Mbali yakuwepo mzozo kwa wabunge na wananchi kuhusu urushwaji wa bunge live kwenye television ya taifa Tbc, sasa baadhi ya vyombo vya habari binafsi vimetambua umuhimu wa kupata habari kwa wakati juu ya wananchi wataifa hili. Vyombo hivyo vinavyorusha matangazo ya bunge mpaka sasa ni pamoja na Star bunge, Azam Tv, 87.5 kwa wakazi wa Dar nk.
Habari za leo ndugu zangu, naomba tujadiliane kuhusu ile taarifa iliyotolewa na Mh.Nape juu ya kutorushwa kwa shughuli za bunge live na Television ya Taifa TBC na badala yake kuwepo na kipindi maalum kinachoitwa "Leo katika bunge" ambacho kitakuwa kinarushwa kikiwa recorded, je unafikili kufanya hivyo ni sawa??
Mimi kwa upande wangu naona kwamba kitendo cha mh.Nape kuamua kufanya hivyo nikujaribu kupunguza madudu wanayoyafanya baadhi ya wange pindi wanapokuwa ndani ya bunge. Kwa maana yakwamba kama kipindi kitakuwa kinarecodiwa kisha kueditiwa yale yote mambo watakaokuwa wameyafanya baadhi ya wabunge ambayo niyakulidhalilisha bunge basi yatakuwa yanaondolewa kisha wananchi tunaoneshwa yale yaliyomazuri.
Lakini kwa upande mwingime ilo litakuwa sio suruhisho juu ya nidhamu kwa wabunge, chamsingi ni kuwaonyesha wananchi live juu ya kile kinachokuwa kikifanyika ndani ya ukumbi wa bunge.
Ili wananchi wenyewe waweze kuwaukumu wabunge wao kutokana na vile wanavyovifanya pindi wawapo bungeni. Kurusha recorded edited report haisaidii hata kidogo, maana kufanya hivyo ni kuficha maovu ya baadhi ya wahusika.
Ni nini maoni yako?