Featured

    Featured Posts

Loading...

CCM YAHUSISHWA KATIKA MAUAJI YA DIWANI MULIGA.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Ivi kuna ukweli wowote juu ya habari hii?? Kijana huyu anaitwa "Simon Shilage" ana umri wa miaka 22, Kabila Msukuma. Yeye kwa kushirikiana na mwenzie mmoja ambaye bado hajapatikana ndio waliomuua Diwani wa kata ya Kimwai huko Muleba Ndg.Faustine Muliga wa chama cha wananchi CUF.

Kijana huyu amekamatwa jioni ya leo na wananchi wa kijiji cha Kyota akijaribu kutoroka. Amekutwa na panga lenye damu alilotumia kumuua diwani Muliga. Alipohojiwa amekiri kwamba ni kweli yeye na mwenzie mmoja (hakumtaja jina) ndio waliomuua Mhe.Muliga kwa kumkata mapanga.

Amesema kazi hiyo walitumwa na aliyekua mgombea udiwani wa Kata hiyo kwa ticket ya CCM kwenye uchaguzi uliopita, ambaye alikua mpinzani wa Muliga lakini alishindwa kwenye uchaguzi.

Ameongeza kuwa Mgombea huyo wa CCM aliwaahidi kiasi cha shilingi milioni 1.5 ikiwa watafanikiwa kumuua Muliga na aliwapa "advance" ya shilingi laki moja na nusu (150,000/=).

Baada ya makubaliano hayo vijana hao walimvamia Muliga nyumbani kwake majira ya saa 2 usiku akiangalia "Taarifa ya Habari" ambapo walimkata mapanga maeneo mbalimbali mwilini mwake kabla ya kutokomea kusikojulikana.

Kijana huyu amekamatwa leo na wananchi wenye hasira kali ambao walitaka kumuua lakini akaokolewa na Polisi. Hata hivyo wananchi hao walifanikiwa kumkata sikio lake moja la kushoto kama anavyoonekana pichani.

Kwa sasa anashikiliwa kituo cha Polisi Muleba kwa upelelezi, kabla ya kupandishwa Mahakamani kujibu tuhuma za Mauaji.

Chanzo: Bakeza Amwesiga.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top