Wananchi wa kata ya Ndongosi watembea kilomita 5 kutafuta mawasiliano ya simu.
Wananchi waishio katika kata ya Ndongosi iliyoko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wamelalamikia kukosa mawasiliano ya simu ambapo wamekuwa wakitembea kilomita tano kufuata eneo lenye mtandao wa simu ambako hupanda juu ya miti ili kuweza kuwasiliana na ndugu zao.
Wakizungumza na Mutalemwa Blog katika eneo yanakopatikana mawasiliano ya simu ambalo wamelipa jina la mtandaoni ambako husafiri kilomita tano kutoka makao makuu ya kata na hupanda juu ya miti ili kuweza kupata mawasiliano ya simu wamesema kuwa kukosekana kwa mawasiliano ya simu kunawafanya washindwe kuwasiliana na ndugu zao pindi wanapoata matatizo.
Wameiomba serikali kwa kushirikiana na na makampuni ya simu za mkononi kuwejengea minara ya simu ili waweze kupata mawasiliano ya simu.
Akizungumza na wananchi hao mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Benson Mpesya ambaye wananchi hao wa kata ya Ndongosi wamempongeza kwa ujio wake wakidai kuwa hawajawahi kutembelewa na kiongozi kwa miaka mitano amesema tatizo la kukosa mawasiliano ya simu amelichukua na atalifanyia kazi.