha simba cha chui na cha tembo akisindikizwa na viongozi wengine wa majimbo na mitaa amesema licha ya mwekezaji kushinda keshi ya kumiliki eneo lote la ardhi yao amekubali kuwapa hekta 224 ikiwa ni jitihada za waziri na kufanya nae mazingumzo ambapo amewataka wananchi hao sasa kutambua kuwa maeneo watakayopangiwa wataishi kwa amani.
Mh mbunge saidi kubenea akimwakilisha mbunge wa jimbo la kawe mh halima mdee alikasirishwa na hatua ya wananchi hao kugoma kutoa shiling elfu kumi kama fedha ya kusaidia zoezi la kupima viwanja hivyo na kuwatahadharisha endepo zoezi hilo likikwama basi itakuwa wamejitakiwa wenyewe kuendelea kuwa wakimbizi.
Nao baadhi ya wakazi wa maeneo hayo licha ya kumshukuru mh waziri wa ardhi wamesema sasa wanaweza kufanya shughuli za kimaendeleo na kujikwamua kiuchumi.