Kwanza ni kwamba mawaziri wote 4 na naibu waziri wamezirudisha fomu jana kabla ya saa 10 jioni. Na kila mmoja alikua na sababu zake kama ifuatavyo.
1. Makamba: Anasema huwa anamtumia mwanasheria wake kuzipeleka fomu zake kila anapo jaza lakini kwa wakati huu mwanasheria wake alikua na udhuru wa muda mrefu na aliye mtuma hakufanya hivyo. Makamba amezipeleka fomu zote jana kwa kutumia mwakilishi wake kabla ya saa 10 jioni.
2. Dr Mahiga: Anasema yeye alibanwa na majukumu hasa safari za nje hivyo kushindwa kupata muda wa kuzipeleka fomu hizo tume japo amekiri kuwa agizo la Rais limetoa somo zuri kuhakikisha kila jambo linafanyika kwa wakati.
3. Kitwanga: Yeye anasema fomu zake alizipeleka toka tarehe 4 january na ameshangaa kwamba anatajwa japo jana baada ya tume ya maadili kuzitafuta zilipatikana.
4. Mpina: Yeye anasema ameshindwa kupeleka fomu kutokana na kuto jua mshahara wake. Amekiri kuwa inaonyesha Rais pamoja na kujua sababu aliyo kuwa nayo bado alimpa masaa 12 kupeleka hizo fomu kiashiria kwamba sababu zake Rais hakuzikubali.
Jana hiyohiyo alimwita mhasibu na kujua mshahara wake na fomu akazirudisha.
5. Dr ndarichako sababu zake hazija patikana japo naye jana hiyohiyo alituma mwakilishi kuzirudisha fomu zote tume ya maadili.