Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

NAIBU WAZIRI ASITISHA MKATABA WA KAZI WA MWENYEKITI WA BARAZA LA ARDHI CHATO, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Naibu waziri asitisha mkataba wa kazi wa mwenyekiti wa baraza la ardhi chato ili apishe uchunguzi.

Naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi,Angeline Mabula amesitisha mkataba wa kazi wa Emmanuel Mogasa ambaye Mwenyekiti wa baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya chato iliyoko mkoani Geita mkoa ili apishe uchunguzi wa tuhuma zinazochunguzwa juu  yake  za kujihusisha na vitendo vya rushwa katika kutoa maamuzi ya mashauri yanayofikishwa katika baraza hilo.

Naibu waziri huyo ametoa maamuzi hayo baada ya kupokea taarifa toka kwa mwenyeti huyo ambayo ilikuwa inaelezea mwenendo mzima wa utendaji wa kazi wa baraza hilo.

Amesema amesitisha mkataba wa kazi wa Mogasa na hivyo atakuwa nje ya ofisi hadi uchunguzi wa tuhuma zinazomhusu utakapokamilika na pia ametoa onyo kwa watendaji idara ya ardhi wa halmashauri ya wilaya ya chato na kutaka wampe taarifa juu ya matumizi ya shilingi zaidi milioni 32 zilizotolewa na wizara kama mkopo kwa ajili ya upimaji wa viwanja wilayani humo ambao hadi sasa haurejeshwa wizarani kulingana na makubalino.

Katika hatua nyingine naibu waziri huyo ameziagiza halmashauri za wilaya na manispaa kuhakikisha  zinatenga viwanja vitakaloliwezesha shirika la nyumba la taifa kujenga bora kwa  gharama nafuu ili nyumba zinazijengwa zinazojengwa na ziwe na unafuu kodi, ametoa agizo hilo baada ya kukagua nyumba zilizojengwa na shirika hilo wilayani chato na muleba mkoani kagera.

Naye,Deogratias Batakanwa ambaye ni meneja wa shirika la nyumba mkoani Kagera na wilaya ya chato ambayo zamani ilikuwa mkoani humo kabla ya kuundwa kwa mkoa wa Geita,ameelezea idadi ya nyumba ambazo shirika hilo limezijenga mkoani Kagera na wilaya changamoto inayokabili ujenzi wa nyumba hizo.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top