Jeshi la polisi lakamata kontena la ving’amuzi feki visiwani Zanzibar.
Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kukamata kontena liloingizwa Zanzibar likiwa na vingamuzi feki zaidi ya 1000 kutoka China ambavyo vilikuwa viingizwe sokoni.
Kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa upelelezi na makosa ya jinai Zanzibar kamishna msaidizi Salum Msangi amesema polisi kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa Interpol na kampuni ya kimatiafa ya ushauri wa kulinda alama za biashara kontena hilo limenaswa bandarini Zanzibar na kukutwa na vingamuzi hivyo vilivyokuwa na lebo za Singsung na Blackstone ambavyo vyote vilikuwa ni feki na polisi inaendelea kuwasilaina na makampuni husika.
DCI Salum Msangi pia katika mkutano huo ametahadharisha jamii kuwa jeshi hilo litaanza kuwachukulia hatua bahadhi ya watu na mitandao ambayo imekuwa ikitukana viongozi na kutoa lugha za matusi na polisi imeanza kuchukua hatua hizo.
Hatua hizo za polisi zimekuja wakati pamekuwapo na malalamiko ya Zanzibar kutumika kwa kuingiza vyakula na vifaa vya umeme ambavyo ni feki na pia bandari na uwanja wa ndege wa Zanzibar kutumika kusafirisha madawa ya kulevya ambapo jehsi hilo pia limefanikiwa kuwakmata watu wawili akiwemo raia wa Ethiopia waliongiza madawa ya aina ya Mirungi kwa njia ya kukausha.