Asilimia 40 ya wakazi Dodoma hawana Mawasiliano.
Zaidi asilimia 40 ya wakazi waishio vijijini Mkoani Dodoma bado hawajafikiwa na huduma ya mawasiliano ikiwemo mitandao wa simu za mkoanoni hali inayodaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa wananchi hao kushindwa kupata taarifa muhumu zikiwemo, za kilimo, hali ya hewa, uchumi na afya na kushindwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na kuendelea kuishi katika lindi la umasikini uliobobea.
Wakati dunia ikitajwa kuwa kama kijiji kufuatia mapinduzui makubwa ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano kwa kuwezesha mamilioni ya watu kupata taarifa kwa haraka lakini mkoani hapa bado wananchi zaidi ya asilimia 40 hawajafikiwa na huduma za mawasiliano ya simu na mtandao hatua inayodaiwa kuchangia kuzorotesha shughuli mbalimbali za kijamii, uchumi na afya huku wadau wa sekta hiyo akiwemo meneja wa TTCL mkoa wa Dodoma Mhandisi Ekaeli Manase wakitoa tahadhari kuhusu hali hiyo.
Wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa eneo ambalo vijiji vyake vinakabiliwa na changamoto hiyo ya ukosefu wa mawasiliano ambapo mmoja kati ya wakazi wa kijiji cha Ving’awe anasema asilimia kubwa hawaoni umuhimu wa mawasilimo kutokana na kutokuwa na elimu huku mamlaka husika zikishindwa kusisitiza makampuni yanayotoa huduma hizo kuwafikia wakazi hao kwa kigezo cha kutokuwepo kwa wateja.
Nao baadhi ya watoa huduma za mitandao ya simu na mawasiliano ya intaneti wanasema changamoto kuwba wanayokabiliana nayo ni hali mbaya ya jiografia kwenye maeneo ya vijijini pamoja na kukosekana kwa miundombinu ya uhakika ya barabara na umeme hali inayowawia vigumu kusambaa kwa haraka kwenye maeneo hayo na gharama kubwa ya vifaa vya mawasiliano.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies