Featured

    Featured Posts

Loading...

WIZI WA UMEME JIJINI MWANZA WAENDELEA KUSHIKA KASI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Zaidi ya nyumba 100 Ilemela zimekamatwa kwa tuhuma za kujiunganishia umeme.

Zaidi ya nyumba 100 katika mtaa wa Bulyehele wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza zimekutwa zikitumia umeme kwa njia ya wizi, baada ya mafundi wa shirika la ugavi wa umeme (Tanesco) mkoani humo kufanya ukaguzi wa kushtukiza na kukuta baadhi ya nyaya zilizokuwa zinatumika kusambaza umeme huo kwa wananchi zikiwa zimechimbiwa ardhini.

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Bulyehele Peter Nkomba anasema sababu kubwa ya baadhi ya wananchi kujihusisha na wizi wa umeme ni kutokana na urasimu unaosababishwa na baadhi ya watendaji wa Tanesco, huku Bi. Siwema Kenedy mkazi wa mtaa huo akieleza wasiwasi wake juu ya hatari ya kuchimbia nyaya za umeme chini ya ardhi hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.

John Chilale ni afisa usalama wa Tanesco mkoa wa Mwanza, anatoa angalizo kwa wananchi kuacha kujiunganishia umeme kinyemela, kwani hali hiyo inachangia kupoteza mapato ya shirika na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini baadhi ya watu wanaolihujumu shirika hilo, ambapo afisa wa kitengo cha kudhibiti mapato wa Tanesco mkoa wa Mwanza Mhandisi King Fokanya amesema wamebaini kuwa umeme huo umekuwa ukisambazwa kwenye nyumba hizo zaidi ya 100 na wateja halali watatu walio na mita zinazotambulika na shirika hilo. 

Tangu kuanza kwa operesheni inayojulikana kama ‘kamata wezi wa umeme (kaweu) mwezi Desemba mwaka jana, zaidi ya watu 18 mkoani Mwanza wamekamatwa na shirika hilo kwa tuhuma za kujiunganishia umeme bila kufuata taratibu za Tanesco na kulisababishia shirika hilo hasara ya zaidi ya shilingi milioni 20.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top