Kampuni ya India imezindua simu janja 'smartphone' yenye gharama nafuu zaidi duniani. Kampuni ya 'Ringing Bells imesema simu yao ya freedom 251 itagharimu rupia 251 pekee(dola 3.6 za kimarekani sawa na Tshs 8,012) na kulitokea hitaji kubwa sana ndani ya saa moja tangu mauzo kufunguliwa.
India ni soko la pili la simu kwa ukubwa duniani na lina matumizi ya simu bilioni moja, Freedom inarajiwa kulenga soko ambalo tayari limetawaliwa na simu za bei rahisi.
Simu hio ina uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu ya GB 8 na kamera nyuma na mbele na toleo hio linafanana na iPhone 4 ikiwemo kitufe cha nyumbani 'Home button'.
Simu hiyo ilianza kuuzwa Alhamisi asubuhi lakini masaa machache baadae, kampuni ilisitisha kupokea oda baada ya tovuti yao kutofanya kazi kutokana na hitaji kubwa: Ilikuwa inatembelewa mara 600,000 kwa sekunde.
Kampuni ya Ringing Bels ilisema itatengeza simu zao ndani ya nchi hiyo japo bado haina kiwanda nchini India. Mifano waliyopewa waandishi ilikuwa ya simu za kichina zenye jina la Adcom na ikiwa na rangi nyeupe. Imeahidi kuanza kutoa simu hizo kwenye kipindi cha miezi minne.
"Inaonekana kampuni imeitolea ruzuku kubwa na haijawa sawa jinsi gani wamejipanga kubakia nayo" Tarun Pathak aliiambia Reuters ambae anatokea kampuni ya utafiti ya Counterpoint Technology.